image

Vyakula vya madini kwa wingi, na kazi za madini mwilini

Utajifunza vyakula vyenye madini kwa wingi, kazi za madini mwilini na athari za upungufu wake

Vyakula vya madini kwa wingi, na kazi za madini mwilini

VYAKULA VYA MADINI KWA WINGI
Madini ni katika virutubisho ambavyo huhitajika katika kuhakikisha kuwa mwili unabakia kati aafya njema.mwili unahitaji madini kwa ajili ya kuimarisha afya ya moyo, mishia, misuli na maeneo mengine ya mwili. Madini tunaweza kuyapata kutoka kwenye vyakula tunavyokula kama mboga za majani, nyama, matunda na nafaka zingine. Je ungependa kujuwa vyakula hivyo ama vyanzo vya madini? Na je ungependa kujuwa ni zipi hasa kazi za madini katika miili yetu?. makala hii ni kwa ajili yako, hapa utakwenda kujifunza mengi kuhusu somo hili.



Kabla ya kuona vyakula hivyo kwanza ningepata kukujuza kazi kuu za virutubisho vya madini kwenye miili yetu. Madini yamegawanyika katika aina kuu mbili kuna ambayo yanahitajika kwa wingi katika miili yetu na kuna ambayo yanahitajika kwa kiasi kidogo. Kwa ujumla madini yana kazi kuu zifuatazo:-



KAZI ZA MADINI MWILINI
1. Madini hutumika kwa ajili ya kudhibiti kiwango cha majimaji kwenye mwili kama madini ya sodium au chumvi


2. Huhitajika madini kwa ajili ya utengenezwaji wa asidi mbalimbali kama asidi ya hydrocloric kama madini ya chloride na phpsphprus


3. Husaidia katika kudhibiti kiwangi cha uzalishaji wa tindikali mwilini kama tindikali ya hydrocloric kama madini ya chloride


4. Husaidia katika usafirishwaji wa taarifa kutoka sehemu moja ya mwili kwenda sehemu nyingine kama madini ya sodium na potassium


5. Husaidia katika ujongeaji wa mishipa kama madini ya sodium na cailcium


6. Madini huhitajika kwa ajili ya kuimarisha afya ya mifupa, misuli, mishipa, meno na moyo kama madini ya calcium na magnesium


7. Huhitajika madini kwa ajili ya kuganda kwa damu maeneo yenye majeraha kama madini ya calcium na phosphorus


8. Huhitajika madini kwa ajili ya kuimarisha mfumo wa kinga mwilini kama madini ya calcium


9. Huhitajika katika utengenezwaji wa hemoglobin chembechembe nyekundu za damu kama madini ya chuma


10. Huhitajika katika kutengeneza protini na genetics material, huhitajika katika utengenezwaji wa manii na ni muhimu katika mfumo wa uzalishaji kwa mfano madini ya zinc



VYAKULA VYENYE MADINI KWA WINGI
Kwa kuwa umesha jifunza kazi za madini zilizotajwa hapo juu, basi tambuwa kuwa kuna aina nyingi za madini ambazo baadhi yake zimetajwa hapo juu. Madini haya unaweza kuyapata kwenye mchanganyiko wa vyakula vingi. Lakini kuna vyakula ambavyo madini huwa ni mengi kuliko vyakula vingine. Hapa chini ninakuletea vyakula ambavyo vina madini kwa wingi ambavyo ni:-



1. Kwenye mbegu kama mbegu za maboga. Mbegu za maboga zina madini mengi sana. Unaweza kula mbegu za maboga kwa kutafuna, kutumia unga wake kama kiungo cha mboga ama kukaanga na kula kama bisi. Mbegu za maboga na m,begu nyingine zenye mfano wake kama mbegu za matango zina madini kama magnesium, zinc, manganese, copper, selenium, na madini ya phosphorus.



2. Kwenye samaki hasa samaki wenye magamba magumu kama kobe (shellfish) jamii ya tondo. Kama umeshawahi kula tondo, utakuwa unaelewa nini klimaamnishwa.kama hutambui nitakujuza. Angalia mfano wa konokono, basi samaki wenye kufanana na konokono wanatembea na majumba yao, ukimshituwa anaingia ndani. Samaki hawa ndio wanaozungumziwa hapa. Samaki hawa wana madini kama selenium, zinc, copper na chuma



3. Mboga za majani jamii ya kabichi. Mboga hizi zina madini kama magnesium, potassium, manganese na calcium



4. Kwenye nyama hasa nyama za viungo maalumu kama maini na figo. Nyama hizi zina madini kama selenium, zinc, madini ya chuma, na phosphorus.



5. Mayai ni moja kati ya vyakula vyema virutubisho vingi sana. Katika mayai kuna madini ya chuma kwa wingi sana, phosphorus, zinc na selenium.



6. Maharagwe, maharage ya na madini kama cailcium, magnesium, madini ya chuma, phosphorus,potassium, madini ya shaba na zinc.



7. Palachichi, tunda hili lina madini kama magnesium, potasium, manganese na madini ya shaba.



8. Maziwa yana madini kama cailcium, potassium, phosphorus, zinc na selenium.



9. Viazi mbatat vina madii kama potassium, magnesium, manganese, calcium, madini ya chuma na madini ya shaba.



10. Pia madini kama potassium, manganese, shamba na magnesium tunaweza kuyapata kwenye matunda kama, ndizi, fenesi, machungwa, pasheni, nanasi na mapera.



ORODHA YA MADINI NA CHANZO CHAKE NA FAIDA ZAKE.
Kwa ufupi ninakuletea orodha ya madini mablimbali na vyakula ambavyo hupatikana. Pia utajifunza kazi za kila aina ya dini ndani ya miili yetu.

1. Madini ya sodium (table salt) Madini haya unaweza kuyapata kwenye spinach, maharage,punje za maboga n.k.



2.Madini ya chuma. Haya hupatikana kwenye maini, nyama, maharage, na mboga za majani. Madini haya ni muhimu kwa utengenezwaji wa hemoglobin yaani chembechembe nyekundu za damu.


3.Madini ya kashiam(calcium). Haya hupatikana kwenye maziwa,maini, mboga za majani na cheese. Madini haya husaidia katika uimarishwaji wa mifupa, meno, misuli na utengenezwaji wa neva. Husaidia piaa kuwezesha kuganda kwa damu kwenye majeraha. Husaidia katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula kwa kuzifanya enzymes kuwa active.



4. Madini ya phosphorus, haya hupatikana kwenye nyama, maziwa, samaki, na mayai. Husaidia katika uimarishwaji wa mifupa, meno,misuli na shughuli za mfumo wa fahamu na utengenezwajiwa genetic materials.



5. Madini ya Potashiam (potassium) Hupatikana kwenye ndizi, machungwa,nyama na kaa. husaidia katika kurekebisha kiwango cha majimaji mwilini.



6.Madini yakopa ( copper) Haya hupatikana kwenye nyama, samaki, na maini.husaidia katika mifupa na utengenezwaji wa hemoglobin (chembechembe nyekundu za damu).



7.Madini yamanganese Madini haya hupatikana kwenye figo,maini, chai na kahawa. Husaidia katika utengenezwaji wa mifupa, na katika mmeng'enyo wa chakula kwa kufanya enzymes ziwe active.



8.Madini ya iodine Madini haya hupatikana kwenye chumvi na vyakula vya baharini kama samaki. Husaidia katika uzalishaji wa homoni ya thyroid.






                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 3412


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Faida za kiafya za kula nyama
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula nyama Soma Zaidi...

Faida za kiafya za topetope (accustard apple/sweetsop)
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula topetope Soma Zaidi...

Vyakula vya vitamin E
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya vitamin E Soma Zaidi...

Faida za kula mayai
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kula mayai Soma Zaidi...

Faida za kula Tango
Matunda ya zamani na ya asili, zijuwe faida za kiafya za tango Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Nazi
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula kitunguu thaumu
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kitunguu thaumu Soma Zaidi...

Fahamau protini na kazi zake, vyakula vya protini, na athari za upungufu wake.
unayopaswa kuyajuwa kuhusu protini na vyakula vya protini, faida zake na hasara zake. Madhara ya kiafya yanayohusiana na protini pamoja na kuyaepuka madhara hayo Soma Zaidi...

Faida za kunywa maji kabla ya kula chochote.
Posti hii inahusu faida za kunywa maji kabla hujula kitu chochote,tunajua kabisa kabla ujala au kunywa chochote sumu nyingi mwilini zinakuwa hazijachanganyikana na chochote kwa hiyo tunapaswa kujua kuwa kuna faida kubwa nyingi za kunywa maji kama ifuatavy Soma Zaidi...

Faida za kula Pilipili
Usiogope kuwashwa, kula pilipili ni nzuri kwa afya yako ia virutubisho vingi sana Soma Zaidi...

Vyakula vya madini kwa wingi, na kazi za madini mwilini
Utajifunza vyakula vyenye madini kwa wingi, kazi za madini mwilini na athari za upungufu wake Soma Zaidi...

Sababu za kuwa na fangasi ukeni
Posti hii inahusu zaidi sababu za kuwa na fangasi ukeni, ni vitu ambavyo usababisha fangasi ukeni kama ifuayavyo. Soma Zaidi...