Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa macho, ni ugonjwa ambao ushambulia zaidi sehemu za nje za macho ambazo kwa kawaida uitwa conjunctiva na cornea hizi sehemu zikipata maambukizi zisipotibiwa mapema uweza kusababisha upofu kwa mgonjwa.
1. Kwanza kabisa tunapaswa kujua ni mdudu yupi anayesababisha ugonjwa huu, kwa jina la kitaalamu huitwa Chlamydia trachomatis ndiye anayesababisha ugonjwa huu, kwa hiyo Kuna baadhi ya viashiria ambavyo usababisha kuenea kwa ugonjwa huu na vyo ni .
2. Mazingira yaliyo makavu na yenye vumbi .
Kwa kawaida mazingira haya ndipo wadudu upenda kukaa na kuzaliana kwa hiyo ni vizuri sana iwapo ugonjwa huu ukitokea watu wanaoishi kwenye mazingira haya kuwa na tahadhari Ili kuweza kuepukana na ugonjwa huu ambao ni hatari kwa macho.
3. Sehemu yenye uchafu na inzi.
Kwa kawaida tunajua kuwa inzi ndo usababisha kuenea kwa ugonjwa huu kutoka kwa mgonjwa mmoja kwenda kwa mwingine kwa sababu ikitokea nzi akagusa jicho lililo na maambukizi na akabeba wadudu hao na kutua kwenye jicho la mtu mzima hao wadudu uanza kushambulia jicho na hatimaye maambukizi uenea sana na kusababisha madhara makubwa kama matibabu hayajafanyika.
4. Sehemu zenye mkusanyiko mkubwa wa watu.
Kwa kawaida kwenye mikusanyiko huwa Kuna matatizo na milipuka mingi ya magonjwa kwa hiyo na ugonjwa huu uonekana zaidi kwenye mikusanyiko ya watu kama vile kwa wakimbizi na wafungwa, hii ni kwa sababu ya kutokuwepo kwa uangalizi wa kutosha na usafi ni kidogo kwa hiyo ugonjwa huu ukitokea mazingira hayo ni vigumu kupona haraka.
5. Sehemu zenye uhaba wa maji.
Kweli ugonjwa huu ujitokeza kwenye sehemu zenye uhaba wa maji kwa sababu Kuna sehemu zina ukosefu wa maji ambapo watu utumia masaa kama matano kutafuta maji na ni vigumu kwenye mazingira hayo kukosekana ugonjwa huu kwa sababu uchafu utakuwepo watu watashindwa kupata maji ya kutosha ya kunawa na kufua nguo zao.
6. Kwa hiyo tunapaswa kuelewa kuwa ugonjwa huu upo kwenye jamii na una dawa ila uzembe ukifanyika Kuna hatari ya kupata upofu kwa hiyo ni vizuri kabisa kuwatibu wagonjwa wetu na kuzingatia usafi Ili kuepuka maambukizi
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
je na wewe ni mmoja katika wenye maumivu ya tumbo upande mmoja?. Basi post hii ni kwa ajili yako.
Soma Zaidi...Katika post hii utajifunz akuhusu vidonda vya tumbo na jinsi vinavyotokea. Utajifunza pia tahadhari anazopasa mtu achukuwe na vyakula salama anavyopaswa kula.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu fangasi wa sehemu za Siri
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea baadhi ya watu walio hatarini kupata fangasi
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maradhi ya macho,dalili na matibabu yake
Soma Zaidi...Kama una tatizo la midomo kuchubuka na kuwa myeupe ama kuwa na vidonda. Post hii inakwenda kuangalia swala hili.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi visababishi vya maambukizi kwenye milija na, ni mambo yanayosababisha maambukizi kwenye milija na ovari.
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na Ugonjwa wa upungufu wa Adrenali ni ugonjwa ambao hutokea wakati mwili wako hutoa kiasi cha kutosha cha homoni fulani zinazozalishwa na tezi zako za adrenali. ugonjwa huu hutokea katika makundi yote ya umri na huathiri
Soma Zaidi...Posti hii inaonyesha namna ya kujizuia,Mambo ya Hatari,na na Mambo yanayopelekea Ugonjwa wa ukosefu wa mkojo
Soma Zaidi...