Huu ni muendelezowa mafunzo ya database kwa kutumia MySQl na hili ni somo la 12. katika somo hili tutajifunza namna ya kufanya mahesabu kwa kutumia SQl katika database
Katika somo ka 10 na 11 tumejifunza namna ya kupangilia data zetu. Sasa hapa tutakwenda kujifunza mambo makuu 3 mabayo nu kuhesabu idadi ya row, kuhesamu jumla ya item na kuhesabu wastani. Hili ndio somo la mwisho ambalo linakwenda kutufungia mafunzo yetu ya database level 1.
1. Kuhesabu idadi ya row.
Lamda hujaelewa row ni nini? Unapoweka data kwenye database kila moja inakaa kwenye row, mmmh, lamda bado lugha ni ngumu, yaani hapa ninachomaanishwa ni data ngapi umeweka. Mfano kwenye table yetu tunatocheza nayo kuna idadi ya menu 10 yaani kuna row 10. sasa fikiria database ni kubwa sana na unataka kujuwa ina row ngapi njia rahisi sio kuhesabu ni kutumia SQL.
Kanuni yetu ni ni kutumia COUNT() function (rejea kuhusu function kwenye mafunzo ya php). utaanza kuselect kisha count ndani ya mabano ya function utaweka jina la column mfano name kisha from ikifuatiwa na jina la table. Unaweza pia kuweka na condition kwa kutumia where . mfano
SELECT COUNT(price) FROM menu
Kwa mfano huu itakuletea 10 kwani idadi ya row hapo ni 10. lakini kama ninataka kuhesabu idadi ta row ambazo price ni zaidi ya 1000 hapo itatubidu tutumie condition. Hivyo itakuwa hivi:-
SELECT COUNT(price) FROM menu WHERE price >1000
Hapo itakuletea 7 yaani jumala ya row zote ambazo price yake ni zaidi ya 1000 ni 7 yaani menu ambazo gharama yake ni zaidi ya 1000 zipo 7.
2. Kutafuta average au wastani
Kufanya hivi tutatumia AVG() function. Mpangilio wake ni sawa na huo uliotangulia hapo juu. Kwa mfano tunataka kujuwa menu zote hapo wastani wake ni kiasi gani. Kumbuka kuna toauti ya wastani na jumla, Wastani ji jumla gawanya kwa idani. (rejea kanuni za hesabu darasa la tano). hivyo itakuwa hivi:-
SELECT AVG(price) FROM menu
Hapo itakupa jibu 4920 yaani wastani wa gharama kwa kila menu ni 4920. kama unataka kuhakiki tumia kanuni huu ya darasa la tano (wastani = jumla/idadi). unaweza pia kutumia WHERE condition kama tulivyoona hapo juu.
3. Kutafuta jumla
Sasa tunataka kujuwa jumala ya menu zote zinagharimu kiasi gani. Ili kufanya hivi tutatumia SUM () function. Hii itatuletea jumala ya item kwenye column. Kama ulivyoona hapo kwenye menu yetu kila kitu na gharama zake saja jumla yake itakuwaje. Mpangilio wa fomula hii ni sawa na hizi mifano miwili iliyotangulia hapo juu. Hivyo itakuwa hivi
SELECT SUM(price) FROM menu
Hiyo itakupa jibu la 49200 yaani kama utajumlisha gharama zote hapo utapata 49200. sasa kama unataka kuthibitisha kanuni hizi kwa hesabu ya darasa la 5 unaweza.
Unaweza pia kutumia condition. Kwa mfano tunataka kujuwa jumla ya menu zote ambazo price ni chini ya 3000. hii itakuwa SELECT SUM(price) FROM menu WHERE price <3000 ambapo tutapata jibu la 6700.
4. Maximum na minimun
Tunataka kujuwa menu yenye gharama ndogo kuliko zote amba kubwa kuliko zote. Kufanya hivi tutatumia MAX() na MIN(). mifano mimngine ni kama ilivyotangulia. Hivyo kama ukipanga vyema itakuwa hivi:-
A. SELECT MAX(PRICE) FROM menu
Hapa itakupa jibu 25000 kwani ndio price kubwa kuliko zote.
B. SELECT MIN(PRICE) FROM menu
Hapo itakupa jibu 300 kwani ndio price ndogo kuliko zote
Na huu ndio mwisho wa mafunzo haya ya database level 1. tukutane level 2 tutakapojifunza mabo mengi zaidi katika database. Usikose mapunzo yetu mengine ya php level 2 na html level 3.
Mafunzo haya yamekujia kwa Ihsani ya bongoclass
Web: www.bongoclass.com
Email: mafunzo@bongoclass.com
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
huu ni muendelezo wa mafunzo ya Database klwa kutumia MySQL na hili ni somo la 11. katika somo hili tutaendelea kujifunza mpangilio wa muonekano wa data kwenye database.
Soma Zaidi...Huuu ni muendeleo wa mafunzo ya database kwa lugha ya kiswahili, na hili ni somo la nane. Katika somo hli utajifunza namna ya kuweka taarifa kwenye database, kuzfuta na kuziediti yaani kuzifanyia marekebisho.
Soma Zaidi...Karibu tena katika mafunzo haya ya html level 2 na hili ni somo la 5. Katika somo hili utajifunza zaidi kuhusu kuweka style kwenye html file.
Soma Zaidi...hili ni somo la pili katika mfululizo wa mafunzo haya ya php level 1 na hapa utajifunza namna ya kuandika faili klako la kwanza la php.
Soma Zaidi...Hii ni tafiti ambayo itakushangaza, kwa namna ambavyo matumizi ya AI yalivyo na athari kwenye uwezo wa kufikiri
Soma Zaidi...Huu ni muendelezo wa mafunzo ya database kwa kutumia MySQL na hili ni somo la 6. Katika somo hili tutakwenda kuona jinsi ya kutengeneza table kwa kutumia MySQL na kwa kutuma SQL.
Soma Zaidi...somo hili la 4 katika mafunzo ya PHP level 1 utajifunza aina za data mabazo php inakwenda kuzitumia.
Soma Zaidi...Haya ni mafunzo ya php na hili ni somo la tano. Katika somovhili utajifunza namna ya kutengeneza functions.
Soma Zaidi...Hii ni project ya HTML ambayo imetengenezwa kulingana na mafunzo ya HTML level1. Tunatarajia project hii kuboreshwa kadiri mafunzo yanavyozidi kusonga mbele.
Soma Zaidi...Haya ni mafunzo ya muda mfupi katika kujifunza hasa ujuzi wa kutengeneza Android App hata kama haujui kitu kuhusiana na Android Development
Soma Zaidi...