image

Je mahari inashusha hadhi ya mwanamke?

Je, Mahari inashusha hadhi ya mwanamke?

Je mahari inashusha hadhi ya mwanamke?

Je, Mahari inashusha hadhi ya mwanamke?



Kama tulivyojifunza katika Qur-an (4:4), mahari ni hidaya kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w). Kwa maana nyingine, mahari ni mali anayoitoa mwanamume kumpa mwanamke anayetaka kumuoa kwa ajili ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu (s.w) aliyemuamrisha kutoa mali hiyo iii kumhalalishia mwanamke anayemtaka awe mkewe wa ndoa. Na mwanamke anapokea mahari hayo ikiwa ni zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w). Kwa mtazamo huu wa Uislamu mwanamume anapotoa mahari hatakuwa na hata chembe ya hisia kuwa ni bei ya mwanamke anayemuoa. Hali kadhalika, kwa mtazamo huu, mwanamke atakapopokea mahari yake hatakuwa na hata chembe ya hisia kuwa amejiuza kwa mume anayemuoa.



llivyo, ni kwamba katika jamii nyingi zisizo za Kiislamu, mahari imefanywa kama bei ya kumnunulia mke inayotozwa na wazazi au walezi wa mwanamke anayeolewa. Ni katika mtizamo huu wa biashara unaowafanya wale wajiitao watetezi wa Haki na Hadhi ya Mwanamke, waishutumu mahari kuwa imetoa mchango mkubwa katika kumnyanyasa mwanamke katika jamii. Ni kweli kabisa kuwa mwanamke, kwa kisingizio cha mahari, amekandamizwa na kunyanyaswa kiasi kikubwa na wanaume katika jamii nyingi za Kikafiri.


Lakini, ni kweli kuwa mahari waliyotoa wanaume katika jamii hizi ndio hasa sababu ya kuwashusha wanawake hadhi zao na kuwakandamiza? Je, mahari yakiondolewa kama watetezi wa haki za wanawake wanavyodai, wanawake watapata haki zao na hadhi yao ikarudi mahali pake? Ukweli ni kwamba tatizo haliko kwenye mahari bali tatizo liko kwenye kukiuka maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu (s.w) katika utoaji wa hayo mahari na katika kuendesha maisha ya kila siku kwa ujumla.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 295


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-