Simulizi za HALIF LELA U LELA zipo nyingi na zinasisimua.. kisa hiki cha samaku wa rangi nne kipo katika kitabu cha kwanza
SAMAKI WA RANGI NNE.
Baba yangu alikuwa ni mfalme wa eneo hili kwa muda usiopungua miaka hamsini. Alifariki akiwa na umri wa miaka 66, na baada ya kufariki kwake mimi nilichukuwa madaraka hayo. Nchi hii i;likuwa nzuri sana ilozungukwa na visiwa vinne ambavyo ndio milima unayoiona. Nilikuwa na mke wangu ambaye ni binamu yangu. Nilimpenda sana mke wangu na niliamini kuwa naye ananipenda kama ninavyompenda. Tuliishi hivyo kwa muda wa miaka kadhaa bila ya kuona mabadiliko yoyote katika mapenzi yetu.
Ilitokea siku moja nilipokuwa nipo kati ya kulala ama kusinzia (mang’amung’amu ya usingizi), vijakazi wawili wa mkewangu wakawa wananipepea. Nikawasikia wanazungumza “namuonea huruma mfalme, anampenda sana mkewe lakini mkewe hampendi, anampenda mtumwa wake.” ni maneno ya mmoja wa wale wajakazi. Mwingine akadakia “yaani anatamani hata amuuwe, na vile anajuwa ucha wipo siku atamuuwa tu”. Wajakazi hawa wakati wanazungumza walidhani nimelala, kumbe nimeyasikia vizuri maneno yao.
Siku ilofuata nikaanza kufanya uchunguzi wa maneno yale. Niligunduwa kuwa ni ya ukweli kama walivyosema wale wajakazi. Hivyo nikamchukuwa yule mtumwa na kuanza kumwadhibu. Kwa bahati mbaya wakati wa kumwadhibu alipigwa vibaya na akapoteza fahamu. Yule mke wangu alikasirika sana na akamtibu lakini bia ya mafanikio. Alifanikiwa kumueka hai, yaani anafahamu lakini haweza kufanya chochote. Mwanamke yule kwa hasira alizonzo wakati ule aliondoka kwa muda na nisijuwe wapi alipokwenda.
Baada ya muda akarudi, na akachukuwa kifuu cha nazi na akaweka maji, kisha akazungumza naneno ya ajabu akamwaga juu. Visiwa vilivyouzunguka mji huu vikawa milima hiyo unayoiona na mji yakiwemo maduka na vinginevyo ukawa bwawa la maji hayo unayoyaona na watu wakageuzwa kuwa samaki hao wa rangi nne unaowaona yaani hizo rangi za samaki ni aina za watu walokuwepo eneo hili. Baada ya kufanya hayo na mimi akanimwagia maji nikawa kama hivi unavyoniona. Haikuishia hapo kila siku anakuja kunitandika mijeledi ya ngozi ya kifaru. Hunitandia kadri anavyotaka kisha huondoka. Hii ndiyo historia yangu na mji huu.
Kijana alimaliza kusimulia hadithi ya nchi yake, mfalme alipatwa na uchungu sana wakati akisikiliza maneno yale. Chozi lilikuwa likimtoka kwa huruma na majonzi. Kish akauliza mahala alipo huyo mwanamke. Kijana akamjibu kwa kumwambia kuwa yeye hajui alipo isipokuwa kila siku jioni baada ya kuniadhibu huenda upande ule (akaelekeza kwa kidole upande wa kusini). Mfalme alikwenda kule alikoelekezwa na kumkuta mtumwa ambaye ni mgonjwa. Akarudi kwa kijana na wakapanga mbinu yako, kisha wakakubaliana watekeleze kesho mpango wao.
Basi mambo yakawa kama walivyokubaliana, siku ilofata mfalme akachukuwa upanga wake na akaunoa safi. Akaenda kwenye lile jumba lenye yule mtumwa mgonjwa. Alipofika akamkata upanga na kummalizia uhai wake, kisha akamuingiza kwenye kisima cha maji. Baada ya hapo akajilaza pale kwenye kitanda kama vile yeye ndiye mgonjwa. Yule mwanamke kama kawaida yake alipokuja siku ile akamuadhibu yule kijana kisha akaelekea kule kwenye mgonjwa wake. Alipofika akamwuliza “u hali gani wangu? Vip tafadhali naomba zungumza nami japo neno moja tuu”. Mfalme alojilaza pale kama yeye ndo mgonjwa akamjibu “sina raha kwakweli” “mmmh utamu ulioje leo kusikia sauti yako. Hebu niambie kipi kinachokukosesharaha jama”. Ni maneno ya yule mwanamke. Mfalme alojifanya ndo mgonjwa akajibu “hiyo sauti ya mumeo inanipa taabu, hebu mrudishe katika hali yake ya kawaida na aondoke hapa”. Basi kusikia hivyo yule mwanamke akatoka na kwenda kuchukuwa maji akayasemea maneno flani kisha akamwagia yule kijana na hapohapo akarudi katika umbo lake. Kisha akamwambia uondoke na nisikuone tena eneo hili, sihivyo nitakuuwa.
Yule kijana alijifanya anaondoka na akajificha ili ashuhudie kinachoendelea. Basi huku yule mwanamke akaelekea kule moyo wake ulipozama, alipofika akamuliza mtumwa wake “nimesha fanya utakavyo, vipi unajisikia amani sasa ?” yule mfalme alojifanya mgonjwa akamwambia hapana, hizo sauti za watu ulowageuza samaki zinanipa shida usiku. Hebu warudishe katika hali yao ya kawaida pamoja na mali zao”. Yule mwanamke akatii an kutoka akazungumza maneno yake ya kichwawi na mji ukabadilika kama ulivyo zamani. Wale watu wa mfalme walokuja kuchunguza samaki walishangaa kujikuta wapo katikati ya mji.
Yule mwanamke mchawi akaenda kwa mtumwa wake. Akamuuliza haya sasa bilashaka umeridhika. Yule mfalme alojifanya mgonjwa akamwambia “sogea hapa karibu” mwanamke akasogea zaidi yule mfalme akachukua upanga na kumkata vipande viwili. Hna huo ukawa ndo mwisho wa mchawi huyu. Mfalme akatoka na kukutana na kijana. Waliflai sana na kuzungunza mengi zaidi kuhusu eneo lile lenye mali mengi na utajiri wa kutosha.
Yule mfalme akamwambia kijana “nimeflai sana, na kwakuwa tupo majirani zaidi tutakuwa ndugu”. Kijana alicheka sana kwa fyraha na mshangao. Kisha akamwambia yule mafalme “kutoka hapa mpaka kufika kwenye utawala wako ni mwendo wa mwaka mmoja. Uliweza kutumia masaa machache kwa sababu eneo hili lilifanyiwa uchawi kama ulivyoona. Basi kijana akamwahidi atamsindikiza wakati wa kurudi mpaka kwake. Mfalme aliflai sana na akamwahidi kumfanya mrithi wa utawala wake kwani yeye hakuwa na mtoto wa kumrithisha.
Basi mambo yakawa hivyo, na safari ilikuwa ni nzuri ya ya furaha zaidi. Wafalme hawa walizungumza mengi na kucheka utadhani mtu na mwanae. Walibeba zawadi nyingi na mali nyingi kutoka ufalme ule tajiri. Walipofika walizigawa mali zile kwa viongozi kulingana na vyeo vyao. Mfalme aliitisha mkutano mkubwa sana siku ilofata na akatangaza nia yake ya kutaka kumrithisha ufalme kijana yule na kumfanya kuwa ni mtoto wake. Basi mambo yakawa kama hivyo,
Nchi ilikuwa katika hali ya furaha sana kwa muda mrefu. mfalme alikuwa katika furaha kubwa zaidi kwa kupata mtoto na mrithi wa utawala wake. Yule mvuvi ambae ndio chanzo cha yote haya alipewa mali nyingi sana za kuweza kutumia yeye na vizazi vyake vingi vijavyo na akamfanya katika watu wake wa karibu. Kufikia hapa Dinar-zade akamaliza hadithi ya mvuvi. Hadithi hii mpaka kwisha ilichukuwa siku nyingi kwa mfale mpaka akalowea na hadithi. Dinar-zade aliponyeka kuuliwa kama hivi ikawa ikiisha hadithi analeta nyingine. Hivyo akaendelea kusimulia hadithi iliyonzuri kuliko hii ya mvuvi nayo i hii;-
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Mankaa Tarehe 2024-09-09 13:26:37 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 53
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Simulizi za Hadithi Audio
👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉4 Kitabu cha Afya
👉5 Madrasa kiganjani
👉6 Kitau cha Fiqh
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 2: Sultani mtoa buradani kufariki
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Bostani la kifalme baghadad
Muendelezo..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 2 Part 2: Hadithi ya mzee wa kwanza na mbuzi wake
Simulizi za HALIF LELA U LELA zipo nyingi sana na husikiliwa na kusomwa na wakubwa kwa wadogo pia hadithi hizi zimeenea duniani Kate zikisikilizwa na maelfu ya watu mbalimbali. Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 12: Sehemu ya tano ya safari ya Sinbad
Muendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 13: Sehemu ya sita ya safari ya Sinbad
Muendelezo wa safari ya Sinbad iliyopo ndani ya kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 10 Part 2: Ni ndoto ama kweli???
Muendelezo..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 7: Sehemu ya nne ya safari ya Sinbad
Muendelezo wa hadithi ya safari ya safari ya Sinbad iliyopo kwenye hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 7 Part 9: Familia mpya
Muendelezo..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 3 Part 3: Kisa cha mke na kasuku
Simulizi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza simulizii hii inasimulia kisa cha mke na Kahuku wake.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 1 Part 2: Simulizi ya kisa cha mfugaji na mkewe
Simulizii hii ni inatoka katika kitabu cha kwanza cha HALIF LELA U LELA Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 14: Simulizi ya binti wa kwanza na mbwa
Tuendeleee kuburudika na simulizii zetu nzuri kutoka katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 13: Simulizi ya nyani kibadilika kuwa chongo
Mwendelezo wa hadithi zetu nzuri na za kusisimua kutoka katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA..... Soma Zaidi...