image

taratibu na namna ya kutaliki, na mambo ya kuzingatia

Taratibu za Kutaliki KiislamuKama palivyo na taratibu za kuoa Kiislamu ndivyo hivyo pia ilivyo katika kuvunja ndoa.

taratibu na namna ya kutaliki, na mambo ya kuzingatia

Taratibu za Kutaliki Kiislamu
Kama palivyo na taratibu za kuoa Kiislamu ndivyo hivyo pia ilivyo katika kuvunja ndoa.
Itakapofikia hatua kuwa mume na mke hawanabudi kuachana, itabidi ufuatwe utaratibu wa kuachana kama ulivyobainishwa katika sharia ya Allah (s.w):


Ewe Mtume mtakapotoa talaka kwa wanawake, toeni talaka katika wakati wa eda zao. (Yaani waacheni wakati wa twahara zao ambazo katika twahara hizo hamkuwahi bado kuwaingilia.) Nafanyeni hisabu ya (siku za) eda. Na mcheni Allah, Mola wenu. Msiwatoe katika nyumba zao wala msitoke wenyewe. ila wakifanyajambo la ufasiki ulio wazi. Na hii ni mpaka ya Allah. Na anayeruka mpaka ya Allah basi amejidhulumu nafsi yake. Hujui (sababu ya kuamrishwa haya). Labda Allah atatokezeshajambojingine baada ya haya (yaanijambo la kupatana). (65:1)


Basi wanapofikia muda wao, ima (warejeeni) muwaweke kwa wema, au farikianeni nao kwa wema; na mshuhudishe mashahidi wawili waadilfu miongoni mwenu. Na simamisheni ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu. Hivyo ndivyo anavyoagizwa yule anayemuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho. Na anayemuogopa Mwenyezi Mungu, (Mwenyezi Mungu) humtengenezea njia ya kuokoka (katika kila balaa). (65:2)



Na wale waliokoma na kutoka hedhi miongoni mwa wanawake wenu, ikiwa mnayo shaka (katika muda wao wa eda), basi muda wa eda yao ni miezi mitatu, na (pia ndiyo eda kwa wale) ambao hawajapata hedhi bado. Na wanawake wenye mimba eda yao ni mpaka watakapozaa. Na anayemwogopa Mwenyezi Mungu, (Mwenyezi Mungu) humfanyia mambo yake kuwa mepesi. (65:4)


Wawekeni humo humo mnamokaa nyinyi, kama mpatavyo (japokuwa mumewawacha; maadamu eda yao hajesha). Wala msiwadhuru kwa kuwatia dhiki. Na kama wakiwa na mimba, wagharimieni mpaka wajfungue. Na kama wakikunyonyesheeni, basi wapeni ujira wao. Na shaurianeni kwa wema. Na kama mkiona udhia baina yenu, basi amnyonyeshe mwanawe (mwanamke) mwengine. (65:6)



Na wanawake walioachwa wangoje (wasiolewe) mpaka twahara tatu zishe. Wala haiwajuzii kuficha (mimba) aliyoumba Mwenyezi Mungu katika matumbo yao, ikiwa wanamwamini Mwenyezi Mungu na siku ya Mwisho. Na waume wao wana haki ya kuwarejesha katika muda huo, kama wakitaka kufanya suluhu. Nao (wanawake) wanayo haki kwa Sharia (kufanyiwa na waume zao) kama ile haki iliyo juu yao kuwafanyia waume zao. Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu (na) Mwenye hi/dma. (2:228).


Talaka (unazoweza kumrejea mwanamke) ni (zile zilizotolewa) mara mbili (za kwanza). Kisha ni kumweka kwa wema au kumwacha kwa ihsani. (Wala usiweze kumrejea tena mpaka aolewe na mume mwengine). Wala si halali kwenu kuchukua cho chote mlichowapa (wake zenu), isipokuwa (wote wawili) wakiogopa ya kwamba hawataweza kusimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu. Basi mkiogopa kwamba hawataweza kusimamisha mipaka ya Mwenyezi Mungu, hapo itakuwa hapana dhambi kwao (mwanamume wala mwanamke katika) kupokea (au kutoa) ajikomboleacho mwanamke. Hii ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu; basi msiiruke. Na watakaoiruka mipaka ya Mwenyezi Mungu, hao ndio madhalimu (wa nafsi zao). (2:229)



Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa utaratibu wa kutaliki Kiislamu ni kama ifuatavyo:
I .Talaka hutolewa kwa matamshi au maandishi kuwa "Nimekuacha" (au kwa maneno mengine yenye maana hiyo).



2.Utoaji wa talaka ushuhudiliwe na mashahidi wawili waadilifu.



3.Talaka itolewe wakati mke yuko katika kipindi cha twahara na wasiwe wamefanya tendo Ia ndoa katika kipindi hicho. Kama wamefanya tendo Ia ndoa katika kipindi hicho cha twahara talaka isitolewe kwani haitasihi. Vile vile talaka haisihi kutolewa mwanamke anapokuwa katika hedhi.



4.Baada ya talaka kutolewa mke analazimika kukaa eda mle mle katika nyumba ya mumewe wakiishi pamoja kama kawaida isipokuwa tu watatengana kwenye malazi. Kila mmoja atawajibika kwa mwenzake kama kawaida katika kipindi chote cha eda.



Eda ya kuachwa ni kipindi maalumu anachokaa mwanamke aliyeachwa ambamo mume aliyemtaliki anaweza kumrejea (kwa talaka rejea). Mwanamke huachika baada ya eda na kuwa huru kuolewa na mume mwingine. Kipindi cha eda kwa wanawake kwa wale wanaopata hedhi ni twahara tatu na wale wasiopata hedhi ni miezi mitatu baada ya kutamkwa talaka. Eda ya mwanamke mwenye mimba huisha pale anapojilungua.Hekima ya kuamrishwa kukaa eda ni kama ifuatav:



(a) Kuwapa wawili muda wa kufikiri zaidi juu ya kuachana kwao na ndio hekima ya amri ya Allah ya kukaa nyumba moja. Katika kipindi hiki mwanamke anashauriwa ajipambe na kujiringisha mbele ya mumewe. Kama mke ndiye aliyoomba talaka, mumewe anatakiwa ajirekebishe na kuonyesha mapenzi na upendo kwa mkewe na azidishe kumletea zawadi.



(b) Kuthibitisha uhalali wa mtoto. Mtoto wa mume aliyetaliki asije akafanywa mtoto wa mume mwingine atakayemuoa mtalikiwa.



5.Kama wawili hawa wataamua kurejeana kabla ya eda kwisha watarejeana kwa wema kwa ahadi mbele ya Allah (s.w) kuwa wataishi kwa upendo.



6.Baada ya eda wawili hawa wanaamrishwa na Mola wao kuachana kwa wema.



7.Si halali kwa mwanamume aliyetoa talaka kuchukua chochote katika vile alivyompa mkewe.



8.Mwanamume anayemwacha mkewe anawajibika kumliwaza kwa kumpa kitoka nyumba (kitu) kitakachomuwezesha kumuweka sawa kiuchumi na kisaikolojia kutokana na mabadiliko haya ya maisha (Qur-an 2:41)



Hakuna kiwango maalumu cha kitoka nyumba kilichowekwa, bali mume atatoa kiasi kinachokidhi haja kwa kadiri ya wasaa wake kama aya inavyotuelekeza: Lakini wapeni cha kuwaliwaza (kitoka nyumba), mwenye wasaa kadiri awezavyo, na mwenye dhiki kadiri awezavyo " (2:236).



9.Mwanamke aliyeomba talaka anawajibika kujikomboa kwa kumrudishia mumewe mahari aliyompa. Mume akisamehe mahari hayo hapana lawama.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 615


Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Fadhila za kufunga mwezi wa ramadhani
Soma Zaidi...

Zijuwe nguzo tano za uislamu na maana zake katika sheria ya uislamu
Hili ni somo letu la kwanza kwenye mtiririko huu wa darsa za fiqh. Katika somo hili utakwenda kujifunza maana ya uislamu na nguzo zake. Soma Zaidi...

Kutoa vilivyo vizuri
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Umuhimu wa uchumi katika uislamu
Post hii itakufundisha faida na umuhimu wa kijenga uchumi katika jamii ya kiislamu. Soma Zaidi...

Sera ya uchumi katika Uislamu
4. Soma Zaidi...

Mambo yanayoharibu swala yaani yanayobatilisha swala.
Post hii itakufundisha mambo ambayo yatasababisha swqla yako isikubaliwe. Soma Zaidi...

Siku ya idi al-fitir na namna ya kusherekea idi
Soma Zaidi...

Je ni kwa nini lengo la finga halifikiwi kwa wafungaji
Lengo la funga ni kuwa mchamungu sasa ni kwa nini wafungaji hawalifikii lengo hili na kuwa wachamungu. Soma Zaidi...

Funga za kafara, aina zake na sababu za funga hizi za kafara na hukumu zake
Soma Zaidi...

Swala ya Idi al-fitir na namna ya kuiendea
Soma Zaidi...

Swala ya jamaa.
Kipengele hiki tutajifunza kusimamisha swala ya jamaa,swala za ijumaa. Soma Zaidi...

Yajuwe masharti ya udhu yaani yanayofanya udhu kukubalika
Posti hii itakufundisha masharti yanayohitajika kwa mwenye kutaka kutia udhu. Soma Zaidi...