image

nmna ya kufanya Talbiy kwa mwenye kuhiji

2.

nmna ya kufanya Talbiy kwa mwenye kuhiji

2. TalbiyaTalbiya ni maneno ya kuitikia wito wa Allah (s.w) pale alipomuamrisha Nabii Ibrahim (a.s) kuwaita watu kwa Hija:


“Na (tukamw am bia Ibrahim): Utangaze kw a w atu habari za Hija, w atakujia


(wengine) kwa miguu na (wengine) juu ya kila mnyama aliyokonda (kwa uchovu wa safari ndefu). Ili washuhudie manufaa yao na kulitaja jina la Mwenyezi Mungu katika siku zinazojulikana ...” (22:2 7-2 8).Maneno ya kuitikia wito huu wa Allah, yaani maneno ya Talbiya, kama yalivyo katika hadith iliyosimuliwa na Abdullah bin Umar (r.a) ni haya yafuatayo:


“Labbayka Allaahumma labbayka. Labbayka laashariika laka
labbayka. Innal-hamda wanni-i-mata laka wal-mulku; laashariika laka”.Tafsiri:
“Naitika wito wako Ee Allah, Naitika. Naitika, Ewe Usiye na mshirika, Naitika. Hakika sifa zote njema na neema zote ni zako na Ufalme ni Wako, Ewe Usiye na mshirika (Bukhari na Muslim).Wanaume wataitika kwa sauti ya juu na wanawake wataitika kwa sauti ndogo. Kwa wale walionuia kwa Hija tu au Hija na ‘Umra, Talbiya huanza mara baada ya kuvaa Ihram na kunuia, mpaka watakapotupa jiwe la kwanza katika mnara mkubwa -”Jamaratul’ Aqaba” siku ya mwezi 10 Dhul-Hija.Talbiya ya ‘Umra huanzia kwenye Miiqaat baada ya kuvaa Ihram na kutia nia ya ‘Umra mpaka kwenye Nyumba Takatifu ya Ka’aba. Kwa wale walionuia Hija ya “Tamattu”, wataanza Talbiya tena baada ya kuvalia Ihram kwa nia ya Hija siku ya mwezi 8 Dhul-Hija, na wataendelea mpaka wakati watakapoanza kutupa jiwe la kwanza kulenga mnara mkubwa siku ya mwezi 10 Dhul-Hija.Wakati wa kwenda Makka Talbiya itarudiwa tena na tena. Isomwe kila baada ya swala ya faradh, kila Haji au Hajjat anapopanda na kuteremka katika kipando au chombo anachosafiria, kila akipanda na akiteremka mlima na kila anapokutana na msafara mwingine.Mtume (s.a.w) alifanya hivyo pamoja na maswahaba wake alioongozana nao katika Hija ya kuaga. Kila alipotaka Waislamu wasome talbiya aliwaamrisha kwa kusema “Takbiir”.Kisha Masahaba wake na yeye mwenyewe walianza kusoma Talbiya kwa nguvu.
                   
           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 137


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-