image

Naman ya kuiendea quran na kuifanyia kazi baada ya kuisoma

Naman ya kuiendea quran na kuifanyia kazi baada ya kuisoma

Namna ya Kuiendea Qur-an



Pamoja na kujifundisha kuisoma Qur-an kwa kuzingatia hukumu zake na kuwafundisha watoto wetu hivyo, hatuna budi kuisoma Qur-an kwa mazingatio ili kufikia lengo la kushushwa kwake. Qur-an imeshushwa ili iwe mwongozo wa maisha yetu yote ya binafsi na ya jamii. Mtume (s.a.w) alipoamrishwa katika mwanzo wa Utume wake "Warattilil-Qur-an tar-tiilaa" - "na soma Qur-an vilivyo" haikuwa na maana ya kumtaka Mtume(s.a.w) kuisoma Qur-an kwa tajwidi kama wasomaji wa tajwid wanavyoghani, bali ni amri ya Allah (s.w) iliyomtaka Mtume(s.a.w) na wafuasi wake, wote wa ulimwengu mzima, waisome Qur-an kwa mazingatio ili waupate kwa uwazi ujumbe uliomo na waweze kuufuata vilivyo katika maisha yao ya kila siku. Wale wanaosoma aya za Qur-an bila ya kuzizingatia na kuziingiza katika utendaji Allah (s.w) amewalinganisha na punda’, mbwa, viziwi na vipofu


Mfano wa wale waliopewa Taurati kisha hawakuichukua, ni kama mfano wa punda aliyebeba vitabu. Ni mfano mbaya kabisa wa watu waliokadhibisha aya za Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu. (62:5).


..Basi mfano wake ni kama mfano wa mbwa, ukimkimea anahema, ukimwacha anahema.. (7:176).


"Viziwi, mabubu, vipofu, kwa hivyo hawatarejea (katika uongofu)." (2:18)


Kwa namna nyingine, Allah (s.w) anatufahamisha kuwa, waja wake anaowapenda atakaowaongoza katika njia iliyonyooka hapa ulimwenguni na kuwalipa ghorofa za Peponi na makazi mazuri kabisa, ni pamoja:


"Na wale ambao wanapokumbushwa aya za Mola wao hawaziangukii kwa uziwi na upofu." (25:73)
Kwa kuzingatia maelezo haya, ili tuweze kuongozwa na Qur-an hatuna budi kufanya yafuatayo:



(i)Tupitie kwa makini maelezo ya kitabu hiki ili tuwe na yakini kuwa Qur-an ni kitabu cha Allah (s.w) kisicho na shaka hata kidogo.



(ii)Kwa kuwa na yakini kuwa Qur-an ni ujumbe kutoka kwa Allah (s.w), hatuna budi kuisoma kwa mazingatio na kujitahidi kupata ujumbe unaotokana na kila aya.



(iii)Ili kuupata kwa uwazi ujumbe wa kila aya au kila sura ya Qur-an hatunabudi kusoma tafsiri na shereheza wanazuoni mbali mbali waliojitahidi kuitafsiri(kuifasili) Qur-an katika lugha tunayoimudu. Qur-an imetafsiriwa katika lugha mbali mbali kikiwemo Kiswahili na Kiingereza.



(iv)Baada ya kuupata kwa uwazi ujumbe wa Qur-an hatuna budi kuyaingiza maagizo ya Mola wetu katika utendaji huku tukimfanya Mtume (s.a.w) kiigizo chetu na huku tukizingatia msisitizo wa aya zifuatazo:


“Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata


shauri, wawe na hiari katika shauri lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotofu ulio wazi (kabisa)." (33:3 6)


"Na wasiohukumu kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri." (5:44)


Na wasiohukumu kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhalimu (5:45)


"Na wasiohukumu kwa yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio mafasiki(5: 47)



(v)Ili kuiingiza Qur-an yote katika maisha yetu ya kila siku na kujipamba na tabia ya Qur-an lazima kujenga tabia ya kuwa wasafiri wa Qur-an wa kudumu kwa kuipitia kwa mazingatio kuanzia sura ya mwanzo (Al-Faatiha) mpaka ya mwisho (An-Naas) na iwe ni ada yetu mpaka tutakapokufa. Kufanya hivyo Mtume (s.a.w) amefananisha na mtu kufanya safari ya kheri isiyokatika, ambayo ina malipo makubwa mbele ya Allah (s.w). Kuipitia Qur-an yote mara kwa mara kwa mazingatio humfanya muumini aweze kuishi katika mipaka ya Allah (s.w) katika kila kipengele cha maishayake.



(vi)Tuwe na tabia ya kuirejea Qur-an kila tunapokwama au tunapokabiliwa na tatizo lolote la kibinafsi au la kijamii. Tusiridhike kujifanyia au kufuata mkumbo katika kuendea mambo ya kibinafsi au ya kijamii bila ya kuangalia kwanza Allah (s.w) kasema nini au kaagiza nini juu ya jambo hilo


au Mtume wake (s.a.w) ambaye ndiye mfasiri wa Qur-an, ameliendeaje jambo hilo. Katika kusisitiza nukta hii tuzingatie agizo la Mtume (s.a.w) alilolitoa mwezi 9 Dhul-Hajj, 10 A.H. (633 A.D) katika uwanja wa Arafa katika Hija ya kuaga (Hijjatul-Wadaa) pale aliposema:
“Nimekuachieni vitu viwili ambavyo mkikamatana navyo hamtapotea abadan, navyo ni kitabu cha Allah (Al-Qur-an) na Sunnah ya Mtume wake."



(vii)Tufanye juhudi ya kusimamisha Uislamu katika jamii kwa mali zetu na nafsi zetu, ili tuweze kuufuata Uislamu wote katika kila kipengele cha maisha ya binafsi na ya jamii kama Qur-an yenyewe inavyo sisitiza:


"Enyi mlioamini! Ingieni katika hukumu zote za Uislamu, wala msifuate nyayo za shetani, kwa hakika yeye kwenu ni adui dhahiri." (2:208)



Ni dhahiri kwamba pale ambapo Uislamu haujashika hatamu za Uongozi wa jamii, Waislamu watakuwa hawana namna ya kutofuata nyayo za shetani katika siasa, uchumi, utamaduni na katika kila nyanja ya maisha ya jamii.Pale ambapo Uislamu haujasimama katika jamii, Waislamu watakuwa wanaswali huku chakula chao na kivazi chao kinatokana na uchumi haramu unaotokana na uzinzi, kamari, riba, ulevi, rushwa utapeli na mengineyo. Watakuwa wanafunga huku futari na daku yao inatokana na uchumi haramu, watakuwa wanatoa zakat na kuhiji kwa mali inayotokana na uchumi haramu; watakuwa wanamuabudu Mwenyezi Mungu wakiwa misikitini na wanapotoka misikitini hufuata sera na sharia zilizotungwa na matwaghuti mabungeni.Hivyo,ni wazi kuwa pale ambapo Uislamu haujasimama katika jamii, Qur-an haitapewa nafasi na kuwaongoza Waislamu katika kila kipengele cha maisha yao, jambo ambalo inabidi Waislamu waingie katika jihadi ili kupigania uhuru wao wa kuongozwa na Qur-an. Kama Waislamu watapuuza suala hili la jihadi na wakaridhika kuishi maisha ya mseto ya kutumikia miungu wawili - Allah (s.w) katika swala, zakat, saum, n.k na Twaghuti katika uchumi, siasa, sheria, n.k. wajue kuwa hawana ridhaa ya Allah (s.w) bali hali yao halisi ni ile inayoelezwa katika aya zifuatazo:


"… Je! Mnaamini baadhi ya kitabu na kukataa baadhi (yake)? Basi hakuna malipo kwa mwenye kufanya haya katika nyinyi ila ni fedheha katika maisha ya dunia, na siku ya Kiyama watapelekwa katika adhabu kali…" (2:85)


"Mwenyezi Mungu ni mlinzi (kiongozi) wa wale walioamini. Huwatoa katika giza na kuwaingiza katika nuru.Lakini waliokufuru walinzi (viongozi) wao ni matwaaghuti. Huwatoa katika nuru na kuwaingiza katika giza. Hao ndio watu wa motoni, humo watakaa milele. (2:25 7)




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 629


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Sababu za kushuka surat al Mauun
Sura hii ni katika sura ambazo zinahitaji kusomwa kwa mazingatio sana. Wanaoswali bila ya kuzingatia swala zao, wameonywa vikali sana. Wanaowatesa na kuwanyanyasa mayatima wameonywa vikali. Wanaowanyima wenye haja na masikini huku wakiwakaripia nakuwasem Soma Zaidi...

Wanaoongozwa na wasioongozwa na quran
Soma Zaidi...

Adabu za kusikiliza quran
ADABU ZA KUSIKILIZA QURANI 1. Soma Zaidi...

Kulaaniwa Bani Israil
Pamoja na kuteuliwa na Allah(s. Soma Zaidi...

Nini maana ya Quran
Post hii inakwenda kukuambia maana ya Quran Soma Zaidi...

Quran haikutoka kwa Mtu zezeta wala mwenye upungufu wa akili
Soma Zaidi...

idadi sahihi kati ya sura zilizoshuka Makka na zile za madina
A. Soma Zaidi...

Sababu za Kushuka Surat Al-Masad (tabat yadaa) na fadhila zake
4. Soma Zaidi...

Sababu za kushuka kwa Surat Al-Asr
Surat Al-Asri imeteremshwa Makka, na hapa utazujuwa sababu za kushuka kwa sura hii Soma Zaidi...

fadhila za sura kwenye quran
FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya. Soma Zaidi...

Tafsiri na mafunzo ya sura zilizochaguliwa - Saratul-fiyl
Quran (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Hukumu za waqfu na Ibtida
waqfu ni misimamo ambapo msomaji wa Quran anaruhusiwa kusimama, kuhema au kumeza mate. Na ibtidai ni kuanza baada ya kutoka kwenye waqf Soma Zaidi...