Posti hii inahusu zaidi sheria za kutunza usafi wakati wa upasuaji, iwapo sheria mojawapo ikienda kinyume ijulikane kuwa usafi haujaenda sawa na pengine kwa kitaalamu huitwa contamination.
Sheria za usafi wakati wa upasuaji.
1.kifaa chochote ambacho kimegusa kidonda cha mgonjwa uhesabiwa kubwa ni kichafu na kinapaswa kufanyiwa usafi kwa kuanzia kwenye ndoo yenye maji ya sabuni, baadae kwenye maji ya chlorine na baadae kwenye maji masafi na baada ya hapo upelekea na kuunguzwa ili kuua wadudu wote na baadae kutumiwa tena. Kwa hiyo hata kama chombo kimegusa kwa sehemu ndogo kinaesabiwa kuwa ni kichafu.
2.Sehemu yoyote safi inapaswa kukutana na sehemu nyingine ambayo ni safi na sehemu chafu inapaswa kukutana na sehemu chafu, ikiwa sehemu ya kifaa kilicho safi limekutana na sehemu nyingine ya kifaa iliyochafu hata sehemu ndogo kifaa hicho kinaesabiwa kubwa ni kichafu kwa hiyo kinapaswa kusafishwa kwa utaratibu unaofaa.
3.Kwa upanda wa wafanyakazi au wahudumu wa kwenye chumba cha upasuaji wanapaswa kutembea kutoka kwenye sehemu safi kwenda sehemu safi na kutoka sehemu chafu kwenda chafu, ikitokea mmoja anatembelea kwenye sehemu safi kwenda chafu anaesabika kubwa hazingatii usafi na anapaswa kubadilisha nguo na kunawa vizuri ndipo anaruhusiwa kuendelea na shughuli za upasuaji.
4.Kutembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine ila sehemu iliyo safi wakati wote wa upasuaji haina maana kwamba umekosea sheria za usafi wakati wa upasuaji, kwa sababu kuna vitu vinapaswa kutolewa sehemu moja kwenda nyingine, ila kama ni kutembea sehemu chafu na kurudi kwenye sehemu safi hapo kuna makosa.
5.Sehemu yoyote kwenye chumba cha upasuaji inapaswa kukingwa kutokana na unyevunyevu kwa maana unyevunyevu utunza uchafu mwingi sana na kusababisha magonjwa mengi na Maambukizi kwa mgonjwa kwa hiyo chumba cha upasuaji kinapaswa kusafishwa mda wote na kuhakikisha kubwa kinabaki safi hata mtu akigusa kwenye sehemu yoyote hasitoke na vumbi.
6.Wakati wa kufanya upasuaji vifaa vyote ambavyo ni safi na vinapaswa kutumiwa kwa mda huo vinapaswa juwa wazi na vinaonekana kwa hiyo wahudumu wanaohusika na vifaa wanapaswa kuwa karibu ili kuweza kuweka vifaa karibu na kuepuka kutoka sehemu moja na kwenda nyingine, kwa hiyo maandalizi ni ya maana kwa mtunza vifaa.
7.Kifaa chochote ambacho kinatiliwa mashaka kuhusu usafi kinaesabiwa kubwa ni kichafu kama kinapaswa kusafishwa na kutumia kama kinahitajika, kwa hiyo waandaaji wa vifaa wanapaswa kuwa makini katika kuandaa vifaa vyao ili kuepuka makosa wakati wa upasuaji na kutilia mashaka kwa baadhi ya vifaa.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa nguo za upasuaji, tunajua wazi kuwa, wakati wa upasuaji tunapaswa kusafisha chumba na mazingira yake lengo ni kuhakikisha kuwa tunazuia wadudu wasisambae au kuingia kwenye mwili wa binadamu.
Soma Zaidi...Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Sababu zinazopelekea kukosa usingizi. Usingizi ni ugonjwa unaoendelea ambao unaweza kufanya iwe vigumu kusinzia, vigumu kubaki usingizini au vyote viwili, licha ya fursa ya kupata usingizi wa kutosha.Ukiwa na kukosa usi
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuzuia dalili za hatari kwa aliyefanyiwa upasuaji, ni mbinu mbalimbali ambazo utumika ili kujaribu kuepuka Dalili za hatari kwa aliyefanyiwa upasuaji.
Soma Zaidi...Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kutunza chumba cha upasuaji, chumba cha upasuaji ni tofauti na vyumba vingine kwenye hospitali kwa hiyo vinahitaji uangalizi wa hali ya juu sana ili kuepuka aina yoyote ya uchafu kuwepo kwenye chumba hicho, zifuatazo ni na
Soma Zaidi...