Presha ya kupanda (hypertension) dalili zake, na njia za kukabiliana nayo

Presha ya kupanda (hypertension) dalili zake, na njia za kukabiliana nayo

MARADHI YA PRESHA YA KUPANDA (HYPERTENSION)

Presha ya kupanda hutokea pale kipimo kinaposoma zaidi ya 120/80mm Hg. Mara nyingi huwezi kujitambua kama unapresha hii ya kupanda mpaka pale inapotokea. Na ndio maana huitwa silent killer yaani muuwajiwa siri. Presha ya kupanda isipo tibiwa ama mgonjwa asipofata maelekezo vyema inaweza kusababisha shambulio lamoyo na kupalalaizi.Presha ya kupanda isipotibiwa ama mgonjwa kufuata maelekezo vyema inaweza kusababisha athari kwenye moyo, kibofu na ubongo. Watu wengi wanakufa duniani kwa sababu ya presha ya kupanad. Wataalamu wa afya wametuwekea staili ambazo zinaendana na ugonjwa huu. Kama mgonjwa atafata maelekezo haya itamsaidia kuishi bila ya kupata presha ama tena kama ana presha itaweza kupunguza athari na isiwe inatoka mara kwa mara.NJIA ZA KUKABILIANA NA PRESHA YA KUPANDA (HYPERTENSION)


1.Fanya mazoezi ya mwili na viungo walau kila siku kwa dakika kama 30 mpaka 60. si lazima uwe unakimbia ama mazoezi magumu ya kutoa jasho, hapana unaweza hata kuamua kutembea kwa miguu kwa mwendo mrefu kwa lisaa limoja na ikawa ni mazoezi tosha.


2.Kula vyakula vilivyo bora kwa afya, ambavyo vinasaidia kupunguza ama kuzuia presha. Kitaalamu mlo huu huitwa DASH yaani Diet Aproaches to Stop Hypertension. Vyakula hivi ni kama:
A.Matunda
B.Mboga za majani
C.Nafaka nzima
D.Samaki, karanga na korosho
E.Wacha kula vyakula vyenye mafuta mengi


3.Punguza ulaji wa chumvi sana. Kuzidi kwa ulaji wa vyakula vyenye chumvi nyingi kunaweza kusababisha presha ya kupanda. Kitaalamu ni kuwa ukila chumvi sana mwili unahitaji kupata maji mengi na hali hii itapelekea presha.
4.Punguza uzito uliozidi mwilini. Rafiki mkubwa wa presha ni kuzidi kwa uzito. Na tambuwa kuwa uzito wa mwili unatakiwa uendane na urefu wa mtu na si umri ama unene alio nao. hivyo tambua. Ili kuhakikisha kama uzito wako upo sawa unaeza kujipimia kiuno chako. Kikawaida wanaume wnatakiwa viuno vyao visizidi nchi 40 na wanawake viuno vyao visizidi nchi 35.


5.Punguza matumizi ya sigara ama wacha kabisa. Ndani ya sigara kuna kemikali za nicotine na nyinginezo. Nicotine ni rafiki sana na presha ya kupanda.
6.Punguza unywaji wa pombe ama wacha kabisa. Unywaji wa pombe sio hatari tu wa afya ya moyo lakini pia unaweza kuleta shida nyingine za kiafya kama saratani. Hakikisha kama ni mnywaji unapunguza unywaji ama unawacha kabisa itakuwa ni bora kwako.
7.Hakikisha huna misongo ya mawazo. Misongo ya mawazo inaweza kuwa ni adui mkubwa wa afya ya ubongo. Ni vyema kusamehe wanaokukosea na kuomba msamaha unapo kosea hali zote hizi mbili zitakusaidia kupunguza misongo ya mawazo. Jichanganye na watu na pemba kuwa mbali na fujo.VYAKULA AMBAVYO HUSAIDIA KUPUNGUZA PRESHA YA KUPANDA AMA HULINDA MWILI DHIDI YA PRESHA YA KUPANDA.
Presha ya kupanda inaweza kupelekea athari kubwa na mbaya sana kwenye afya ya mtu. Presha ya kupanda isipotibiwa ama mtu asipofuata masharti ya kuishi na ugonjwa huu madhara makubwa yanaweza kutokea. Kifo, kupasuka kwa mishipa ya damu, kupalalaizi, kuharibika kwa figo na moyo kushindwa kufanya kazi na kupata shambulio la moyo yote haya yanaweza kuwa ni matokeo ya presha ya kupanda pindi isipotibiwa ama mtu asipofata masharti.:-Unaweza kupamana na presha kwa kufuata mashari kama kufanya mazoezi, kula vyakula salama kwa presha, kupunguza misongo ya mawazo, kupunguza kula chumvi, kupunguza uzito, kupunguza ama kuacha sigara na pombe. Miongoni mwa vyakula salama kwa presha ni kama


1.Mboga za majani ambazo zina madini ya potassium kwa wingi. Madini haya ni mujarabu sana katika kulinda na kuimarisha afya ya moyo. Ulaji wa mboga hizi unaweza kuwa ni njia ya kujilinda na presha ya kupanda. Miongoni mwa mboga hizi ni kama spinachi


2.Maziwa: maziwa ni katika vyakula vyenye madini ya calcium kwa wingi na pia yana mafuta kwa uchache. Hali zote mbili hizi ni muhimu kwa afya ya moyo.


3.Ndizi; ndizi ni katika matunda yenye madini ya potassium kwa wingi. Ulaji wa ndizi unaweza kuwa ni msaada mzuri kwa kulinda mwili dhidi ya presha ya kupamda.


4.Mayai


5.Samaki aina ya salmon na wanaofanana nao.


6.Ulaji wa mbegu za mimea kama maboga na alizeti


7.Kitunduu thaumu: unaweza kutumia vitunguu thaumu kwa kula ama kutafuna, ni vyema kufunga mdomo wakati unapotafuna.


8.Makomamanga; unaweza kula atunda hili kama juisi ama kula kawaida.13.HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPANDWA NA PRESHA


1.Muweke mgonjwa kwenye sehemu tulivu na iliyopowa
2.Mpunguzie nguo na abakiwe na ngue nyepesi na chache
3.Unaweza kumpepea ana muweke kwenye feni
4.Mpe vitunguu thaumu atafune, na afunge mdomo wakati anatafuna
5.Kama hali itaendelea mpeleke kituo cha afya kilicho karibu.                   Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2353


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-