1.
1.Ihram na Nia ya Hija au ‘Umra
Matendo ya Hija au ‘Umra huanza rasmi kwa kuvalia vazi la Ihram. Kama tulivyoona Ihram huvaliwa nyumbani au katika vituo maalum -
Mawaaqiit - vilivyowekwa na Mtume (s.a.w) kabla ya kuingia kwenye uwanja Mtakatifu wa Makka. Wakazi wa Makka huvalia Ihram nyumbani kwa o.
Utaratibu unaofuatwa ni kwamba Hajj, kabla ya kuvaa Ihram, ni sunna kunyoa nywele za makwapani na sehemu nyingine za mwili, kupunguza nywele za kichwani, kunyoa ndevu na kukata kucha. Kisha ni sunnah kukoga, kutawadha na kupaka manukato ndipo uvalie Ihram. Ni vyema kuvaa Ihram wakati wa swala mojawapo ya faradhi. Mtume (s.a.w) katika Hija ya kuaga alivaa Ihram wakati wa swala ya Adhuhuri.
Kabla ya kutia nia ya aina ya Hija au ‘Umra, Haji ataswali rakaa mbili za sunnah, kisha mara tu baada ya kutoa salaam atanuia aina ya Hija anayokusudia kuifanya, na ataitikia wito wa Allah (s.w) kulingana na nia yake.Kama nia yake ni ya kufanya ’Umra (At-Tamattu) ataitika:
Ee Allah nakutikia kwa ‘Umra.
Allahumma labbaikal ’Umrata
Kama nia yake ni ya kufanya Hija na ‘Umra (Al-Qiran) ataitika:
Ee Mola. Naitika kwa Hija na ‘Umra. Allahumma labbaikal hajji wa Umrata
Kama nia yake ni ya kufanya Hija tu (Al-Ifraad) ataitikia: Ee Mola, Naitika kwa Hija Allahumma labbaikal hajji
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
MGAWANYIKO KATIKA QURAN Juzuu, Sura, Aya, Manzil, Qara Wataalamu wa elimu za Qurani katika fani za uandishi na usomaji wameigawanya Qurani katika mafungu ili kuwezesha urahisi kwa wasomaji wa qurani.
Soma Zaidi...Muislamu anapoingia Msikitini kabla hajakaa anatakiwa aswali rakaa mbili za maamkizi ya msikiti, Tahiyyatul-Masjid.
Soma Zaidi...