Muhutasari wa sifa za wanafiki
Kwa kuzingatia aya zote tulizozipitia juu ya wanafikitunaweza kutoa majumuisho ya sifa za wanafiki kama ifuatavyo:- (1)Hutenda kinyume cha imani wanaodai kuwa nayo.
Muhutasari wa sifa za wanafiki
Kwa kuzingatia aya zote tulizozipitia juu ya wanafikitunaweza kutoa majumuisho ya sifa za wanafiki kama ifuatavyo:-
(1)Hutenda kinyume cha imani wanaodai kuwa nayo.
(2)Hujaribu kumdanganya Mwenyezi Mungu pamoja na waumini wakidhani kuwa yaliyo nyoyoni mwao hayajulikani.
(3)Hufanya maovu katika ardhi huku wakidai kuwa wanatenda mema.
(4)Huwaona waumini wa kweli kuwa ni wajinga kwa kufuata kwao Uislamu inavyotakikana.
(5)Huwacheza shere Waislamu.
(6)Hujiiona kuwa wao ni bora kuliko waumini
(7)Hujikomba kwa viongozi wa kitwaaghuti.
(8)Huwafanya makafiri na Washirikina kuwa marafiki zao wa ndani badala ya Allah(s.w) Mtume wake na waumini.
(9)Huyapenda zadi maslahi ya dunia kuliko ya akhera.
(10)Hukataa kuhukumiwa na sheria za Allah (s.w).
(11)Hutumia viapo kama kifuniko cha maovu yao.
(12)Huchanganya haki na batili, kufuru na Uislamu.
(13)Huendea swala kwa uvivu.
(14)Hawamtaji Allah ila kidogo sana.
(15)Huwafitinisha Waislamu.
(16)Huchukia Waislamu wanapofikwa na kheri na kufurahia wanapofikwa na msiba.
(17)Hawako tayari kutoa mali zao katika njia ya Allah (s.w) na wakitoa chochote hutoa kwa ria
(18)Huwazuia watu kutoka katika njia ya Allah.
(19)Huzifanyia stihizai (shere) aya za Qur-an.
(20)Huamrisha maovu na kukataza mema.
(21)Husema uongo na kuvunja ahadi.
(22)Huwa vunja moyo na kuwakatisha tamaa Waislamu wa kweli ili wabakie katika ukafiri sawa na wao.
(23)Hufanya hiyana katika mambo ya kheri na kuchagua mambo mepesi mepesi.
(24)Wanawaogopa na kuwachelea watu zaidi kuliko Allah (s.w).
(25)Hush irikiana na maadui kuupiga vita Uislamu na Waislamu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 kitabu cha Simulizi 👉2 Madrasa kiganjani 👉3 Kitabu cha Afya 👉4 web hosting 👉5 Kitau cha Fiqh 👉6 ai web app
Post zinazofanana:
Maandalizi ya Hijra ya Mtume na Mafunzo tunayoyapata kutoka katika hijra hii
Maandalizi ya Hijra ya Mtume (s.
Soma Zaidi...Sababu ya uislamu kuwa ndiyo dini sahihi pekee
Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Kusingiziwa Nabii Sulaiman Uchawi
Pamoja na Ucha-Mungu aliokuwa nao Nabii Sulaiman watu hawakuacha kumsingizia mambo machafu.
Soma Zaidi...