QURANI KATIKA ZAMA ZA SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Asalaalaamu alykum warahmatullah wabarakaatuh. Katika makalaa hii tutakwenda kuona jinsi ambavyo qurani imekuwa ikielezea mambo ya kisayansi na teknolojia. Mambo haya hayakuweza kujulikana wakati wa kushuka kwa quran kutokana na ufinyu wa elimu hii kwa watu..

1; UMBWAJI WA MWANADAMU
Katika sehemu hii tutaangalia jinsi maumbile ya binadamu yalivyofanyika kwa mnamna ambayo allah ameitaja katika quran. Hapoa tutaangalia aya mbalimbali zinazozungumzia maumbile ya mwanadamu. Pia tutaona jinsi ganai sayansi inalingana na maelezo ya aya hizo. Kwa ufupi namna ambavyo allah amemuumba mwanadamu sio rahisi kuweza kuelezea ila tutaangalia hatua tuu ambazo mzimejaribu kuelezea namna ya uumbaji wa mwanadamu ulivyokuwa unashangaza. Kwa ufupi uumbwaji wa mwanadamu tunaweza kuuangalia katika namna zifuatazo;-

1; AMEMUUMBA KWA UDONGO
Zipo aya nyingi zinazoelezea kuwa chimbuko la mwanadamu wa kwanza ni udongo yaani ameumbwa mojakwamoja kwa kutumia udongo. Baada ya hapo namna ya uumbaji wa wanadamu waliofuata ilibadilika na kuwa kwa kutumia mbegu ya uzazi. Baadhi ya aya zinazoelezea tukio hili la uumbwaji kwa udongo ni kama ifuatavyo;-

''na kwayakini tulimuumba mwanadamu kwa udongo uliosafi ' ' [quran 23:12] ' 'ambaye ametengenezumbo la kila kitu, na akaanzisha umbo la mwanadamu kwa udongo.Na kisha akakifanya kizazi chake kwa mchujo wa majiyaliyo madhaifu. [quran 32:7-8]

Kwa ufupi aya hizi zimetuwezesha kujuwa hatua za uumbwaji wa mwanadamu zilivyo pitia ambazo ni;-
1; Binadamu wa [adam] aliumbwa kwaudongo nmoja kwa moja.
2; kisha binadamu waliofuata wakaumbwa kwa mchujo wa maji [manii].

Zipo aya nyingi tuu zinazoelezea khabari hii ya uumbaji kama;-22:5, 38:71, 40:67, 37:11.

UTHIBITISHO WA SAYANSI
Nukta ya msingi tunatakiwa tuitazame hapa ni ile iliyosema tumemuumba mwanadamu kwa udongo ulio safineno la kiarabu SULALA linatupa picha kuwa katika uumbwaji wa mwanadamu sio udongo wote umetumika isipokuwa baadhi tu ya udongo uliochujwa. Yaani udongo ulichujwa na kusafishwa vizuri na kuchukuliwa ule uliosafi kitaalamu tunaita SAMPLE.

Udongo umeudwa kwa element zinazopataikana ardhini. Sayansi imegunduwa element zaidi ya 100 ambazo zipo ardhini nazo ndo zilizotengeneza udongo. Kwakuwa mwili wa binadamu umeumbwa na udongo ni lazima element hizo pia zipatikane katiKa mwili wa binadamu. Upatikanaji wa element zilizomo kwenye udongo ndani ya mwili wa binadamu unatuthibitishia kuwa mwanadamu ameumbwa kwa udongo.

Uchunguzi wa kina wa mwili wa binadamu unaonesha kuwa element zote zilizounda mwili wa binadamu zinapatikana kwenye udongo. Uchunguzi huu unatuonesha kuwa jumla ya element zilizounda mwili wa binadamu ni 26 ila zipo 6 ambazo zipo kwa kiwango kikubwa[95%] ambazo ni;-
1; oxigen
2; nitrogen
3; salfa
4; kabon
5; fosforas
6; hydrojen

Pamoja na element nyinginezo mwili wa binadamu umeundwa kwa element 26 ambazo pia hupatikana kwenye udongo.
Nukta ya msingi hapa ni ile kauli ya kusema kuwa ‘’ tumemuumba mwanadamu kwa udongo uliosafi’’ [23:12]. Neno la kiarabu SULALA linatuonesha kuwa udongo alioumbiwa mwanadamu ulichujwa na kuwa safi yaani ulichunjwa na kuondolewa element zingine na kubakiziwa na element kadhaa.

Katika udongo kuna zaidi ya element 100 ila katika mwili wa binadamu kuna element 26. Hii inamaana kuwa kila element zilizomo katika mwili wa binadamu zipo katika udongo lakini si kila element iliyopo katikaka udongo ipo mwilini mwa binadamu. Kauli hii inatupa picha kamili ya mchujo huu wa udongo kutoka element zaidi ya 100 na kupata element 26 ambazo ndo zinajenga mwili wa binadamu nazo ni;- oxigen, kabon, hydrojen, kalsiam, fosforas, potasiam, salfa, klorine, sodiam, magnesiam, silikon, chuma, zink, kopa, boron, kobalt, vanadiam, iodine, seleniam, manganese, molybdeniam, na kroniam.

Mmoja katika waandishi wa kiislamu dr. Harun yahya amezungunza maneno yafuatayo‘’....when the human body is examined today, it may be discovered that many elements present on the earth are also to be found in the body living tissue contain 95% carbon, hydrogen, oxygen, nitrogen, phosphorus, and sulfur, with a total of 26 differents elements ’ ’[ kelvin griffin, ‘ ’the elemental composition of life ’ ’. www.Ideo. columbia. edu/dees/lect21. html].v