Hapa utajifunza maana ya Tajwid kilugha na kisheria. Pia nitakujuza jukumu ya kusoma tajwid.
Neno ‘Tajwiyd ’
linatoka na neno جَ و د (jawwada) kilugha ina maana ‘ufundi’, yaani kufanya kitu kwa uhodari au ustadi.
Maana yake Kishariy’ah: Kuitamka kila herufi kama inavyotakiwa kutamkwa, kwa kuipa haki yake na swiffah zake huku ukifuata hukmu zote za Tajwiyd.
Katika qurani na sunnah imehimizwa sana kusoma qurani kwa tajwid au tartila. Elimu hii ya tajwid imeanza zamani toka enzi za masahaba na toka mtume yupo hai. Pia alikuwa Mtume akiwaelekeza masahaba kwa watu maalumu ili wapate kujifunza qurani kiufasaha. Imepokewa kuwa Mtume (s.a.w) amesema: ((Mwenye kupenda kuisoma Qur-aan kama vile ilivyoteremshwa basi na asome kwa Qiraa-ah [kisomo] cha ibn Ummi ‘Abd)) (amepokea Ibn Majah na ahmad)
Pia Allah amesema :وَرَتِّلِ ٱلْقُرْءَانَ تَرْتِيلً “na soma Qur-aan kwa tartiylaa (kisomo cha utaratibu upasao” Katika kuonesha maana ya neno tartiyla ‘Aly Ibn Abi Talib ambaye ni khalifa wa nne baada ya kufariki mtume amesema: التَّتيلُ هُوَ تَجيد الحْوفَ ومَ عْ رِفةِ الوقوفِ “Ni kuisoma Qur-aan kwa ujuzi wa kutamka herufi ipasavyo na kuwa na ujuzi wa hukmu za kusimama”
Hukumu ya kujifunza tajwid:
Kusoma qurani bila ya tajwid yaani kuchunga herufi ni katika makosa mbele ya maulamaa wa tajwid. Maulamaa wa elimu hii wanazungumza kuwa kujifunza tajwid ni faradh al-kifaya kwa kauli za walio wengi. Pia wapo wanaosema ni faradh ‘ayn yaani ni faradhi ya lazima kwa kila muislamu.
Hawa waliosema ni faradhi kifaya yaani sio faradhi ya lazima kwa wote ila inatosha kwa wachache wakiwa na elimu hii, kundi hili pia linazungumza kuwa inapasa kwa msomaji asisome kwa kukosea ijapokuwa hajui hukumu za tajwiid. Yaani achunge matamchi kama yalivyoandikwa asije akatamka vinginevyo na kubadilisha maana.
Umeionaje Makala hii.. ?
Surat al Baqarah ni katika sura ambazo tunapaswa tuwe tunasoma mara kwa mara. Post hii itakufundisha kuhusu fadhila za sura hii.
Soma Zaidi...DARSA ZA TAJWID YALIYOMOSURA YA 01 .
Soma Zaidi...Qalqala imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Qalqalatul qubra yaani qalqala kubwa na qalqalat as shughura yaani qalqala ndogo.
Soma Zaidi...Qur-an inavyogawa MirathiMgawanyo wa mirathi umebainishwa katika Qur-an kama ifuatavyo:Mwenyezi Mungu anakuusieni juu ya watoto wenu: Mwanamume apate sawa na sehemu ya wanawake wawili.
Soma Zaidi...2:UUMBWAJI KWA MAJI YA UZAZIUumbwaji wa mwanadamu umepitia hatua mbalimbali na haya yote yamefanywa kwa sababumaalumu ili tipate mazingatio.
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha fadhila na faida za kusoma surat al Imran
Soma Zaidi...