Sifa za Waumini zilizotajwa katika surat Ahzab

Bila shaka wanaume wenye kufuata vizuri nguzo za Uislamu, na wanawake wanaozifuata vizuri nguzo za Uislamu, na wanaume wanaoamini vizuri nguzo za Imani, na wanawake wanaoamini vizuri nguzo za Imani, na wanaume wanaotii, na wanawake wanaotii, na wanaume wa

Sifa za Waumini zilizotajwa katika surat Ahzab

Sifa za Waumini zilizotajwa katika surat Ahzab



Bila shaka wanaume wenye kufuata vizuri nguzo za Uislamu, na wanawake wanaozifuata vizuri nguzo za Uislamu, na wanaume wanaoamini vizuri nguzo za Imani, na wanawake wanaoamini vizuri nguzo za Imani, na wanaume wanaotii, na wanawake wanaotii, na wanaume wasemao kweli, na wanawake wasemao kweli, na wanaume wanaosubiri, na wanawake wanaosubiri, na wanaume wanaonyenyekea na wanawake wanaonyenyekea, na wanaume wanaotoa (Zaka na) sadaka, na wanawake wanaotoa (Zaka na) sadaka, na wanaume wanaofunga, na wanawake wanaofunga, na wanaume wanaojihifadhi tupu zao, na wanawake wanaojihifadhi, na wanaume wanaomtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi, na wanawake wanaomtaja Mwenyezi Mungu (kwa wingi) Mwenyezi Mungu amewaandalia msamaha na ujira mkubwa. (33:35)


Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanapokata shauri, wawe na hiari katika shauri lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotofu (upotevu) ulio wazi (kabisa). (33:36).



Mafunzo
Kutokana na aya hizi tunapata mafunzo yafuatayo:
Kwanza,
Muumini wa kweli ni yule anayejitahidi kwa kadiri ya uwezo wake kutekeleza yale yote yaliyoorodheshwa katika aya (33:35) na kutekeleza maamrisho mengine yote ya Allah (s.w) na Mtume wake pamoja na kuacha makatazo yote ya Allah (s.w) na Mtume wake. Kwa muhtasari sifa za waumini zilizoorodheshwa katika aya hizi ni hizi zifuatazo.



(i)Wenye kutoa shahada ya kweli kwa kutekeleza vilivyo maamrisho yote ya Allah(s.w) na kuacha makatazo yake yote.
(ii)Wenye kuziingiza katika matendo nguzo zote za imani.
(iii)Wenye kumtii Allah (s.w) na Mtume wake ipasavyo katika kukiendea kila kipengele cha maisha na kuwatii wenye mamlaka juu yao kwa mujibu ya maelekezo ya Allah (s.w) na Mtume wake.
(iv)Wenye kusema na kusimamia ukweli
(v)Wenye kujipinda katika kufanya subira katika kuendesha maisha yao ya kila siku na katika kusimamisha Uislamu katika jamii.
(vi)Wenye kujiepusha na kibri, majivuno, majigambo, n.k. katika kuhusuhubiana na watu katika mchakato wa maisha ya kila siku.
(vii)Wenye kutoa yale Allah(s.w) aliyowaruzuku kwa ajili ya kuwahurumia wenye kuhitajia na pia kwa ajili ya kuundeleza Uislamu na kuusimamisha katika jamii.
(viii)Wenye kuleta mara kwa mara funga za sunnah baada ya kuikamilisha funga ya Ramadhani na funga za kafara kwa yule aliyelazimika kwazo. Yaani wenye kuwa katika
swaumu angalu siku tatu kwa kila mwezi.
(ix)Wanaojihifadhi na zinaa na kujiepusha na vishawishi vyote vya zinaa.
(x) Wenye kumtaja na kumbumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi.



Pili, katika Uislamu waumini wanaume na waumini wanawake wana haki sawa mbele ya Allah (s.w). anayeheshimiwa zaidi mbele ya Allah ni yule aliye mchaji zaidi kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:


"Enyi watu! Kwa hakika tumekuumbeni (nyote) kwa (yule) mwanamume (mmoja, Adamu) na (yule yule) mwanamke (mmoja, Hawwa). Na tumekufanyeni mataifa na makabila (mbali mbali) ili mjuane (tu).Hakika aheshimiwaye sana miongoni mwenu mbele ya Allah ni yule amchaye Allah zaidi katika nyinyi. Kwa yakini Allah ni mjuzi mwenye habari (za mambo yote)." (49:13)




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Tawhid Main: Dini File: Download PDF Views 860

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 Dua za Mitume na Manabii    👉5 kitabu cha Simulizi    👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina   

Post zinazofanana:

Mafundisho ya Mitume

Mafundisho ya mitume ni eneo lingine linalo thibitisha kuwepo Allah (s.

Soma Zaidi...
(b)Umbile la Mwanaadamu ni la kidini

Ukizingatia maana halisi ya dini, kuwa dini ni utaratibu wa maisha, utadhihirikiwa kuwa umbile la mwanaadamu ni la kidini.

Soma Zaidi...
Kuamini vitabu vya mwenyezi Mungu (s.w)..

Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Humtegemea Mwenyezi Mungu peke yake

Hawamuogopi au kumtegemea yeyote kinyume na Mwenyezi Mungu.

Soma Zaidi...
MAANA NA HUKUMU YA TAJWIDI

Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa

Soma Zaidi...
Kumuamini malaika wa mwenyezi Mungu

Nguzo za Imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...