Posti hii inahusu zaidi Njia za kufanya Ili kupunguza maumivu ya tatizo la uti wa mgongo, ni njia unazopaswa kufanya pale unapokuwa na tatizo la uti wa Mgongo.
Njia za kufanya ukiwa na tatizo la uti wa mgongo.
1.Tumia vitu vya moto.
Kama Kuna tatizo la uti wa mgongo,lazima kutumia vitu vya moto zaidi kuliko vya baridi Ili kupunguza hali ya kusinyaa kwa misuli na kufanya misuli kutanuka na maumivu huwa kidogo sana.mfano kuweka maji ya moto kwenye taulo na kujikanda na taulo la moto kwenye sehemu ya maumivu.
2. Tumia barafu kama mtu amepata ajali Ili kupunguza moto ambao upo kwenye pingili, pengine kama ni kuvunjika pingili zinakuwa za moto sana na kusababisha maumivu Ili kupunguza maumivu makali kwenye uti wa mgongo, barafu inabidi itolewe Ili kupunguza joto ambalo upelekea maumivu na kitendo hiki kisizidi dakika Kumi.
3. Mazoezi mepesi yatumike.
Mtu mwenye matatizo ya uti wa mgongo mazoezi mepesi yatumike Ili kufanya mwili kutanuka na kuruhusu kuruhusu damu ipite na pengine sehemu iliyokuwa umepata shida inaweza kurudi kwa kutumia mazoezi na mazoezi yasiwe makali sana kwa sababu yanaweza kusababisha kuvunjika zaidi, kwa hiyo mazoezi ni ya lazima.
4.Acha kubeba vitu vizito.
Kwa mtu mwenye matatizo ya uti wa mgongo anapaswa kuepuka kubeba vitu vizito kwa sababu katika kubeba vitu vizito Kuna hatari unaweza kusababisha maumivu zaidi na kumpelekea ulemavu wa kudumu, kwa hiyo watu wenye matatizo ya uti wa mgongo wanapaswa kuacha kubeba vitu vizito.
5.Tumia godoro gumu wakati wa kulala.
Wakati wa kulala wenye matatizo ya uti wa mgongo wanapaswa kulalia magodoro magumu Ili kufanya pingili zikae kwenye sehemu yake kwa sababu katika kutumia godoro matatizo ya mgongo yanaweza kupungua na kuwa kwenye hali ya kawaida.
6.Tumia mshipi wa mgongo
Watu wenye matatizo ya uti wa Mgongo wanapaswa kutumia mshipi wa kufungia mgongo Ili kuufanya mgongo uweze kushikana vizuri na pingili zinaweza kurudi kwenye hali yake kawaida, kwa kufanya hivyo mtu anaweza kukaa kwa mda mrefu kusimama kwa mda mrefu akiwa amefunga mgongo wake.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa vericose veini, hili ni tatizo ambalo utokea katika mzunguko wa damu hasa kwenye miguu.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu faida za bamia mwilini
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na maambukizi ya tishu ya matiti ambayo husababisha maumivu ya matiti, uvimbe, joto na uwekundu. Pia unaweza kuwa na Homa na baridi. Ugonjwa huu huwapata zaidi wanawake wanaonyonyesha ingawa wakati mwingine hali hi
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea sababu za maumivu ya tumbo kitovu i
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu namna ya kushiriki ngono na mtu aliye na VVU na UKIMWI
Soma Zaidi...Zijuwe sababu za kuumwa nankichwa upande mmoja wa kichwa.
Soma Zaidi...Upasuaji ni kundi la ki medical linalohusu kutoa kiungo kisichohitajika kwenye mwili.
Soma Zaidi...Ugonjwa wa ulevi wakati Mtoto akiwa tumboni (fetasi) ni hali ya mtoto inayotokana na unywaji pombe wakati wa ujauzito wa mama. Ugonjwa wa pombe wa fetasi husababisha uharibifu wa ubongo na matatizo ya ukuaji.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na sababu zinazopelekea kukosa choo ,yaani kinyesi kuwa kigumu au kukosa kabisa choo.
Soma Zaidi...