image

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 12: Dirisha moja kwanini????

Muendelezo....

 

KWA NINI DIRISHA MOJA?

 

 

 

Siku hiyo Aladini aliamka mapema, na kuelekea sehemu ya kuogea. Aliridhishwa vyema na usafi wa chooni na alivyovikuta. Alifanya usafi wa mwili wake, huku akimuacha binti Sultani akiwa bado amelala kwa uchovu wa pirikapirika za jana nzima. Baadaye binti mfalme aliamka na kufanya usafi kisha wote wakaelekea kupata kifungua kinywa. Wote walikuwa wamevaa pete sawa kwa rangi. Pete zilizokuwa za dhahabu huki vichwa vya pete vilikuwa ni almasi yenye kichwa cha yule ndege wao. Mama Aladini alipowaona watoto wake machozi ya furaha yalimtoka, hata akatamani mzee Mustapha angelikuwa hai siku kama ya leo.

 

 

Kama mfalme alivyoahidi, alifunga safara wake na matarumbeta yake kwenda nyumbani kwa Aladini. Walijipanga wananchi kwa kumuheshimu mfalme wao kila alipopita. Haukuchukuwa muda mrefu saana, hatimaye msafara ukawa nje ya jumba kubwala Aladini. Halikuwa ni umba la gorofa matarumbeta yote yalinyamaza punde sauti za kasuku zilipoanza kusiika. Sauti zilizidi uzuri wa matarumbeta. Mfalme alifurahi na kutabasamu. Sharubu za mfalme zilipepea vyema kwenye upepo mwanana mbele ya miti ya mauwa na matunda nyumbani kwa Aladini.

 

 

Macho ya mfalme yakaelekea kwenye ukuta wa jumba hili, na baada ya kujidhisha kwa uzuri ulioje ghafla mfalme akakaza macho a sura. Pale alipoona dirisha moja. Mfalme alimlaumu Aladini kwenye nafsi yake. Mfalme alimlaumu na kuwaza laiti kama angeliishiwa na pesa ya wajenzi ama vifaa angelinambia tu ningemtekelezea. Wakati haya yanaendelea kutokea Aladini, mkewe na Mama yake wakaja kuwapokea. Ilikuwa ni furaha juu ya furaha. Msafara ukaingia ndani na mjakazi mukuu akaendelea kupanga kila mtu kumpa majukumu yake. Kisha mfalme akaa kupata chakula. Na mazungumzo ya hapa na pale yakaanza.

 

 

Mfalme alionyesha kuridhika sana na ubora wa nyumba na wajenzi. Wakiwa wanazungumza hapa na pale binti mfalme alikuwa anahisi kitu kwa baba yake kana kwamba ana jambo anataka kulisema. Binti akaanza kumdadisi baba. Hatimaye mfalme akafunguka. “baba umejenga jumba zuri sana ila sikuridhishwa na dirishao majo., baba uliishiwa na wajenzi ama vifaa”? “baba nimewacha kusudi ili na wew utie baraka zako, umalizie dirisha lile iwe sifa kuwa hata mfalme amechangia katiaka ujenzi” ni majibu ya Aladini. Mfalme alifurai sana na kuona kumbe mkwe wake anampenda sana. Basi mfalme akaahidi kuanza kazi kesho kuleta wajenzi.

 

 

Mazungumzo yaliendelea na baadaye mama Aladini akajiunga na mazungumzo kisha Mama Aladini akaondoka na binti mfalme. Hapo mfalme akapata fursa ya kuwa pekee na mkwewe. Wakatoka nje na kuendelea kupata upepo na kuzungumza kwa undani. Walizungumza sana hata mfalme akazungumza ya moyoni kabisa kuwa anatarajia kupata mjukuu apema. Na oia Aladini ajiandae kuwa mfalme ajae pindi atakapo fariki. Basi ilkuwa ji furaha juu ya furaha. Ilipofika jioni Mfalme akarudi kwake ikulu. Waliangana kwa ucheshi sana hasa mama Aladini na Mfalme walikuwa kama dada na kaka sasa.

 

 

Baada ya mfalme kuondoka mama Aladini naye akaaga kuondoka kurudi kwake. Aladini ijapokuwa liamsihi sana mama yake waishi wote lakini mama alikataa. Watu wote walipondoka aladini alibaki yeye na mkewe na wafanyakazi. Aladini aliuweka mshumaa wake juu ya meza na kumwambia mkewe asijeutoa mshumaa ule. Lakini hakumwambia siri hasa ya mshumaa ule. Pia Aladini alikuwa navaa pete mbili moja ile ilofanana na mkewe na nyingine ni ile pete ya ajabu. Pia hakumwambia mkewe siri ya pete ile. Hata hivyo mkewe hakuonyehsa kutaka kujuwa chochote katika vitu hivi.

 

 

Siku ilofata mfalme alileta mafundi kujenga bila mafanikio. Hawakuwa na ujuzi hata hivyo hawakuwa na vifaa pia. Nchi nzima ilitafutwa madini yaliyoweza kurekebisha dirisha bila kupatikana. Hatimaye mfalme akakiri kushndwa kazi. Basi kwa Aladini haikuwa ni kazi kubwa. Ilikuwa ni kazi ya usiku mmoja chini ya nguvu ya jini wa mshumaa. Asubuhi dirisha lkawa safi. Basi maisha yaliendelea kwenda hatimaye miezi kadhaa ikapiata. Aladinia kawa anakwenda kuwinda na mkwewe kujifurahisha.

 

 

Maendeleo ya Aladini yaliweza kushangaza uma na hayakuweza kuridiwa na watu wote. Mmoja wapo alikuwa ni waziri mkuu. Ambaye mpaka sasa alipo hakujulikani. Ukweli ni kuwa baada ya tukio la ndoa ya Aladini waziri aliondoka kwenda kutafuta siri ya aladini. Waziri alifika mbali sana mpaka nchi za Afrika huko alikutana na mchawi mkubwa sana. Mchawi huyo ndiye aliyetoa siri nzima ya Aladini na maisha yake. Waziri mkuu alimpatia mchawi hongo kubwa sana ili ahakikishe kuwa Aladini anapotea, na anapata aibu kubwa na udhalili.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Mankaa Tarehe 2024-09-10 14:46:52 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 92


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Simulizi za Hadithi EP 10 Part 6: Ndoa ya pili
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 17: Siri ya wageni yafichuka
Muendelezo........ Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 2: Aladini kwenye pango la utajiri
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Nurdini na Barua ya mfalme wa baghadad
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 6: Hadithi ya Ndoa ya siri
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 9: Hadithi ya binti wa ndotoni.
Simulizi hii pia inapatikana kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 8: Harusi ya aladini kufanyika na binti wa mfalme
Muendelezo...... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 11: Kisa cha Kalid na Jalid
Tuendelee kusikiliza na kusoma visa, hadithi, na simulizi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza tuwe pamoja mpka mwisho...... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 16: Viatu vya ajabu vyaondoka na mkono wangu
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 25: Kaka wa nne wa kinyozi
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 3: Simulizi ya kuingia kwa wageni
Simulizii hii ya kuwasili kwa wageni inapatikana ndani kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... moja kwa moja tusikilize kisa hichi.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 10: Mapenzi kwenye mtihani
Simulizii hii inapatikana katika kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...