Suratul-takaathur (102) imeteremshwa makkah Ina aya nane

Quran (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

  1. Kumekughafilisheni (katika) kutafuta wingi (wa mali na jaha na watoto na kujifakharisha kwayo).
  2. Hata mmeingia makaburini (mmekufa kabla ya kufanya kheri yeyote).
  3. Sivyo hivyo! Karibuni hivi mtajua (kuwa sivyo hivyo).
  4. Kisha (nasema) sivyo hivyo karibuni hivi mtajua (kuwa sivyo hivyo).
  5. Sivyo hivyo! Lau kama mnajua ujuzi wa yakini (kuwa sivyo hivyo msingefanya hivyo).
  6. Hakika mtauona moto wa Jahiym.
  7. Kisha (nasema) mtauona (moto) kwa yakini.
  8. Kisha kwa hakika mtaulizwa siku hiyo juu ya neema mlizopewa (mlizitumiaje).

 

Mafunzo kwa Ufupi.

  1. Pupa katika kutafuta anasa za dunia ndizo hupelekea mtu kumuasi Mwenyezi Mungu (s.w).
  2. Kuchuma mali na kuhangaikia watoto sio jambo baya, bali lisitusahaulishe katika kumtumikia Mwenyezi Mungu (s.w).
  3. Kuwepo siku ya mwisho ni jambo lisilo na shaka ili kila mtu akaulzwe juu ya jinsi alivyotumia neema alizopewa.
  4. Kutumia vibaya neema na vipawa tulivyonavyo hupelekea kumuasi Mola wake na hivyo kustahiki adhabu.
  5. Neema na vipawa tulivyonavyo ni dhamana kwetu na tutaulizwa siku ya Kiama.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Quran Main: Dini File: Download PDF Views 1062

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Bongolite - Game zone - Play free game    👉6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana: