Makala hii itakufundisha maradho makuu ya macho, matibabu yake na tiba zake
MARADHI YA MACHO
Matatizo ya macho yapo mengi katika jamii, lakini mara nyingi matatizo ya macho yanatibika iwapo mgonjwa ataonana na daktari mara atakapoona dalili. Miongoni mwa matatizo ya macho ni kupoteza uwezo wa kuona.
1.Kutoona karibu (long sightedness)
Tatizo hili mara nyingi huwatokea watu wenye umri wa miaka 40 na kuendelea.
Dalili
A.Katika mazingira ya kawaida anaona sawa sawa
B.Kushindwa kusoma herufi ndogo ndogo
C.Kushindwa kufanya kazi za sehemu ndogo ndogo mfano kutunga sindano.
Matibabu: Kutumia miwani ya kusomea.
2.Kutoona Mbali (short sightedness)
A.Hayana umri maalum
B.Myopia – haoni mbali vizuri
C.Hyperopia – haoni mbali na kichwa kinauma akikosa kuvaa miwani yenye namba ndogo kusaidia lense.
NB: Mgonjwa anasoma karibu bila miwani
Matibabu: Kutumia miwani ya kuonea mbali
3.Mtoto wa Jicho (cataract)
Dalili
A.Kidoto cheupe katikati ya kioo cheusi cha jicho (kinafunika mboni ya jicho)
B.Kidoto cheupe kisichobadilika kwa mwangaza
C.Kupunguza nuru ya macho
NB - Mtu anaweza kuzaliwa nacho au kupata ukubwani, inaweza kuwa kwenye jicho moja au yote. Mgonjwa huona mchanganyiko wa rangi anapoangalia mwangaza kama taa za umeme au gari.
Matibabu
Mtoto wa Jicho huwa anatibika kwa upasuaji mdogo na kumuwezesha mgonjwa kuona tena.
4.Presha ya macho (glaucoma)
Tatizo hili husababishwa na kuongezeka presha ya jicho (intraocular pressure) kutokana na kukosekana uwiano wa mzunguko wa majimaji ndani ya jicho (aqueous fluid) kinachotoka kidogo kuliko kinachoingia.
Matokeo
Glaucoma hukandamiza na kuuharibu mshipa wa fahamu ya jicho na kusababisha kupungua kwa nuru na baadae kupoteza nuru ya macho.
Matibabu: Kuonana na daktari kwa ushauri na dawa
5.Macho tongo
Hutokea ama kwa mtu mmoja mmoja, makundi au kwa msimu.
Sababu:
Vimelea ambavyo huzaliwa kwenye sehemu za uchafu Wakati wa msimu huambukiza kwa kukosa elimu ya afya, kwa mfano kutokuosha mikono baada ya kuamkiana na mgonjwa mwenye maradhi haya au kutumia vifaa vya macho kwa zaidi ya mtu mmoja kama vile miwani.
Dalili
A.Kuhisi kama kuna mchanga ndani ya jicho
B.Kuvimba mifuniko ya macho bila kupoteza nuru.
C.Macho kuwa mekundu sana (conjuctivitis)
D.Kutoka tongo kila mara
Matibabu
Mgonjwa atumie dawa alizoandikiwa na daktari tu, kwani dawa za matone za macho ni nyingi na zina kazi tofauti.
6.Matatizo ya sehemu nyeusi ya jicho (cornea)
Kuna matatizo manne makubwa
1. Kovu - kidoto/kibaka cheupe
2. Kidonda - kidoto kijivujivu
3. Kuingiwa na kitu - kemikali,mdudu, vumbi n.k
4. Kutoboka na kutoa maji.
Indhari: hali ya pili mpaka ya nne zikitokea mgonjwa akimbizwe
hospital wakati jicho limefunikwa baada ya huduma ya kwanza
Dalili
KOVU
1.Haina maumivu
2.Jicho haliwi jekundu
3.Jicho halivimbi
4.kupungua nuru jicho
KIDONDA
A.Kinayo maumivu
B.Jicho lililoathirika huwa
C.jekundu
D.Jicho kupunguka nuru
E.Kuuma jicho kwenye
F.mwangaza
G.Kutoka machozi
H.Jicho kuvimba
Kidonda kinaweza kusababishwa na bakteria, fangas, ukosefu wa vitamin A au kwa kuumia mfano; kujichoma na kitu chenye ncha au kitu kigumu, kuingiwa na kitu jichoni, kuungua au kuingia kemikali jichon.
Indhari: Iwapo jicho litaumia lifunike jicho lisipate mwangaza kisha mpeleke mgonjwa hospitali.
7. Kemikali na kuungua
Kama mgonjwa ameingia kemikali kama vile acid, alkali, saruji, chokaa mtie maji ya mchuruziko kwa takriban dakika 15 mfululizo na baadae mpeleke hospitali
8.Macho kuwasha na kutokwa na machozi (conjuctivitis)
Huwakumba zaidi watoto wa umri kati ya miaka 5 -15 ambao hupendelea kucheza sehemu za vumbi au kwenye muangaza mkali (pwani yenye mchanga mweupe sana)
Watu wazima wenye kufanya kazi kwenye viwanda vinavozalisha vumbi, na wenye pumu ya muda mrefu.
Dalili
A.Macho kuwasha (Nuru ya macho haipungui)
B.Macho kubadilika rangi (kahawia)
C.Kutokwa na machozi mengi (sana)
D.Kushindwa kuangalia kwenye muangaza mkali
Matibabu
Kusafisha macho mara kwa mara kwa maji safi.
Kutumia dawa kwa maelekezo ya daktari
9.Kinundu katika mfuniko wa juu au chini wa jicho
DALILI
A.Kinundu kisichouma
B.Mara nyingi hupona wenyewe au unaweza kukikanda kwa maji ya uvuguvugu.
C.Kisipopona au kitakapokuwa kikubwa huhitaji upasuaji mdogo.
10.Uvimbe katika mfuniko wa jicho (cellulitis)
A.uvimbe kwenye mifuniko ya jicho
B.inaweza kuzuwia jicho kucheza (kutembea tembea)
C.mara nyingi hutokea baada ya kusambaa kwa maambukizo
D.ya socket ya jicho kutoka pembezoni kwa saines (sinusitis) za pua
E.husababisha kupoteza nuru za macho
Matibabu: Mpeleke mgonjwa kwa daktari wa masikio, pua na koo (ENT).
Umeionaje Makala hii.. ?
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya viungo vinavyoathiriwa na ugonjwa wa malaria
Soma Zaidi...Posti hii inahusu dalili za ukosefu wa misuli. ukosefu wa udhibiti wa misuli wakati wa harakati za hiari, kama vile kutembea au kuokota vitu. Ishara ya hali ya msingi, Ataxia inaweza kuathiri harakati, hotuba, harakati za jicho na kumeza.
Soma Zaidi...Malaria ni katika maradhi ambayo husambazwa na na mbu jike aina ya anopheles.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi magonjwa ya kurithi ambayo hubebwa na vinasaba vya urithi kutoka kizazi kimoja kwenda kingine.magonjwa haya hata hivyo ,si kila kasoro huwa ni ugonjwa kwa mtu mfano ,ualbino na kitoweza kutofautisha rangi kama vile nyekundu na kija
Soma Zaidi...Kila mtu anaweza kupata ugonjwa wa pumu, hata hivyo kuna ambao wapo hatarini zaidi kupata pumu.
Soma Zaidi...Unyogovu (Depression ) ni mojawapo ya ugonjwa wa akili ambao unahusishwa na hisia za huzuni, kukosa matumaini, na kupoteza furaha au shauku katika shughuli za kila siku. Huu si tu hisia ya huzuni iliyokatisha tamaa, bali ni hali sugu inayoweza kuathiri mabadiliko ya mwili, mawazo, na tabia ya mtu. Unyogovu unaweza kutokea kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya kemikali katika ubongo, maumbile, mazingira, na matukio mbali mbali katika maisha ambayo kupelekea mgonjwa kuwa hivyo.
Soma Zaidi...Saratani ya Figo ni Saratani ambayo huanzia kwenye figo. Figo zako ni viungo viwili vyenye umbo la maharagwe, kila kimoja kikiwa na ukubwa wa ngumi yako. Ziko nyuma ya viungo vyako vya tumbo, na figo moja kila upande wa mgongo wako.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kujikinga na magonjwa, kwa kawaida tunajua wazi kuwa magonjwa yapo na yanasambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na mengine hayasambai yanaweza kumpata mtu mmoja akapona au magonjwa mengine si ya kupona
Soma Zaidi...Posti hii inshusiana na dalili za anemia ya minyoo
Soma Zaidi...