Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za minyoo
DALILI ZA MINYOO
Wakati mwingine ni vigumu sana kujua kama una minyoo, kwani minyoo wanaweza kukaa ndani ya mwili kwa muda mrefu bila ya kuonesha dalili yeyote, ama madhara yeyote. Na dalili za minyoo pia hutofautiana sana, kulingana na aina za minyoo. Lakini zifuatazo ni katika dalili kuu:-
Kichefuchefu
Kukosa hamu ya kula
Maumivu ya tumbo
Kupungua uzito
Uchovu wa viungo
Kuona utelezi mwingi kama kamasi kwenye kinyesi
Kuona minyoo kwenye kinyesi.
Kuona damu kwenye kinyesi
Tumbo kujaa
Dalili hizi kama nilivyotangulia kusema kuwa zinatofautiana kulingana na aina ya minyoo. Sasa hebu tuone kwa ufupi dalili hizi kulingana na aina ya minyoo:-
minyoo aina na tapeworm dalili zao ni:
Kuvimba kwa ngozi ama kujaa ama kujaa kwa tumbo
Kuwa na alegi
Kuwa na homa
Matatizo katika mfumo wa fahamu, kama kifafa
minyoo aina ya hookworm dalili zao ni kama:-
Kuwashwa
Kupata ugonjwa wa anaemia (upungufu wa seli hai nyekundu kwenye damu) hivyo kukosa oksijeni ya kutosha mwilini
Kuwa na uchovu wa hali ya juu.
minyoo aina ya trichinosis, minyoo hawa wana dalili kama:-
Kupata homa
Kuvimba kwa uso
Maumivu ya misuli na kuchoka
Maumivu ya kichwa
Kutokupenda kupigwa na mwanga
Matatizo katika macho (conjuctivist)
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Ugojwa wa pumu ni hatari na unaweza kutokea ghafla. Lakini je unaweza kusababisha kifo, makalahii itakwend akujibu swali hili
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kuepuka Ugonjwa wa raundi.
Soma Zaidi...Seli ni chembechembe hai ambazo zimo ndani ya mwili wa binadamu na hufanya kazi mbalimbali kwenye mwili, binadamu hawezi kuishi bila seli.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia ambazo VVU huambukizwa
Soma Zaidi...Katika makala hii utajifunza kuhusu kifua kikuu, dalili zake, sababu zake, chanzo chake na mambo hatari kwa mgonjwa.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu mbalimbali,za miguu kufa ganzi,ni tatizo ambalo uwakumba watu wengi na walio wengi hawafahamu kabisa ni sababu zipi ambazo uleta tatizo hili.
Soma Zaidi...Kuona damu kwenye mkojo kunaweza kusababisha wasiwasi. Ingawa katika hali nyingi kuna sababu zisizofaa, Damu kwenye mkojo (hematuria) pia inaweza kuonyesha ugonjwa mbaya.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi ugonjwa wa kuharisha, kuharisha ni kitendo Cha kupitisha kinyesi Cha maji chenye damu au kisichokuwa na damu
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Ugonjwa wa akili .
Soma Zaidi...MATATIZO YA CHOO KIDOGO NA FIGOFigo ni kiungo muhimu sana katika uchujaji wa mkojo, na afya ya mfumo wa utoaji taka mwili.
Soma Zaidi...