Nadharia ya uchumi kiislamu

Nadharia ya uchumi kiislamu

1.

Nadharia ya uchumi kiislamu

1.Nadharia ya uchumi wa Kiislamu
Mfumo wa uchumi katika Uislamu ni utaratibu utokanao na Qur-an na Sunnah juu ya uzalishaji, umilikaji, usambazaji, na utumiaji wa mali na huduma pamoja na miiko yake. Kwa msingi huo, uchumi huo umejengwa juu ya fikra ya ukati na kati (Iqtisaad), hivyo umetofautiana na mifumo mingine iliyobuniwa na watu.


Dhana (concept) ya ukati (Iqtisaad) katika shughuli za kiuchumi ni kule kutoa uhuru kwa mtu binafsi (sekta binafsi) kuchuma na kumiliki mali ili iwe motisha kwake ya kuchapa kazi wakati huo huo serikali ikisimamia na kutoa miongozo katika uzalishaji na ugawaji, na vile vile kuwa na sekta zake (sekta za umma) ili kila mwana jamii apate haki za kimsingi. Mifumo iliyobuniwa na watu imeathiriwa na udhaifu wa kibinaadamu wa kuelemea upande huu au ule.



Ipo mifumo ya kiuchumi kama vile ubepari ambao umeelemea mno katika ubinafsi kiasi ambacho umepuuza kabisa haki za kijamii. Katika mfumo huu (ubepari) umma hauna chake; mali, huduma na shughuli mbali mbali hubinafsishwa. Wachache chini ya mfumo huu ndio hunufaika na rasilimali za Taifa. Hujilimbikizia mali, na motisha yao ya uzalishaji ni ile faida waipatayo. Serikali kuu ya mfumo huu wa kibepari hushirikiana na wachache hao waliohodhi mali, kuwanyonya walio wengi.



Pia, kuna mfumo wa uchumi wa Kikomunist au Kijamaa ambao nadharia yake imeelemea mno katika “usawa” wa sare kiasi cha kudhoofisha mno motisha ya watu binafsi na hivyo kupelekea kukosekana kwa ufanisi katika uzalishaji. Katika mfumo huu mali na shughuli mbali mbali hutaifishwa (toka milki ya watu binafsi kuwa milki ya taifa).


Ukweli ni kwamba huwa si mali ya taifa kama inavyotangazwa bali mbiu ya “usawa”, na “mali ya umma”, chini ya mfumo huu, ni mwavuli tu uliokinga kikundi cha watu kilichojipa mamlaka ya uendeshaji wa nchi kwa sura ya chama au serikali kwa maslahi ya kikundi hicho. Kikundi hicho ndicho humiliki na kutafuna mali huku wananchi wengi wakiendelea kudhulumiwa kwa sababu mbali mbali. Hivyo hakuna usawa ulio chini ya mfumo huu bali ni ubinafsi ule ule ambao huhamishwa toka kwa mtu binafsi kwenda kwenye kikundi fulani.




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views: 1805

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 web hosting     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Dua za Mitume na Manabii     👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    

Post zinazofanana:

Ni ipi hukumu ya muislamu anayekula mwezi wa Ramadhani bila ya sababu ya kisheria

Endapo muislamu hatafunga mwezi wa Ramadhani bila ya ruhusa je atatakiwa afanye nini. Je ataweza kuilipa funga hiyo?

Soma Zaidi...
haki ya kutaliki: kuacha na kuachwa katika ndoa ya kiislamu

Haki ya KutalikiKatika jamii nyingi za kjahili haki ya kutoa talaka iko kwa mwanamume tu na mwanamke hana haki yoyote ya kumtaliki mumee.

Soma Zaidi...
Hifadhi ya Mwanamke na Maadili ya Jamii

(c) Hifadhi ya Mwanamke na Maadili ya JamiiKimaumbile wanaadam kama walivyo wanyama, wamejaaliwa kuwa na mvuto wa kimapenzi kati ya mume na mke ili kuwawezesha kutekeleza wajibu mkubwa wa kuzaana na kuendeleza kizazi.

Soma Zaidi...
Ni zipi najisi katika uislamu

Post hii inakwenda kukupa orodha ya vitu vilivyo najisi.

Soma Zaidi...