Menu



Simulizi za Hadithi EP 3 Part 3: Kisa cha mke na kasuku

Simulizi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza simulizii hii inasimulia kisa cha mke na Kahuku wake....

HADITHI YA MKE NA KASUKU.

 

Hapo zamani kulikuwa na mfanya biashara, ambaye alikuwa na familia yake na mkewe ambaye alimpenda san. Hakuamini kama atakuja kuachana naye. Kwakuwa yeye ni mfanya biashara alikuwa akisafiri mara kwa mara. Ijapokuwa kuanwatu walikuwa wakimpa maneno kuhusu mkewe alikuwa ahawaamini. Ilifikia wakati sasa aliingiwa na mawazo ya kutaka kuwaamini japo hakufanya hivyo,

 

Sikumoja alipopata safasi alikwenda kwenye maduka yanayouzwa ndege wa kufuga. Alinunuwa kasuku mmoja laiye mzuri sana. Kasuku huyu pia alikuwa na uwezo wa kuzungumza habari zilizofanyika wakati bwana wake hayupo. Alimnun ua kasuku yule kwa gharama za juu na akamuweka kwenya kitundu chake. Alimpelekea mkewe na kumwambia “mtunze ndege wangu huyu, na umuweke ndandi na katu usimtowe”. Mke alitii ankumchukuwa kasuku yule na kumugifadhi ndani.

 

Mfanya biashara huye alitoka na kuenda mbali ya mji. Huku nyuma mkewe akafanya ya kuyafanya pale ndani. Ulipofika wakati mfanya biashara alirejea nyumbani. Alimchukuwa kasuku wake na kutoka naye nyumbani ili kutafute mahala pa faragha kisha akamuuliza kasuku kilichofanyaka pale ndani wakati hayupo. Kasuku aliyasema yote aliyoyaona na hayakumpendeza yule mfanya biashara. Aliporejea nyumbani aligombana saa na mkewe. Mke alishangaa ni nani alomwambia. Aliwapa adhabu watumishi wake akidhani ndio walovunja siri. Ila baada ya muda akagunduwa kuwa ni kasuku ndiye muongo.

 

Mfanyabiashara laipata safari nyingine ya kibiashara. Alipoondoka yule mkewe alipotaka mufanya anayoyafanyaga aliwaita wajakazi wake watatu. Mmoja akamwambia aweke beseni la maji chini ya tundu la kasuku, na mwengine akamwabia maji juu ya tundu la kasuku na mwinguni akamwambia achukuwe kioo na kwa kutumia mwanga wa mshumaa ammulike kasuku kwa mwanga uloakisiwa na kioo. Akamwambia afanya hivi kulia na kushoto. Wakati mambo yote haya yakifanyika yule mke nae alikuwa akifanya mambo yake anayoyafanyaga wakati mumewe akiondoka.

 

Siku ilofata mfanyabiashara akarudi nyumbani. Akamuuliza kasuku kilichotokea kasuku akamwambia “mmh bwana wangu mvua ilikuwa kubwa pamoja na radi nilishindwa kujuwa kinachotokea.” yule mfanyabiashara alijuwa kuwa hakuna mvua ilonyesha usiku ule. Akaona kuwa kasuku ni muongo hivyo akaamua amchinye. Baada ya siku akaja kugunduwa kuwa kasuku alikuwa mkweli ila alichezewa mchezo, alijilaumu sana lakini lawama zisingemrudisha kasuku.

 

Baada ya kumaliza kuzungumza hadithi hii (mvuvi akamwambia jini maneno aliyoyasema ) mfalme akamwambia waziri “sitakusikiliza kwa hili, nitamshughulikia tabibu na kama nisije nikajuta kama mfanya biashara alivyojuta baada ya kumuuwa kasuku asiye na hatia”. Waziri akajibu “mfalme tabibu anataka kukuuwa, siwezi kumuacha na kama itatokea nimefanya kosa nitakuwa tayari kuadhibiwa kama alivyoadhibia waziri wa mfalme flani” “alifanya nini huyo waziri” ni swali aliodakia mfalme. Waziri akasimulia hadithi ifuatayo;-

Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Mankaa image Tarehe 2024-09-09 13:09:57 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 130


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 4: Simulizi ya chongo wa kwanza mtoto wa Mfalme
Tusikilizie simulizii inahusu chongo wa kwanza wa mtoto wa mfalme iliyopo ndani ya kitabu cha kwanza cha Hadithi za HALIF LELA U LELA..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 16: Kitabu cha ajabu
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 2 Part 2: Hadithi ya mzee wa kwanza na mbuzi wake
Simulizi za HALIF LELA U LELA zipo nyingi sana na husikiliwa na kusomwa na wakubwa kwa wadogo pia hadithi hizi zimeenea duniani Kate zikisikilizwa na maelfu ya watu mbalimbali. Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 10 Part 3: Asubuhi yenye varangati
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Hadithi ya Nurdini Mtoto wa Waziri
Hii ni hadithi ya kitabu cha tatu cha hadithi za HALIF LELA U LELA... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 5: Mshenga wa Aladini kwa mara ya pili mbele ya mfalme
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 11: Ndani mwa junba la Aladini
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 12: Sehemu ya tano ya safari ya Sinbad
Muendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 28: Hadithi ya mshona nguo (fundi cherehani)
Muendelezo...... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 10 Part 2: Ni ndoto ama kweli???
Muendelezo..... Soma Zaidi...