Posti hii inahusu zaidi magonjwa nyemelezi ambayo kwa kawaida utokea pale ambapo kinga ya mwili inashuka.
Magonjwa nyemelezi
1.Ugonjwa wa kifua kikuu
Ni mojawapo ya magonjwa nyemelezi kwa kawaida utokea pale ambapo kinga ya mwili ikishuka huu ugonjwa unaweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya hewa au endapo mgonjwa hajaanza kutumia dawa na pengine uambukizwa pale mtu akishika makohozi ya mgonjwa wa kifua kikuu na kama hajanawa mikono anaweza kushika kitu chochote Cha kula akajiambukiza, zifuatazo ni dalili za ugonjwa wa kifua kikuu.
_ kukohoa ndani ya wiki mbili na zaidi
_ kupungua uzito
_ kuwa na joto hasa wakati wa usiku
_ Homa za mara kwa mara
_ makohozi kuwa na damu
2. Magonjwa ya ngozi
Huu ni ugonjwa ambao pia ni nyemelezi kwa mtu ambaye kinga yake Iko chini, ambapo ngozi ya mgonjwa ushambulia sana na bakteria na kufanya mwili uwe na maupele upele ambayo hayaponi au uchukua mda mrefu kupona na pengine vidonda uweza kusababisha maambukizi mengine kama vile Homa kupanda zaidi na kusababisha madhara makubwa hasa kwa watoto kama vile degedege kwa hiyo tunapaswa kuwa macho iwapo kinga ya mwili ikishuka na kutafuta njia ya kuipandisha.
3.Kandidiasisi
Ni ugonjwa nyemelezi ambao utokea ikiwa kinga ya mwili ikishuka na hasahasa ushambulia sehemu za Siri na kusababisha maupele na kumfanya mtu aanze kujikinga , huu ugonjwa usababishwa na fangasi ambazo ushambulia sehemu za Siri,kwahiyo unaweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya kujamiiana kwa mtu Mwenye ugonjwa na ambaye Hana,kwa hiyo mtu akiwa na huu ugonjwa anapaswa kwenda hospitalini Ili akapatiwe dawa maana ugonjwa huu upo na unatibika
4. Mkanda wa jeshi.
Huu ni ugonjwa ambao utokea Baada ya kinga ya mwili kushuka, ugonjwa huu usababishwa na virusi ambaye ushambulia kulingana na sehemu ya nevu zinapopita kwa hiyo maambukizi uendana na nevu ya sehemu ndo maana utakuta mtu amishambuliwa sehemu fulani, Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na Homa kutokea, maumivu kwenye sehemu ya maambukizi. Mgonjwa wa mkanda wa jeshi anaweza kupatiwa dawa kwa kufuata nadalili na hali ya maumivu na vidonda vilivyopo.
Magonjwa nyemelezi yakitokea ni lazima mgonjwa apelekwe hospitali mara moja Ili kuepuka madhara makubwa yanayoweza kujitokeza kwa sababu iwapo kinga imeshuka sana magonjwa zaidi ya mawili yanaweza kutokea kwa wakati mmoja, kwa hiyo tuwe makini kulinda afya nzetu na kutumia dawa zinazohitajika .
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Madonda ya tumbo ni ugonjwa unaotokana na kuwepo kwa vidonda kwenye Koo, tumboni na kwenye utumbo mdogo
Soma Zaidi...Fangasi hawa kitaalamu wanafahamika kama vagina yeast infection na majina mengine ya kitaalamu ni kama vagina candidiasis, u vulvovaginal candidiasis au candidal vaginitis.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunz akuhusu ugonjwa wa Bawasiri na dalili zake. Pia utajifunza njia za kujilinda nao.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia Watu wale ambao wana Maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maradhi ya macho,dalili na matibabu yake
Soma Zaidi...SABABU ZA KUTOKEA KWA VIDONDA VYA TUMBO Sababu za kawaida za vidonda vya tumbo ni maambukizo na bakteria Helicobacter pylori (H.
Soma Zaidi...Malaria ni katika maradhi yanayosumbua sana na kusababisha maradhi ya watu wengi sana duniani.
Soma Zaidi...Ukimwi ni upungufu wa kinga mwilini.unasababishwa na virusi ambavyo hutokea kwa mtu mwingine kwa njia mbalimbali
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dalili za uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo, ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye tatizo la uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo, ingawa sio watu wote wenye dalili kama hizi Wana uvimbe kwenye kibofu Cha mkojo Ila zikitokea mtu anapaswa
Soma Zaidi...Saratani inahusu ugonjwa wowote kati ya idadi kubwa ya magonjwa ambayo yanaonyeshwa na ukuaji wa seli zisizo za kawaida ambazo hugawanyika bila kudhibitiwa na kuwa na uwezo wa kupenya na kuharibu tishu za kawaida za mwili. Saratani mara nyingi ina uwezo
Soma Zaidi...