SURA YA TATU
HUKUMU YA NUN SAKINA NA TANWIN
KUKUMU ZA NUWN SAAKINAH NA TANWIYN.
Nuwn saakinah: Ni herufi ya nuwn نْ isiyokuwa na i’raab ambayo huthibiti katika kutamkwa, kuandikwa, kusimama na katika kuunganisha. Tanwiyn: Ni nuwn saakinah iliyozidi inapatikana mwisho wa nomino kwa kutamkwa wakati wa kuunganisha na hutengamana na hiyo nomino wakati wa kuandika na kusimama.(al-hidaayah.com).

Wataalamu wa Tajwid wanaeleza hukumu nne pindi nuwn sakinah na tanwiyn zinapokutana. Hukumu hizo ni:-
1. الإِظْهاَرْ AL-IDHWHAAR - KUDHIHIRISHA.
Maana yake ni kukibainisha kitu wazi. Katika hukmu za Tajwiyd ni kuitoa kila herufi katika makhraj yake bila ya kuweko na ghunnah. Nayo hutokea pale Nuwn saakinah au tanwiyn inapofuatiwa na mojawapo wa herufi sita za al-halq (koo) ambazo ء ه ح خ ع غ
Bofya kitufe cha MFANO 01, MFANO02,kusikiliza mfano
Mifano.
NUN SAKINA
NUN SAKINA
www.al-hidaayah.com

II- الإِدْغاَم AL-IDGHAAM – KUINGIZA, KUCHANGANYA.
Idghaam ni kuingiza kitu kwenye kitu. Katika hukmu za Tajwiyd ni kuingiza herufi saakin kwenye herufi yenye i’raab na kuzipelekea herufi mbili hizi kuwa herufi moja ya pili nzito. Na hutokea pale nuwn saakinah au tanwiyn inapofuatiwa na moja ya herufi sita za idghambazo ni ي ر م ل ن و

Sharti za idgham.
Idgham sikuzote inafanyika kwenye maneno mawili tu. Herufi ya mwisho ya neno la kwanza iwe na atnwiyn au nun sakina na herufi ya kwanza ya neno linalofata iwe ni moja ya herufi za idgham zilizotajwa hapo juu.

Sasa ikitokea nun sakina au tanwiyn zimekutana na moja ya herufi hizi za idgam katika neno moja hapa kinachotakiwa ni kuleta idhhar kwenye nun sakina au tanwiyn. Na hii idhwhaari ndiyo inayoitwa idhwhaar mutlaqa yaani idhwhaar halisi.katika qurani kuna maneno manne tu ambayo kuna idhwhaar tutlaqa.
NUN SAKINA

Aina za idgham.
1.idgham bighunnah
Idghaam bighunnah ni kuingiza nuwn saakinah au tanwiyn kwenye herufi za ي ن م و pamoja na kuleta ghunnah inayotokea puani. Na hii hutokea pale nun sakina na tanwiyn zinapokutana na moja ya herufi hizo nne.
NUN SAKINA

2.Idghaamu bighayri ghunnah
ة" إِدْغَامُ بِغَيْرِ غُن (Idghaamu bighayri ghunnah) ni kuitia na kuichanganya nuwn saakinah au tanwiyn katika herufi za ر ل bila ya kuleta ghunnah inayotokea puani.
NUN SAKINA
Makundi mengine ya idgham.
1.Idghaamu Kaamil
Hii huitwa idgham iliyokamilika ambayo pia inaweza kugawanyika katika makundi mawili ambayo ni;-
idgham kaamil bighunnah.: Hii hutokea pale nun sakina au tanwiyn zinapokutana na ن na م . Hapa kutakuwa na idgham pamoja na kutia ghunnah yaani kunung’unisha nun sakina au tanwiyn.
Idghaamu Kaamil Bighayri Ghunnah: hii hutokea pale nun sakina au tanwiyn inapokutana na ر ل. Hapa kutakuwa na idgham ila bila ya kunung’unisha nun sakina au tanwiyn.

Mifano ya idgham kaamil
NUN SAKINA

2.idghaamu naaqisw.
Hii hutwa idghamu iliyopunguwa, na hutokea pale nun sakina au tanwiyn inapokutana na و ي. Imeiytwa ni pungufu kwa sababu inakuwepo idgham bila ya kupoteza sifa ya nun sakina au tanwin.
Mifano:
NUN SAKINA
Bofya kitufe cha MFANO 03, kusikiliza mfano

III- الإقْلاَبْ AL-IQLAAB - KUGEUZA.
Maana yake ni kugeuza kitu na kinavyotakiwa kuwa au kupindua kitu. Katika hukmu za Tajwiyd ni kuigeuza nuwn saakinah au tanwiyn kwa kuitamka kama ni م (miym) pamoja na kuleta ghunnah.. (www.alhidaayah.com). Hukumu hii inapatikana pale tu nun sakina au tanwiyn inapokutana na ب (baa) tu. Hivyo herufi ya iqlab ni moja tu.
NUN SAKINA
NUN SAKINA

III- الإِخِفاء AL-IKHFAA - KUFICHA
Katika hukmu za Tajwiyd ni kuificha nuwn saakinah au tanwiyn katika herufi za ikhfaa. Hivyo nuwn saakinah au tanwiyn itatamkwa ikiwa baina ya idhwhaar na idghaam kwa kuipa ghunnah isiyokuwa na shaddah. Hukumu hii inapatikana pale nun sakina au tanwiyn inapokutana na moja ya herufi hizi ث ج د ذ ز س ش ص ض ط ظ ف ق ك
NUN SAKINA
Bofya kitufe cha MFANO 04,MFANO 05 na MFANO 06, kusikiliza mfano