Makala hii inakwenda kukuletea masharti yanayompasa mwenye vidonda vya tumbo ayafate. Je ni vyakula gani vinafaha sana kwa mwenye vidonda vya tumbo?
Masharti ya vidonda vya tumbo
1.Punguza ama wacha kabisa unywaji wa pombe
2.Punguza misongo ya mawazo
3.Epuka vyakula vyenye gesi kama baadhi ya aina za maharagwe
4.Hakikisha unakula kwa wakati.
5.Epuka kukaa na njaa kwa muda mrefu
6.Epuka matumizi ya madawa ya aspirin na jamii za madawa hayo. Kama ni lazima utumie madawa mbalimbali na ya mchanganyiko hasa yale ya kuzuia maumivu, basi kwanza zungumza na daktari akupe maelekezo.
7.Punguza ama wacha kabisa uvutaji wa sigara
8.Hata kama hutakuwa na hamu ya kula jilazimishe ule ama tumia dawa za kuongeza hamu ya kula.
9.Epuka vyakula vyenye mafuta kwa wingi.
10.Kunywa maji mengi ya ya kutosha kila siku
11.Onana na daktari mara kwa mara unapohisi mabadiliko ya hatari mwilini mwako.