12.
12. Swala ya Kuomba Mvua - (Swalatul Istisqaa)โ
Istisqaa ina maana ya kuomba maji. Uislamu unatuhimiza kumuelekea Allah kwa msaada wakati wa matatizo na dhiki. Kwa hiyo panapokuwa na ukame Waislamu wanahimizwa kumuomba Allah(s.w)kwa unyenyekevu katika jamaa. Maombi haya yanajulikana kama โSwalatul Istisqaaโ. Kutokana na Hadithi mbali mbali maombi haya yanaweza kuombwa katika namna tatu zifuatazo:
(a)Kuomba Dua bila ya swala.
(b)Kuomba dua katika khutuba ya Ijumaa au mwisho wa swala za faradhi.
(c)Namna ya tatu ambayo ni muhimu sana ni ile ya kuswali rakaa mbili zinazofuatiwa na khutuba na kumalizia na Dua.
Maombi haya hapana budi yaombwe kwa unyenyekevu mkubwa ukiambatana na imani kamili juu ya uwezo waAllah usio mipaka.
Swalatul Istisqaa Inavyoswaliwa
Swala hii ni sunnah iliyokokotezwa wakati wa ukame na huswaliwa katika jamaa uwanjani kama inavyo swaliwa swala ya Idd. Kama swala ya Idd katika rakaa ya kwanza kuna takbira saba baada ya Takbira ya kuhirimia na kuna Takbira tano kabla ya kuanza Suratul Fatiha katika rakaa ya pili. Ni sunnah katika rakaa ya kwanza, baada ya Al-fatiha kusoma Surat-Qaf au Al-Aโlaa na katika rakaa ya pili kusoma baada ya Alfatiha. suratul-Qamar au Al-Ghashiyah. Imamu ni sharti awe kiongozi wa ngazi ya juu au naibu wake anayeshughulikia mambo ya Waislamu.
Swala hii hufuatiwa na khutuba mbili kama ilivyo katika khutuba za Idd. Ni sunnah Imamu kuleta istighf'aari mara tisa kabla hajaanza khutuba ya kwanza na ya pill.
Istighfaari hii ni kusema
"Astaghafirullahil-aladhim alladhii laa ilaaha illa huwal-hayyul-qayyuum-almudabbiru kullu-shayin wa-atubu ilaihi"
Ni sunnah wakati wa kuomba dua kugeuza mikono au kuelekeza mbinguni migongo ya viganja vya mikono . Tunafahamishwa hill katika Hadith za Mtume (s.a.w) zifuatazo kuwa:
Abduilah blrs 7.aid Al-Arrsarl (r.a) amesimuiia kuwa Mtume (s.aw) aWaaenda rye ya rryi Qi Iwswali swaIatu1-IsiisgaaAUpotaka. kuorrtba dua, alielekea Qibia nra alaageura. kiiemba choke. (Muslim).
Arras bin MaWc (r.a) amestmuIia kuu~a Mturne (s.a w) katika kuomba dua ya mvua alielekaezaJuu mtgongo yaviganfa uyake vya miknno. (Muslim).
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya.
Soma Zaidi...Tafsiri ya Quran kwa iswahili iliyotafsiriwa na Sheikh Ali Muhsin Al-BArwani
Soma Zaidi...