Simulizi za Hadithi EP 10 Part 2: Ni ndoto ama kweli???

Muendelezo.....

NDOTO AMA KWELI?

Siku zikaenda hatimaye mwaka ukafika. Kamaralzamani akiwa bado anafikiria na kuwazuwa. Hatimaye mfalme akamuita tena na kumwambia “mwanangu, numekupa muda mrefu wa kusubiria jibu lako. Natamani sasa ni muda wa wewe kutoa maamuzi”. kamaralzamani akamueleza kuwa “baba bado sijafikiri kuoa, kwani bado sijaona anayenifaa na aliyenipendeza”. majibu haya yalikuwa kama mwiba kwenye masikio ya Mfalme.

 

 

Mwanangu mwaka mzima umeshindwa kumpata wa kukufaa. Ni maneno ya masikitiko ya mfalme. Mfalme akaondoka kwa jazba huku akimueleza kuwa kesho atatakiwa atoe maamuzi yake ya mwisho kabla ya kulazimishwa. Mfalme akamuendea mkewake na kumueleza hali nzima kisha akamtaka ashiriki katika kumshauri mtoto waokipenzi. Malkia alimuita Kamaralzamani na kumtaka azungumze bila ya kificho kuhusu kinachomsubuwa.

 

 

“mama sitoweza kuoa mwanamke nisiyempenda, tambuwa kuwa maamuzi ya ndoa ni maamuzi ya kimaisha eidha nijefurahia maisha ama niwe katika dhiki. Nitakapomuona atakayenipendeza nitakuwa tayari kuoa” ni maneno ya Kamaral zamani akimueleza mama yake. Kesho mfalme akamuita tena Kamaralzamani ili kujuwa maamuzi yake ya mwisho. Kamaralzamani akamueleza baba yake yale yale aliyomueleza mama yake. Mfalme alikasirika sana. Mfalme alitamani sana kumuona mjukuu wake haraka iwezekanavtyo.

 

 

Mfalme akaagiza kuwa Kamaralzamani afungiwe kwenye nyumba yake iliyo mbali na ikilu na ulinzi mkali uwe hapo. Asiruhusiwe kutoka nje mpaka pale atakapobadili maamuzi yake. Kwa upande mwingine Kamaralzamani alifurahia maamuzi haya kwa ni sasa angeweza kupata muda mwingi kusoma vitabu na kupumzika. Ijapokuwa kwa waliozoea kuchakarika kuambiwa uwe sehemu moja ni adhabu tosha. Basi mambo yakawa hivyo kama alivyotaka mfalme. Na Kamaralzamani aliwekwa ulinzini hata ikatimia wiki.

 

 

Katika lijumba ambalo kamaralzamani amefungiwa kulikuwa na kisima cha zamani sana. Kisima hicho inasemekana ina miaka kati ya 30 mpaka 50. hakuna aliyeweza kudhibiti vyema hesabu ya kisima hicho. Katka kisima hicho kuliishi familia moja kubwa ya majini. Jini Maimuna akiwa ni mmoja wapo wa majini hao. Sikumoja usiku jini naimuna alitoka kwenye kisima. Aliingia ndani ya jumba hilo na kukuta sura ngeni. Loo alikuwa ni kijana mwenye sura nzuri kamwe hajapatapo kutokea katika nchi ile.

 

 

Jini maimuna alistaajabu sana kwa uzuri wa kijana hata akatamani angelikuwa yeye binadamu aolewe. Baada ya kustaajabu kwa muda mrefu Maimuna aliondoka na kupotelea angani akielekea nchi za mashariki ya mbali, hata akafika mipakani mwa china na India, pembezoni mwa milima mirefu sana. Huko akakutana na jini Makata. Jini makata alikuwa na nguvu sana na mbawa zake zilikuwa na sauti za kunguruma hewani. Jini maimuna aliogopa sana kwani hakuwa na amani mbele ya jini makata.

 

 

Makata: “unatoka wapi maimuna” Natokea nchi za mashariki ya kati” Je una mpya yeyote unisimulie”, ndio nimekuytana na akijana Mzuri sana huko nitokako, kwa uzuri huo hata mwanamke wa kumzidi hajapatikana.na kijana huyo ni wa kiume” “ wee basi kijana wako hawezi kushinda uzuri wa binti niliyemuona huko kwa mfalme wa china, uzuri ambao duniani hajapatapo kutokea zaidi yake” yalikuwa ni majibizano kati ya makata na Mainuna.

 

 

Siku zoyte makata alikuwa anashinda kwenye ugomvi wa majibishano kutokana na ukubwa wake, ujeuri, hasira na uwezo wake wa kubishana. Lakini leo maimuna nae aliendelea kukomaa na ubishi. Mwisho wa mapishano waliamuwa kutafuta suluhu.wakaamuwa kumtafuta mwenzao awasuluhishe mgogoro wao. Katika kupitapita ndipo wakakutana na Subiani jini wa Misituni. Baada ya kuelezwa ugomvi subiani akaamuwa kuwakutanisha vijana wote wawili kisha aamshwe mmojammoja, atakayestaajabu zaidi kwa mwenzie atakuwamshindi wa pili.

 

 

Basi wakamchukuwa Binti wa china na kumpeleka mashariki ya kati kwa kamaralzamani. Katika kitanda kimoja wakawalaza. Wakaanza kumuamsha binti, aliyejulikana kwam jiana la Nurati. Alipoamshwa alistaajabu sana kuona kuna kijana mzuri sana pembeni yake. Nurat alitokea kumpenda palepale kijana yule, akachukuwa pete mbili alizokuwa nazo kisha akamvisha pete moja kama ishara ya upendo. Hapo majini wale wakampulizia usingizi na akalala fofofo.

 

 

Kisha wakamuamsha kamaralzamani naye alistaajabu kama alivyostaajabu mwenzie. Akajiuta ana pete kama ya yile binti pale alipolala. Pete zilifanana. Kamaralzamani akajuwakuwa ni huyu binti amemvalisha. Kisha wale majini wakampulizia usingizi naye akalala fofofo. Majini hawa wakamrudisha Nurat huko walikomtoa na Kamaralzamani wakamrudisha kwenye kitanda chake. Majini walipata suluhisho kuwa wote wawili ni wazuri sana hakuna aliyemzidi mwenzie maana wanafanana sura zao. Majini wale waliondoka huku wamesahau kuaachanisha zile pete zao.

 

 

Asubuhi kamaralzamani anaamka akawaza alichokiona jana, akaangalia godoro tupu. Mwanzo akajiwa ni ndoto tu lakini alipoangalia kidoleni mwake kuna pete akajuwa ni kweli si ndoto. Hali kama hii nayo ilikuwa kwa binti wa mfalme wa nzchi za mashariki ya mbali Nurat ambaye naye alijuwa ni ndoto ila alipoona pete hana amebakiwa na moja akajuwa ni kweli.

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Mankaa image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Burudani File: Download PDF Views 425

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 Madrasa kiganjani    👉4 Simulizi za Hadithi Audio    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 10: Ndoa ya binti mfalme na Sinbad

Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza muendelezo......

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 2 Part 2: Hadithi ya mzee wa kwanza na mbuzi wake

Simulizi za HALIF LELA U LELA zipo nyingi sana na husikiliwa na kusomwa na wakubwa kwa wadogo pia hadithi hizi zimeenea duniani Kate zikisikilizwa na maelfu ya watu mbalimbali.

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 8: Simulizi ya chongo wa tatu mtoto wa mfalme

Muendelezo wa hadithi ya mtoto wa mfalme mwenye chongo katika hadithi ya HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza.....

Soma Zaidi...