Namna ya kutawadha yaani kuchukuwa udhu

Kuchukuwavudhu ni ibada, lakini pia ni matendo ya kuufanya mwilivuwe safi. Katika post nitakwenda kukifundisha namna ya kutia udhu katika uislamu.

Ili uweze kutawadha kwanza unatakiwa uandae maji yaliyo safi.  Maji safi ni yale ambayo hayajachanganyika na najisi na yakawa yamenajisika. 

 

Baada ya kuandaa maji yako sasa ni wakati wa kutekeleza ibada ya udhu.  Vyemakuanza kupigamswaki.  Kwani kupiga mswaki ni sunnah ambazo zimesisiyizwa sana katika Uislamu. 

 

Hatuwa za kuchukuwa udhu:

1. Kutia nia:

Nia ni kukusudia kitendo. Hii ni hatuwa ya kwanza na muhimu kwani Mtume s.a.w amesema "kila jambo hulipwa kwa kuzinhatia nia" hadithi ni sahihi. 

 

2. Anza na kupiga bismillah kisha osha kiganja vya mikono.  Osha kwanza kabla hujatumbukiza mikono kwenye chombo. 

 

3. Kisha osha uso: 

Uso unatakiwa uoshwe kwa marefu hake na mapana.  Hakikisha unaziosha sehemu zote za uso kama kwenye kidevu na kufika hadi kwenye maoteo ha masikio.  Uoshaji wa uso unaambatana na kusukutuwa na kuingiza maji puani. 

 

Hivyo basi kwa mpanhilio utaanzakusukutuwa kisha utaingiza maji puani.  Utafanya hivi mara tatu kisha ndipo utaosha uso pia utaosha mafa tatu.  Pia utaosha na kwenye ndevu kuhakikisha kuwa ngozi ya kidefu imepata maji. 

 

4. Kuosha mikono. 

Baada ya kumalizakuosha uso utaosha mikonokwa utaratibu utaanza mkono wa kulia mara tatu kisha mkono wa kushoto mara tatu. Hakikisha kuwa mkono unauosha mpakakwenye kiwiko.  Vyema ukafika juu zaidi. 

 

Endapo mkonoutakuwa huna amaumekatwa utaosha kipande kilichopo.  Baa ya kumaliza mkono wa kulia utaosha wa kushoto. 

 

5. Kupaka maji kichwani: 

Hapa utafanya hivi mara moja kama alivyokuwa akifanya Mtume S.A.W. Hata hivyo hakuna ubaya ukizidisha.  Lengo hapa ni kuoaka maji kichwani na si kuosha nywele. 

 

Upakaji wa maji utaendana na kupaka maji kwenye masikio. Nje ya masikio nandani yake. Kidole cha cha shahada kiingie ndani yavsikio na gumba kipake juu ya sikio. 

 

Ni katika sunnah kutumia maji yaleyale yaliotumika kupakakichwa.  Yaani baada ya kupaka maji kichwani utaingiza kidole cha shahada ndani ya sikio,  kisha gumba wwka juu ya pindo za sikio kwa juu na kupaka maji. 

 

Unapopaka kichwa utaanzia mbele kuja nyuma kisha utatoa nyumana kuleta mbele,  kisha ndipp utamalizia masikioni .

 

6. Kuosha miguu

Kisha utaosha miguu miwili mara tatutatu.  Utaanza wa kulia na kumalizia wa kushoto.  Hakikisha maji yanaingia mpaka kwenye mipasuko ya miguu yaani magaga.  Hakikisha unaosha mpaka kwenye fundo zamiguu yaani kungu za miguu. Vyema ukizidisha mpaka kwenye ugoko. 

 

Baada ya hapo utakuwa umeshatia udhu. Usikose post inayofuata itazungumzia dua ya kumaliza kutia udhu. 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1901

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 Bongolite - Game zone - Play free game    👉4 Kitau cha Fiqh    👉5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)   

Post zinazofanana:

Kusimamisha swala za Sunnah

Nguzo za uislamu, kusimamisha swala za Sunnah (EDK form 2: Dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Sharti za kutoa zaka

Masharti ya Utoaji wa Zakat na Swadaqat Utoaji katika njia ya Allah (s.

Soma Zaidi...
Nafasi ya serikali katika ugawaji

Serikali ina nafasi katika kufanya mgawanyiko katika uchumi.

Soma Zaidi...
Hukumu ya talaka iliyotolewa kabla ya tendo la ndoa

Endapo mtu atamuacha mke wake kabla hata ya kukutana kimwili, basi talaka hii itahukumiwa kwa namna hii.

Soma Zaidi...
Tofauti kati ya hijjah na umrah

Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...