Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa nguo za upasuaji, tunajua wazi kuwa, wakati wa upasuaji tunapaswa kusafisha chumba na mazingira yake lengo ni kuhakikisha kuwa tunazuia wadudu wasisambae au kuingia kwenye mwili wa binadamu.
Umuhimu wa nguo za upasuaji.
1.Nguo za upasuaji zinaweka umbali kati ya mgonjwa na mhudumu ili kuepuka kusambaa kwa Magonjwa kutoka kwa mhudumu kwenda kwa mgonjwa na kutoka kwa mgonjwa kwenda kwa mhudumu kwa kufanya hivyo utaratibu na nidhamu ya upasuaji uende vizuri likiwa na lengo kuu ambalo ni kuzuia kusambaa kwa Magonjwa wakati wa upasuaji, kwa hiyo wahudumu wa afya wanapaswa kushika sheria za kuvaa nguo hizi. Ambao hawafanyi hivyo wanapaswa kuchukuliwa hatua.
2. Vile vile nguo za upasuaji usaidia kuzuia damu na majimaji ambayo yanaweza kutoka kwa mgonjwa kwenda kwa mhudumu, ikitokea kwa bahati mbaya maji yakaruka kutoka kwa mgonjwa kwenda kwa mhudumu spidi ya kwanza yatafikia kwenye apron na hayataweza kumfikia mhudumu, kwa hiyo wahudumu wa upasuaji wanapaswa kujikinga na magonjwa kwa kuvaa nguo za upasuaji kwa kufuata mtiririko wote kwa sababu wakati wa upasuaji chochote kinaweza kutokea.
3.Pia nguo za upasuaji usaidia kuzuia magonjwa na chemikali nyingine kusambaa kutoka kwa mgonjwa kwenda kwa mhudumu kwa mfano kama mgonjwa ana Maambukizi ya ukimwi, na homa ya ini katika kufanya upasuaji ukiwa na nguo za upasuaji unaweza kuepuka na magonjwa haya, kwa hiyo wahudumu wawe makini sana katika kutumia nguo za upasuaji ili kuepukana na magonjwa na kemikali nyingine zinazotumika wakati wa upasuaji.
4. Kwa hiyo baada ya kujua faida za nguo za upasuaji kila kituo cha afya wanapaswa kuwa na nguo zote za kufaa na zinapaswa kusafishwa kwa wakati na kwa utaratibu maalum na pia wanaoziandaa wanapaswa kuwa waangalifu na kuwa na ujuzi katika kazi hiyo, pia na wahudumu wanaozivaa wanapaswa kuwa na moyo wa kujali wa kutumia nguo hizo kwa wakati wake na kwa usahihi kwa sababu wasipozitumia wanaweza kuhatarisha maisha yao na wagonjwa pia.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Posti hii inahusu zaidi nguo za kuvaliwa kwenye chumba cha upasuaji na kazi zake, hizi ni nguo ambazo wahudumu wa afya wanapaswa kuzivaa wakati wa upasuaji kwa ajili ya kuwakinga na Maambukizi kati ya wahudumu wa afya na wagonjwa pia
Soma Zaidi...Figo ni moja katika orgn zenye umuhimu sana mwilini na endapo itaatirika kwa namna yeyote ile, madhara makubwa kwenye mwili yanaweza kutokea na hata kifo. Katika post hii utajifunza jinsi ya kulinda mwili wako dhidi ya matatizo ya figo
Soma Zaidi...Zijuwe nyakati ambazo dua inakubaliwa kwa haraka zaidi. Zijuwe nyakati ambazo ukiomba dua hitakubaliwa.
Soma Zaidi...Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.
Soma Zaidi...Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...Kama tulivyosema hapo juu kuwa afya ni kuwa mzima kimwili na kiakili.
Soma Zaidi...