NJIA ZA KUZUIA KIUNGULIA
Kiungulia hutokea pale tindikali zilizopo tumboni zinapanda juu na kufikia koo sehemu ambayo inaunganisha tumbo na koo la chakula. Kiungulia sio shida sana kiafya kwani huwa kiaondoka chenyewe. Hata hivyo kuna watu wapo hatari kupata kiungulia cha mara kwa mara.Je na wewe ni mmoja katika wanaopata kiungulia mara kwa mara. Je kiungulia ni kikali kiasi cha kuharibu ratiba na uhuru wako? Makala hii ni kwa ajili yako. Hapa nitakuletea njia ambazo zitakusaidia kuzuia kiungulia cha mara kwa mara.Njia za kuzuia kiungulia
1.Usile chakula kingi kupitiliza
2.Punguza uzito ulio nao
3.Punguza unywaji wa pombe
4.Usinywe sana chai ya majani ya chai yenye caffein kwa wingi
5.Tafuna bigjii zisizo na sukari nyingi
6.Wacha kutumia kitunguu kisichopikwa kama kwenye kachumbari
7.Epuka vinywaji vyenye carbonate. Soma lebo ya kinywaji chako kama ni soda ama maji kama kuna carbonate
8.Usinywe kwa wingi juisi zilizotokana na vitu vya uchachu kama limao
9.Punguza kula chokoleti kwa wingi
10.Unapolala inuka kichwa chako kwa mfano tumia mto
11.Usilale ndani ya masaa matatu baada ya kula
12.Ukilala lalia upande wa kushoto usilalie upande wa kulia.Dawa za kutibu kiungulia
Unaweza kutibu kiungulia kwa kutumia antacid kama vile Tums, Rolaids na Maalox. Dawa ambazo zimetengenezwa kwa madini ya calcium carbonate au magnesium ni nzuri pia. Magnesium si nzuri kama ujauzito upo mwishoni.Madaktari wengi wanakataza kwa wajawazito matumizi ya antacid ambazo zimechanganywa na sodium, ama zila lebo ya aluminium carbonate kwani zinawza kupelekea kukosa choo. Pia dawa hizi za kiungulia zinakatazwa kwa wajawazito Alka-Seltzer.