Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za minyoo na sababu zake
Dalili za minyoo, sababu zake na kuiepuka minyoo.
Minyoo ni katika wadudu vimelea vinavyowapa shida watu wengi leo hii. Minyoo sio virusi wala bakteria kama ambavyo watu wengi wamekuwa wakidhania.minyoo ipo katika makundi meengi na huishi katika maeneo mbalimbali kwenye miili yetu ikiwemo tumbo, ini, utumbo, ubongo na kwenye damu na maeneo mengine. Dalili za minyoo hutofautiana sana kulingana na aina ya minyoo na wapi ipo. Lakini zipo dalili zenye kufanana kwa minyoo wote. Katika makala hii nitakwenda kukujuza baadhi ya dalili za minyoo katika mwili wako, pia tutaona sababu za kupata minyoo, wapi minyoo inapatikana na vipi tutaizuia:-
Utaweza kupata minyoo katika hali zifuatazo:-
1.kula kitu kisichooshwa kwema kwa maji yaliyo safi na salama
2.Kunywa maji ambayo si masafi na si salama
3.Kula nyama ambayo haikuiva vyema, ama nyama mbichi
4.Kutembea pekupeku kwenye ardhi yeye minyoo
5.Kula udongo,
6.Kinyesi cha wanyama na binadamu
DALILI ZA MINYOO
Wakati mwingine ni vigumu sana kujua kama una minyoo, kwani minyoo wanaweza kukaa ndani ya mwili kwa muda mrefu bila ya kuonesha dalili yeyote, ama madhara yeyote. Na dalili za minyoo pia hutofautiana sana, kulingana na aina za minyoo. Lakini zifuatazo ni katika dalili kuu:-
1.Kichefuchefu
2.Kukosa hamu ya kula
3.Maumivu ya tumbo
4.Kupungua uzito
5.Uchovu wa viungo
6.Kuona utelezi mwingi kama kamasi kwenye kinyesi
7.Kuona minyoo kwenye kinyesi.
8.Kuona damu kwenye kinyesi
9.Tumbo kujaa
Dalili hizi kama nilivyotangulia kusema kuwa zinatofautiana kulingana na aina ya minyoo. Sasa hebu tuone kwa ufupi dalili hizi kulingana na aina ya minyoo:-
1.minyoo aina na tapeworm dalili zao ni:
A.Kuvimba kwa ngozi ama kujaa ama kujaa kwa tumbo
B.Kuwa na alegi
C.Kuwa na homa
D.Matatizo katika mfumo wa fahamu, kama kifafa
2.minyoo aina ya hookworm dalili zao ni kama:-
A.Kuwashwa
B.Kupata ugonjwa wa anaemia (upungufu wa seli hai nyekundu kwenye damu) hivyo kukosa oksijeni ya kutosha mwilini
C.Kuwa na uchovu wa hali ya juu.
3.minyoo aina ya trichinosis, minyoo hawa wana dalili kama:-
A.Kupata homa
B.Kuvimba kwa uso
C.Maumivu ya misuli na kuchoka
D.Maumivu ya kichwa
E.Kutokupenda kupigwa na mwanga
F.Matatizo katika macho (conjuctivist)
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Posti hii inahusu zaidi namna au njia za kuepuka na Ugonjwa huu wa ngiri ambao uleta madhara kwa watoto, vijana na watu wazima, kwa hiyo ili tuweze janga hili ni lazima tufanye yafuatayo.
Soma Zaidi...Watu wengi wamekuwa wakijiuliza kuwa ukimwi huonekana baada ya muda gani toka kuathirika?
Soma Zaidi...Pisti hii inahusu zaidi dalili za mtoto mwenye Maambukizi ya ugonjwa wa Dondakoo, tunajua wazi kuwa ugonjwa huu uwashambulia hasa watoto wadogo ambao wako chini ya miaka mitano, kwa hiyo zifuatazo ni baadhi ya Dalili zinazoweza kujitokeza kwa watoto hawa.
Soma Zaidi...HATUA ZA KUJIKINGA NA VIDONDA VYA TUMBO Unaweza kupunguza hatari yako ya vidonda vya tumbo ikiwa unafuata mikakati sawa inayopendekezwa kama tiba ya nyumbani kutibu vidonda.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi Sababu za uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo, hali hii uwatokea sana wanawake zaidi ya wanaume, kwa kitaalamu hali hii ya kuwa na uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo huitwa cystitis.
Soma Zaidi...Tambuwa kiungulia, sababu zake, dawa za kiungulia na namna ya kupambana na kiungulia
Soma Zaidi...Posti hii inaonyesha Dalili na ishara za kuvimba kope ambayo kitaalamu hujulikana Kama blepharitis.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia ambazo VVU huambukizwa
Soma Zaidi...Hapautajifunza rangi kuu za mkojo na dalili zako kiafya, mkojo mchafu na dalili zake
Soma Zaidi...