Posti hii inahusu zaidi dalili za mtoto Mwenye UTI,ni dalili ambazo uwapata watoto wadogo chini ya umri wa miaka mitano.
Dalili za UTI kwa mtoto chini ya umri wa miaka mitano.
1. Mtoto anakuwa na njano
Mtoto mdogo mwenye chini ya umri wa miaka mitano akiwa na ugonjwa wa UTI akiwa na Maambukizi ya UTI anaweza kuwa na njano kama dalili mojawapo ya ugonjwa wa UTI.
2. Joto la mwili kushuka kuzidi kiasi
Mtoto mdogo akiwa na ugonjwa wa UTI joto lake la mwili kushuka kupitia kiasi, hii utokea hasa kwa watoto wenye Chini ya umri wa miezi miwili kwa hiyo mama akiona dalili hii anapaswa kumwangalia mtoto wake na kupima UTI.
3. Mtoto akiwa na UTI anaweza kuharisha na kutapika, hii utokea kwa sababu maambukizi yanakuwa yameenea sehemu mbalimbali za mwili na usababisha kutoa kila kitu ambacho uingia mdomoni na kumfanya mtoto aanze kutapika na kuharisha, lakini si kila mtoto anayeharisha na kutapika ni kwa sababu ya ugonjwa wa UTI lakini mama na mlezi wanapaswa kupima mtoto ikiwa ataonyesha dalili za kuharisha na kitapika.
4.Maumivu ya chini ya Tumbo.
Hii ni dalili ambazo ujitokeza kwa watoto kuanzia miezi miwili mpaka miaka mitano, kwa Sababu ya maambukizi kuenea sehemu mbalimbali tumbo uanza kuuma hasa chini ya kitovu kwa hiyo mtoto kama hawezi kuongea ukimgusa kwenye tumbo anasikia maumivu lakini wale wenye uwezo wa kuongea wanaweza kuponyesha dalili.
5.Maumivu wakati wa kukojoa
Hii ni dalili mojawapo kwa mtoto Mwenye dalili ya UTI, kwa Sababu ya maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo na bakteria wameshaharibu kibofu mtoto usikia maumivu makali wakati wa kukojoa na pengine uanza kulia Lia kwa sababu ya maumivu.hapa mtoto kama anaweza kuongea atakwambia kama hawezi utaona analia wakati wa kukojoa.
6. Kiasi Cha kikohoa kwa mtoto kuongezeka.
Hii utokea kwa sababu ya maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo, kwa hiyo kibofu Cha mkojo hushindwa kutunza mkojo kwa mda mrefu na halimaye mkojo uanza kutoka mara kwa mara. Kwa hiyo hii Dalili ukolijitokeza mama inabidi awe makini kwenda kwenye vipimo Ili kuangalia kama Kuna UTI au la.
Angalisho: hapo juu ni Dalili za UTI kwa watoto iwapo mtoto atapatwa na dalili hizo usinunue dawa kumpatia ukadhani mara Moja ni UTI Bali inabidi kuchukua vipimo maana hizo Dalili uweza kujitokeza hata kwa magonjwa mengine.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kupambana na saratani
Soma Zaidi...posti hii inazungumzia kuhusiana na Ugonjwa na Ugonjwa unaohusiana na joto ambao hujulikana Kama Anhidrosis ni kutoweza jasho kawaida. Usipotoa jasho mwili wako hauwezi kujipoza, jambo ambalo linaweza kusababisha joto kupita. wakati mwingine inaweza k
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia mtoto akiwa na ugonjwa wa UTI.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu kiungulia kwa wanawake wajawazito na tiba yake, ni ugonjwa au hali inayowapata wajawazito walio wengi kwa sababu ya kuwepo kwa mabadiliko ya homoni wakati wa ujauzito.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuwahudumia wenye Maambukizi kwenye mifupa, ni njia ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kuwasaidia wenye Maambukizi kwenye mifupa.
Soma Zaidi...Mrija wa mkojo hutoa mkojo nje ya mwili lakini mrija huu unapoziba hufanya utoaji wa mkojo kutoka kwa shida au maumivu
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa upele, ni dalili au mwonekano wa mgonjwa wa upele.
Soma Zaidi...Kama una tatizo la midomo kuchubuka na kuwa myeupe ama kuwa na vidonda. Post hii inakwenda kuangalia swala hili.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za maumivu ya jino
Soma Zaidi...