Yajuwe masharti ya udhu yaani yanayofanya udhu kukubalika

Posti hii itakufundisha masharti yanayohitajika kwa mwenye kutaka kutia udhu.

Masharti ya udhu

Ili udhu wa mtu ukamilike hapana budi kuchunga na kutekeleza masharti yafuatayo kabla ya kuanza kutawadha:

 


(i)Kuwa na “maji safi” ya kutosha kuweza kutitirika (yasiwe ya kupakaza tu) katika viungo vya udhu vinavyooshwa.

 


(ii)Kutokuwa na kitu kilichogandamana (kama vile lami, rangi, ulimbo, n.k) kitakachoweza kuzuia maji kufika kwenye ngozi ya viungo vya udhu. Ni lazima mtu aondoe hicho kilichogandamana ndio aanze kutawadha.

 

(iii)Kutokuwa na uchafu mwingineo au vumbi,la aina yoyote au kitu chochote juu ya viungo vya kutawadhia kitakachobadilisha rangi, harufu au tamu ya maji yatakayotiririka humo. Ni sharti mtu awe msafi kwanza ndipo aanze kutawadha.

 


(iv)Kuondoa najisi juu ya viungo vya udhu kabla ya kuanza kutawadha.

 


(v)Kukata kucha ndefu zinazozuia maji kufikia kona za vidole, kabla ya kuanza kutawadha.

 


Masharti haya haya ndiyo masharti ya kuoga katika kuondoa hadathi ya kati na kati na hadathi kubwa, bali pamoja na hayo,kwa wanawake wenye kusuka, hawana budi kufumua misuko yao isiyoruhusu maji kupenya.

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1461

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 kitabu cha Simulizi    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana: