Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu elimu ya kuhusu HIV na UKIMWI
ELIMU YA KUHUSU HIV NA UKIMWI
Ni nini maana ya Ukimwi?
UKIMWI ni ufupisho wa maneno “upungufu wa kinga mwilini” ni hali sugu, inayoweza kutishia maisha inayosababishwa na virusi vya Ukimwi (VVU). Kwa kuharibu mfumo wako wa kinga, VVU huingilia uwezo wa mwili wako kupambana na viumbe vinavyosababisha magonjwa. Viumbe hivyo ni kama bakteria, virusi, protozoa, fangasi na vinginevyo.
Nini maana ya Virusi Vya Ukimwi (VVU)?
VVU ni ufupisho wa maneno Virusi Vya Ukimwi, ni virusi vinavyosababisha upungufu wa kinga mwilini. Hudhoofisha mwili uwezo wake kujilinda dhidi ya vijidudu vya maradhi. Neon hili kwa lugha ya kiingereza hufupishwa kama HIV.
VVU ni maambukizo ya zinaa. Yanayoweza pia kuenezwa kwa kuongezewa damu iliyoambukizwa au kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua au kunyonyesha. Inaweza kuchukua miaka mimngi huwenda 5 mpaka 10 kabla ya VVU kudhoofisha kinga yako ya mwili hadi kufikia ukimwi.
Je ipo tiba ya VVU na UKIMWI?
Hakuna tiba ya VVU / UKIMWI, lakini kuna dawa ambazo zinaweza kupunguza kasi ya ukuaji wa magonjwa na uharibifu wa kinga ya mwili. Dawa hizi zimepunguza vifo vya UKIMWI katika mataifa mengi yaliyoendelea. Lakini VVU inaendelea kupunguza idadi ya watu barani Afrika, Haiti na sehemu za Asia. Dawa hizi mimkusanyiko wa dawa nyingi kwa pamoja hufahamika kama ARV yaani Ant-Retrovirus na matibabu yake hufahamika kama ART yaani Ant-Retroval Therapy. Dawa hizi piazimegawanyika katika makundi mengi kama NRTIs, NNRTs, Protease inhibitors na nyinginezo kibao.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowMrija wa mkojo hutoa mkojo nje ya mwili lakini mrija huu unapoziba hufanya utoaji wa mkojo kutoka kwa shida au maumivu
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na uvimbe wenye uchungu wa mishipa midogo ya damu kwenye ngozi yako ambayo hutokea kutokana na ongezeko la joto la ghafla kutokana na halijoto ya baridi. Pia inajulikana kama pernio, chilblain inaweza kusababisha kuwasha,
Soma Zaidi...Huu ni ugonjwa wa fangasi wanaosababishwa na mashambulizi ya fangani aia ya yeast waitwao candida.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi madhara ya kutotibu ugonjwa wa uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo,ni madhara yanayotokea kwenye mfumo mzima wa kupitisha mkojo na via vya uzazi kama ifuayavyo.
Soma Zaidi...Maumivu ya tumbo yanaweza kusababishwa na mambo mengi ikiwemo typhod, vidonda vya tumbo na shida nyingine kwenye mfumo wa chakula.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu sababu za mwanamke kuumwa tumbo chini ya kitovu, ni tatizo ambalo limewapata wanawake wengi na pengine sababu ni vigumu kupata au pengine zinapatikana lakini kwa kuchelewa hali ambayo usababisha madhara mbalimbali kwenye mwili.
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea namna na jinsi ya kujikinga au kuzuia Ugonjwa wa ini.
Soma Zaidi...Hapa nitakueleza namna ambavyounaweza kupunguza hatari ya kupata maradhi ya ini. Kwa njia hizi unaweza kujikina wewe na wengineo na maradhi haya hatari ya ini.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya viungo vinavyoathiriwa na ugonjwa wa malaria
Soma Zaidi...