QURAN NA SAYANSI
Uumbwaji kwa maji ya uzazi

2:UUMBWAJI KWA MAJI YA UZAZI
Uumbwaji wa mwanadamu umepitia hatua mbalimbali na haya yote yamefanywa kwa sababu maalumu ili tipate mazingatio. Kwani kila kitu ALLAH amejaalia kukiwekea sababu na ndivyo atuambiavyo katika quran;- ‘’.. .na tukampatia njia ya kupatia kila kitu’’ [18:84].

Baada ya binadamu wa kwanzqa kuumbwa kwa ugongo allah akajaalia binadamu waliofuata kuwaumba kwa mchanganyiko wa maji ya uzazi. Katika sehemu hii tutaona jinsi maji haya yalivyoelezewa katika kupatikaniwa umbo la binadamu. Maji haya yanapatikana kwa baba na kwa mama pia kama tutakavyoona katika kurasa za mbele.

Maji haya yapatikanayo kwa baba ndio yatachukuwa nafasi kubwa katika maelezo ya uumbwaji wa mwanadamu. Kwa ufupi manii ambayo kitaalamu huitwa semen ambapo ndani yake ndo kuna mbegu za uzazi ambazo kitaalamu huitwa spermyamezungumziwa katika quran kwa namna mbalimbali ambazo zitatupatia mazingatio. Kwa mfano ALLAH ametaja kuwa;-
1; maji yatokayo kwa kuchumpa
Miongoni mwa sifa za maji haya ya uzazi ALLAH ameyataja moja kwa moja katika quran pale aliposema;- ‘ ameumbwa mwanadamu kwa maji yatokayo kwa kuchumpa. Yatokayo katikati ya na mifupa ya mgongo mbavu ’ ’ [86:6-7]. hivyo maji haya yametajwa kuwa
1; yanatoka kwa kuchumpa
2; yanatoka katikati ya mifupa ya uti wa mgongo na mbavu. Kwa ufupi maji yaliyotajwa hapo ni manii yaani semen ambayo ndani yake ndo kuna mbegu za uzazi ambazo ni sperm. Pia itambulike kuwa maji yalayotajwa hapo yanatoka kwa mwanaume na si kwa mwanamke

Uthibitisho wa kisayansi
Uchunguzi unaonesha kuwa 95% ya manii[semen] ni majimaji yatokayo kwenye tezi zilizopo karibu na kibofu cha mkojo ambazo ni kama seminal vesicles, prostate na tezi zilizopo kwenye mrija wa mkojo [urethra]. Tezi hizi ambazo hutoa manii ni sawa kabisa kusema zipo katikati ya uti wa mgongo na mbavu.

Siotatizo kusema tezi hizo zipo katikati ya uti wa mgongo na mbavu kisa mbavu zipo juu kwani hata kichwa kipo katik\ati ya mabega ijapokuwa kichwa kipo juu.
Pia uchunguzi wa kisayansi unathibitisha kuwa 2% ya manii ni mbegu za uzazi yaani sperm ambazo hupatikana kwnye korodani[testes] na wakati wa kufikia ‘'ejaculation'' sperm husafiri kutoka kwenye korodani na kuelekea kwenye hizo tezi na kuchasngsnyika pamoja na kupatikana manii kisha manii husafiri kuelekea nje.
Manii kutoka kwa kuchumpa wakati wa ‘ejaculation na hukadiriwa yakiwa na mwendokasi [speed] wa maili 28 kwa saa wakati sperm zenyewe husafiri kwa mwendokasi wa nchi 8 kwa saa au 4 mphr.

2; mbegu ya uhai uliyo changanyika Umbile la mwanadamu limepitia hatua nyingi sana kama tutakavyoendelea mbele kuona lakini ukiachilia mbali na hatua zote alizopitia mwanadamu wakati wa kuumbwa lakini umbile la mwanadamu bado limebakia kuwa dhalili kama ALLAH anavyotueleza;-
‘‘ kwa yakaini umbo la mbingu na ardhi ni kubwa kuliko umbo la mwanadamu’’[40:57] Allah anatueleza kuwa amemuumba mwanadamu kwa mbegu ya uhai iliyochanganyika yaan
‘’nutfatin amshaaj ’ ’kama alivyosema
‘kwa hakika tumemuumba mtu kwa mbeguya uhai iliyo changanyika ’ ’ [76:2]

Kwa ufupi katika aya hii tunaelezwa kuwa mwanadamu ameumbwa kwa maji ya uzazi yaliyo changanyika. Wafasiri wa quran wamejaribu kuichambuwa vizuri aya hii kwa namna ambavyo Allah aliwajaalia. Tutaona pia jinsi gani aya hii invyolingana na uchunguzi wa kisayansi.

Uthibitisho wa kisayansi
Sayansi inakubaliana juu ya machanganyiko huu katika namna zifuatazo;-
1; uchunguzi wa kisayansi unaonesha kuwa ;-
Manii ni mchanganyiko wa mbegu za kiume yaani sperm na majimaji yatokayo katika tezi kama tulivyotaja hapo nyuma. Mbegu sperm huchanganyika na majimaji hayo yenye mchanganyiko wa citric acid, prostaglandin, flavin, ascobic acid, ergothioneine, cholesterol, phosphase, hyaluronidase na sperm.

Kwa ufupi manii ni mchanganyiko wa mbegu za kiume yaani sperm ambazo hutengenezwa kwenye korodani na kisha husafiri wa kati wa ‘’ejaculation”kuelekea kwenye zile tezi ambazo zinazalizha yale majimaji mengine na kupatikana manii yaani semen. Kisha manii haya hutoka nje kupitia urethra wakati wa ‘’ejaculation’’na kama yataingia katika mji wa mimba yaani uterus na kufika katika mirija ya falopia huko mchanganyiko wa pili unatarajiwa kutokea kama tutakavyoona.

2; uchunguzi wa kisayansi pia unaonesha kuwa;- Yai la mwanamke yaani ovumhutengenezwa kwenye ovary kisha baada ya kukomaa huingia katika mirija ya falopia kitendo hiki kinaitwa kitaalamu ovulation. Huko katika mirija ya falopia yai hili hukutana na sperm amazo ni mbegu za kiume na hapa ndo tunapata mchanganyiko wa pili.

Pia yai hili la mwanamke huwa linapatikana likiwa katika majimaji fulani kama zilivyo mbegu za kiume ambazo nazo hupatikana katika majimaji fulani. Ili mimba iweze kutungwa ni mpaka pale mbegu ya kiume sperm itakapochanganyika na yai la mwanamke yaani ovum tukio hili lote hutokea katika mirija ya falopia na kitaalamu kitendo hiki huitw ‘’fertilization’’

Yai la mwanamke huweza kusubiri mbegu ya kiume kwa muda wa masaa 48 tu likingoja kukutana na mbegu ya kiume katika mirija ya falopia. Na mbegu za kiume zinaweza kusubiri kwa muda wa masaa 78 zikisubiri kukutana na yai la mama katika mirija ya falopia.

Endapo mbegu ya baba yaani sperm haitachanganyika na yai la mama yaani ovum mimba haiwezi kutokea yaani mtoto hawezi kupatikana lamda kwa njia ya miujiza. Kitendo hiki cha kukutana hizi mbegu mbili ndo fertilization au fusion. Kwa hali kama hii mchanganyiko usipopatikana tukio muhimu la menstrationlinatarajiwa kutokea kwa wanawake walio katika umri wa kupata mimba.

Kwa ufupi maelezo haya yanatupa ufahamu juu ya pale alipotuamb ia Allah kuwa ametuumba kwa maji yaliyochanganyika ili atujaribu. Bila shaka quran imeendana sahihi na uchunguzi wa kisayansi juu ya maelezo ya aya hii.

3; Mchujo wa maji dhalili Katika aya nyingine tunakuja kupata funzo kuwa maji aliyoumbiwa mwanadamu licha ya kuwa na sifa zilizotajwa katika kurasa zilizopita ila pia maji haya yanasifa kuwa ni madhalili na pia na yamechujwa kama tunavyoelezwa katika quran;-
‘ ’Ambaye ametengeneza umbo la kila kitu, na akaanzisha umbo la mwanadamukwa udongo.
Na kisha akakifanya kizazi chake kwa mchujo wa maji yaliyo madhalili ’ ’[32:7-8]
‘je ! hatukukuumbeni kwa maji yaliyo madhalili? ’ ’ [77:20]

kwa ufupi matumizi ya neno sulala kwenye aya hii yanatupa picha hilisi kuwa sio maji yote yalitumika katika utungaji wa mimba bali kulifanyika mchujo wa majimaji hayo. Yaani ni sawa na kusema kuwa sio mbegu zote zilizomo kwenye majimaji ya manii zilitumika katika utungaji wa mimba bali mmajimaji haya ya manii yalichujwa na mengine kutumika na mengine kuachwa. Mchujo huu tukakuja uona vizuri hapo chini.

Uthibitisho wa sayansi
Sayansi inathibitisha kuwa sio kiasi chote cha mbegu za kiume yaan sperm hutumika katika utungaji wa mimba bali kiwango kidogo sana ndo hutumika kama tutakavyoona;-

1; sayansi inathibitisha kuwa manii ni mchanganyiko wa majimaji yapatikanayo katika tezi na mbegu za kiume zinazopatikana kwenye korodani. 95% ya manii ni majimaji hayo na 2% ni mbegu yaani sperm. Lakini katika utungaji wa mimba mbegu pekeyake ndo hutumika yaani katika kukutana kwa mbegu na yai majimaji mengine yanabakia pembeni na mbegu pekee ndo huhitajika katika utungaji wa mimba. Hivyo huu ni mchujo wa majimaji hayo

2; sayansi imegunduwa pia katika ejaculationmoja mwanaume hutoa mbegu zifikazo milioni 250- 300 lakini katika utungaji wa mimba mbegu moja tuu ndo hutumika vinginevyo chance ya kutumika mbili ipo lakini ni ndogo sana kwa baadhi ya mimba za mapacha. Huu bila shaka nao ni mchujo wa majimaji hayo.

3; katika tumbo la mama sehemu inayohusika katika utungaji wa mimba huwa na hali ya asidi hivyo hali hii huzifanya zile mbegu zilizo dhoofika kufa na kubakia zile zenye nguvu ambazo ndo zitakwenda kuminyana katika utungaji wa mimba. Hivyo hali hii pia inatupa picha jinsi mchujo huu unavyozidi kufanyika.

4; wakati mamilioni ya mbegu za kiume spermatozoansyanapokutana na yai huminyanakulilainisha na kupata nafasi ya kuingia ndani ili nuclear ya mbegu ikakutane na ile ya yai yaan ovum. Katika kiminyano hiki mbegu ya kwanza ikibahatika kuingia yai linatengeneza utando mgumu ambao utazuia mbegu nyingine kuingia. Hivyo hapa tunazidi kupatapicha zaidi jinsi mchujo huu unavyoendelea kufanyika.

Kwa kumalizia matumizi ya neno la kiarabu sulala limesaidia kutupa picha halisi ya kuwa majimaji haya yalichujwa kwa namna mbalimbali na kupata sample moja. Darsa hii itaendelea kwenye ukurasa wetu mkuu wa Quran na sayansi au au Bofya hapa