Wajibu wa mjamzito katika utaratibu wa uleaji wa mimba
Posti hii inahusu zaidi wajibu wa Mama mjamzito katika kileo mimba sio yeye tu Bali na wote waliomzunguka wanapaswa kuhakikisha kuwa mama mjamzito anapaswa kufanyiwa huduma zote Ili kuweza kujifungua salama na bila shida yoyote.
Wajibu wa Mama mjamzito.
1. Mama mjamzito anapaswa kuwa na mda wa kutosha wa kupumzika.
Kwa sababu mama anakuwa na matalajio ya kujifungua salama anapaswa kupumzika kwa mda mrefu na hasa hasa anapaswa kuinua miguu juu anapokuwa amelala na anapaswa kulala chini wakati wa alfajiri hayo yote yana mpatia mazoezi ya kufaa na kutosha anapokaribia kujifungua na hivyo kumwezesha mtoto kukua vizuri na Baadae kujifungua bila shida, kwa hiyo jamii na ndugu wa familia wanapaswa kuhakikisha kuwa Mama anapata mda wa kutosha wa kupumzika.
2. Mama anapaswa kipata chakula Bora chenye virutubisho.
Kwa kumpatia Mama chakula chenye virutubisho umfanye Mama kuwa na madini yabayohitajika mwilini kama vile madini ya chuma ambayo usaidia wakati wa ujauzito, vyakula vyenye vitamini A ambavyo umsaidie mtoto aweze kuona, kwa hiyo Mama anapaswa kupatiwa Aina zote za vyakula kama vile wanga, protein, mafuta na mboga mboga za majani ambazo uongeza damu mwilni na wakati wa kujifungua anakuwa na damu ya kutosha. Kwa hiyo jamii ziachane na Mila potofu kuhusu vyakula kwa wanawake.
3. Kuepuka Aina yoyote ya kemikali .
Mama mjamzito anapaswa kuepuka Aina yoyote ya kemikali kama vile pombe ambayo ikiingia ndani uweza kuaribu ubongo wa mtoto katika makuzi anapokuwa tumboni mwa mama,Moshi wa sigara nao ni hatari kwa Mama mjamzito kwa sababu unaweza kuharibu mapafu ya mtoto akiwa tumboni kwa mama, Madawa ya kulevya pia nayo ni hatari kwa afya ya Mama na Mtoto, kwa hiyo mtoto akiwa tumboni kwa mama anaweza kuzaliwa akiwa zezeta kwa Sababu ya madawa ya kulevya.
4. Kuwepo kwa mhudumu karibu na Mama mjamzito.
Mama mjamzito anapaswa kuwa na mhudumu wa karibu kwa mfano wataalamu wafya au mkunga Ili kuhakikisha kujua siku na mda wa kujifungua kwa Mama kwa kufanya hivyo tunaweza kuepusha madhara mbalimbali ambayo uweza kuwakuta wanawake wakati wa kujifungua kwa hiyo Mama mjamzito anapaswa kwenda klinic mara kwa mara Ili kuangalia afya yaka na maendeleo ya mtoto kwa ujumla .
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉2 Dua za Mitume na Manabii 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 Madrasa kiganjani 👉5 ai web app 👉6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
SIKU HATARI ZA KUPATA UJAUZITO KWA MWENYE MZUNGURUKO WA SIKU KIDONGO AU NYUNGI
SIKU YA KUPATA UJAUZITO Kawaida wanawake walio wengi mzunguruko wa siku zao ni siku 28 lakini wapo ambao ni zaidi ya hapo na wapo ambao ni chini ya hapo.
Soma Zaidi...Umuhimu wa kunyonyesha mtoto
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kunyonyesha mtoto, kunyonyesha ni kitendo cha Mama kutumia titi lake Ili kuweza kumpatia mtoto lishe kwa kipindi chote ambacho Mama upaswa kutumia kwa kunyonyesha mtoto wake kwa hiyo Kuna faida ambazo mama uzipata kutoka
Soma Zaidi...Sababu za kutokea uvimbe kwenye kizazi.
Posti hii inahusu zaidi sababu za kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi,kwa kawaida tumesikia akina mama wengi wanalalamika kuhusu kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi na wengine hawajui sababu zake kwa hiyo sababu zifuatazo ni za kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi.
Soma Zaidi...Madhara ya kutumia vidonge kwa akina dada vya uzazi wa mpango
Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kwa sababu ya kutumia vidonge vya uzazi wa mpango kwa akina dada.
Soma Zaidi...Njia za kuzuia mimba zisiharibike.
Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kuzuia mimba zisiharibike, kwa sababu kila mama anayebeba mimba anategemea kupata mtoto kwa hiyo na sisi hamu yetu ni kuhakikisha kwamba mtoto anazaliwa kwa kuzuia mimba kuharibik
Soma Zaidi...