Simulizi ni nzuri sana maana zinafundisha na hazibagui mkubwa wala mdogo... tusikilize na kusoma kisa cha tabibu wa mfalme....kutoka katika kitabu cha kwanza cha HALIF LELA U LELA...
TABIBU WA MFALME
Katika nchi ya Zouman iliyopo maeneo ya uajemi alikuwepo mfalme mkubwa sana. Mfalme huya alipenda kusoma na kucheza mpira wa farasi, alimwamini sana waziri wake. Mfalme huyu alikuwa na ugonjwa ambao matatibu wengi walijitahidi lakini walishindwa. Kila tabibu mzuri katika nchi yake alijaribu bila ya mafanikio. Mfalme alikata tamaa ya kupon augonjwa wake.
Ilitokea katika nchi ile kuna tabibu ambaye ni mjuzi sana lakini hakutambuwa kama mfalme ana tatizo hilo. Tabibu huyu aliitwa Douban. Alipo[ata taarifa za ugnjwa wa mfalme alikusanya mavitabu yote na utabibu na kuanza kustadili kuhusu ugonjwa wa mfalme wake. Na hatimaye akafanikiwa kugunduwa dawa itakayomtibu mafalme. Dawa ambayo ingemtibu mfalme hata bila ya kumgusa. Siku ilofata alivaa nguo zake safi za kitabibu na akaenda ikulu kuomba kumuona mfalme. Kwa kuwa alijitambulisha kama tabibuilikuwa ni rahisi kwake kumuona mfalme. Alipiga magoti na kumueleza mfalme kilicho mleta. “nina dawa ya kutibu maradhi yako hata bila ya kukugusa kwa uwezo wa Allah” ni tabibu akimwambia mfalme. “ukitibu maradhi nilonayo nitakufanya tajiri na utakuwa ni katika watu wangu wa karibu” kwa furaha mfalme akimwambia tabibu Douban. “Ndio mkuu tutaanza tiba yetu kesho IN shaa Allah” ni maneno aliyoyasema tabibu.
Siku hiyo tabibu alivaa safi mavari yake na kuiweka dawa yake tayari kwa ajili ya kumtibu mfalme. Aliiweka dawa yake kwenye fimbo ya kuchezea mpira wa farasi. Kisha akamwambia mfalme atumie fimbo ile kuchezea mpira wa farasi na apige kwa nguvu mpaka jasho limtoke. Mambo yaka wa kama hivyo na mechi ikaanza. Mfalme alicheza kwa uwezo wake wote na akawa anapiga mpira kwa fimbo yenyedawa. Kila anapopiga ndio dawa inavyiongia kutoka kwenye fimbo kuingia mwilini mwake. Mechi ilipoisha akamwambia mfalme akifika nyumbani kwake aoge kisha alale. Mfalme alifanya vivyohivyo na alipoamka ailikuwa ni asubuhi. Alistaajabu kuona ampona kabisa maradhi yake.
Aliagiza tabibu Douban aletwe mbele yake ili amlippe alichomwahidi. Mambo yakawa vivyo hivyo aliletwa tabibu na kutoa heshima kwa mfalme. Mfalme alifurahi na kumpa utajiri yeye na familia yake. Tabibu Douban akawa ni katika watu wa karibu na mfalme. Baadhi ya viongozi wa nchi walimonelea wivi tabibu. Waziri mkuu alikuwa ni muhanga wa jambo hili. Alikuwa akikasirika sana kumuona tabibu na mfalme. Hakupenda ukaribu wao na alitafura mbinu na njama mbalimbali kuweza kuwatenganisha.
Sikumoja kaamuwa kutekeleza mpango wake, alimfata mfalme na akamweleza kuwa amegunduwa kuwa huyu tabibu anataka kukuuwa. “kama angetaka kuniuwa kwa nini amenitibu” ni swali la mfalme kwa waziri. “huenda ange kuuwa muda ule angejulikana, lakin sasa umemwamini muda si mrefu atatekeleza madhambi yake” waziri akimjibu mfalme. Mabishano haya yalichukuwa muda mfalme akimtetea tabibu na waziri akimkandamiza tabibu. Mwisho mfalme akamwambia tabibu “nakumbuka vizuri maneno ya waziri mfani alipomwambia mfalme Sinbad alipotaka kumkinga mwanae asiuliwe” . “ni maneno ganihayo ewe mfalme wangu” waziri akimuuliza mfalme kwa shauku. Mfalme akamjibu “alimwambia usiamini maneno ya mtu yeyote hata akiwa mkweo kisha akamsimulia hadithi hii”;-
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Mankaa Tarehe 2024-09-09 13:07:45 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 65
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani
👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉3 kitabu cha Simulizi
👉4 Simulizi za Hadithi Audio
👉5 Kitabu cha Afya
👉6 Kitau cha Fiqh
Simulizi za Hadithi EP 2 Part 4: Hadithi ya mzee wa tatu na mbwa wake mwekundu.
Hadithi za HALIF LELA U LELA hii ni moja wapo imetoka katika kitabu cha kwanza imaelezea kisa cha mzee wa tatu.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 7 Part 9: Familia mpya
Muendelezo..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 19: Mfalme na waziri wake
Hadithi hii inapatikana katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 3 Part 1: Kisa cha mvuvi na jini
Simulizii hii inapatikana katika kitabu cha kwanza cha HALIF LELA U LELA .... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 7 Part 6: Hadithi ya ugeni wa dhati
Muendelezo..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 10: Ndoa ya binti mfalme na Sinbad
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza muendelezo...... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 8 Part 2: Siri ya kifo
Simulizi hii pia inapatikana kwenye kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 8 Part 1: Hadithi ya tunda
Simulizi hii pia inapatikana kwenye kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part24 : Kaka wa tatu wa kinyozi
Muendelezo Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 16: Hadithi ya safari ya saba ya Sinbad
Muendelezo wa safari ya Sinbad....... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 19: Kinyozi
Hii ni simulizi iliyopo ndani ya kitabi cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 14: Wageni
Simulizii hii ni nzuri na ni mojawapo ya hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili...... Soma Zaidi...