Qurayh ni jina la kabila la Mtume Muhammad S.A.W. Sura hii itakwenda kukujulisha neema ambazo Maquraysh wamepewa na hawataoewa wao wowote baada ya wao.
SURAT AL-QURAYSH
Sura hii ina majina mawili. Inaitwa Qureish na pia inaitwa Li ii laafi. Ibni Abbas anasimulia ya kuwa ilishuka Makka. Qureish ni jina la kabila lililotoka kwa Nadhir bin Kinana (Razi).
Wengine wanasema neno Qureish limetoka katika neno Qarsh ambalo ni jina la samaki mkubwa wa bahari anayekula samaki lakini yeye haliwi. Hivyo kwa ukubwa wa kabila lao na kwa kuheshimiwa na watu wote nao wakaitwa Kureish. Makureish walikuwa watu wa Makka na walinzi wa Kaaba, na kwa sababu ya kuilinda Kaaba waliheshimiwa sana.
Sura hii imeshuka kwa maqurayshi kama alivyosema Mtume (s.a.w) “Allah amewapa neema Maquraysh ambayo hajampa yeyote kabla yao na hatampa yeyote baada yao:
Ukhalifa umepewa mtu katika wao, uangalizi wa nyumba tukufu ya Allah umepewa mtu miongoni mwao, kazi ya kuwapa maji mahujaji imepewa mtu katika wao, utume umepewa mtu katika wao, wamepewa ushindi dhidi ya jeshi la tembo, walimuabudu Allah kwa miaka saba ambapo hakuna yeyote aliyekuwa akimuabudu Allah, na sura kwenye quran imeshushwa kwa ajili yao na hakuna yeyote aliyetajwa kwenye surahiyo ila wao (kwa kupewa jina la al-quraysh)
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Hapa utajifunza maana ya iqlab katika usomaji wa Quran kwa tajwid
Soma Zaidi...SURATUL-KAUTHAR Imeteremshwa maka, na sura hii imeshuka kwa sababu al-aAs ibn Waail.
Soma Zaidi...Asbab nuzul surat al bayyinh. Sura hii imeteremka Madina na ina aya nane.
Soma Zaidi...Kama tulivyoona kuwa id-ghamu ipo katika aina kuu mbili ambazo ni id-ghamu bighunnah na id-ghamu bighair ghumnah. Sasa hapa tutajifunza makundi mengine ya idhgamu.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu srat al fatiha, faida zake na maudhui zake
Soma Zaidi...Sura hii inaonya vikali tabia ya kusengenya na kusambaza habari za uongo. Wameonywa vikali wenye tabia ya kujisifu kwa mali, kukusanya mali bila ya kuitolea zaka.
Soma Zaidi...