MAUMIVU YA VIUNGO NA VIUNGO KUWAKA MOTO.

Viungio ni sehemu za mwili ambapo mifupa hukutana. Viungio ndio ambavyo huruhusu mifupa kujongea. Miongoni mwa viungio ni kama mabega, hips, viwiko, magotini, shingoni, voganjani na maeneo mengineyo. Maumivu ya viungio ni hali ya kutokuwa sawa ama kuuma ama kupata jaoto kwa viungio. Tatizo la kuuma kwa viungio ni la kawaida sana na mara nyingi halihitaji dawa. Mtu anaweza kuhisi kama viungo vinawaka moto hali hii pia ni katika hali zinazotambulika kama maumivu ya viungo.Ila hutokea maumivu ya viungo yakawa ni mtokeo ya maradhi ama majeraha na ajali. Maumivu ya viungo mara nyingi sababu kuu ni ugonjwa unaoitwa arthrist. Hata hivyo zio zaidi ya sababu 20 za maumivu ya viungo.Je na wewe unasumbuliwa na maumivi ya viungio?. makala hii ni kwa ajili yako. Hapa tutakwenda kunagalia sababu za maumivu ya viungo. Makala hii ni moja kati ya juhudi zetu za kuelemisha jamii juu ya yale ambayo yanatokea mara kwa mara kwa watu.


Nini husababisha maumivu ya viungo na viungo kuwaka moto?


1.Kuwa na infection (mashambulizi ya bakteria na virusi) kwa mfano virusi vya influenza, hepatitis


2.Kuwa na uvimbe kwenye viungio kitaalamu hutambulika kama inflamation


3.Mfumo wa kinga mwilini (autoimmune diseases) kushambulia maeneo ya viungo na kupelekea inflamation ama kuuwa seli. Hakuna sababu maalumu inayojulikana kusababisha jambo hili


4.Kukusanyika kwa asidi ya uric kwenye viungo (uric acid) mara nyingi hii huathiri miguu na utahisi kama miguu inawaka moto. Kutokunywa maji kwa wingi kunaweza kuwa m,oja ya sababu ya hambo hili. Kama una maradhi ya figo, ama shida kwenye tezi ya thyroid ama una maradhi ya kurithi inaweza kuleta shida hii kwa kiasi kikubwa. Watu wengine walio hatarini ni wenye kunywa pombe, wenye shinikizo la juula damu (presha ya kupanda, marahi ya ini kisukari na shida kwenye tezi ya thyroidSababu nyingine za maumivu ya viungo
5.Kulainika na kuvunjika kwa mfupa laini (cartilage) w kwenye magoti.
6.Kuwa na majeraha
7.Kufanya kazi ngumu kwa muda mrefu
8.Kuwa na saratani
9.Kumung’unyika na kuvunjika kwa mifupa kutokana na ugonjwa unaojulikana kama osteoporosis
10.Udhaifu wa mifupa na mategeNJIA ZA KUZUIA MAUMIVU YA VIUNGO NA VIUNGO KUWAKA MOTO
1.Tumia dawa za kukata maumivu
2.Fanya mazoezi ya mara kwa mara
3.Kabla ya kufanya mazoezi jikunyuekunjue kwanza (stretch) ili kuvipa moto viungo
4.Kunywa maji mengi na ya kutosha
5.Punguza uzito wa mwili wako kama upo juu sana.
6.Hakikisha unakula mlo kamili
7.Kama mtoto anasumbuliwa na hali hii hakikisha anakunywa maji mengi, pia vitamini D vya kutosha.