Post hii itakwena kukufundisha kuhusu historia fupi ya Ukimwi na matibabu yake. Ni wapi wapo hatarini kupata maambukizi na ni kitu gani wafanye?
Ukimwi ni moja ya matatizo ya kiafya ambayo yanaathiri afya ya mwili, akili na kijamii. Toka dunia imeanza kutambuwa ugonjwa huu miaka ya 1980 mpaka sasa tayari mamilioni ya watu wamesha kufa kutokana na maradhi yanayohusiana na UKIMWI. kila mtu anaweza kupata ukimwi awe mtoto ama mtumzima. Lakini wapo watu ambao wapo hatarini Zaidi. Je na wewe ni miongoni mwao, je unataka kujuwa ni tahadhari zipi watumie, na dawa zipi watumie? Endelea na Makala hii upate majibu yako.
Kutokana na mendeleo ya sayansi na teknolojia hasa katika Nyanja za afya, leo hii watu walio hatarini Zaidi kupata maambukizi wanaweza kupewa dawa za kusaidia kuwakinga na kuwapunguzia hatari ya kuweza kupata maambukizi mapya. Hata jhivyo elimu Zaidi bado inatolewa kuwasaidi watu hawa kuweza kujilinda na kujikinga na maabukizi ya VVU na UKIMWI. Bilas haka ungependa kuwajuwa watu hawa pamoja na tahadhari wanazopatiwa na wanazopasa kuzitumia. Basi endelea na Makala hii hadi mwisho.
Je ni kina nani hao walio hatari Zaidi kupata maambukizi?
Kama nilivyokueleza hapo mwanzo kuwa kila mtu yupo hatarini kupata maambukizi bila ya kujali umri, eneo, jinsia wala muonekano. Lakini wapo watu ambao wao wapo hatarini Zaidi. Hatari hii hutokana na maeneo wanayoishi, jamii wanayoishi, tabia zao na shughuli wanazofanya. Hapa nitakuletea baadhi tu ya watu ambao wapo hatarini Zaidi kulingana na vigezo hivyo. Watu haw ani kama:-
Nini nifanye endapo ninaishi katika mazingira hatarishi ya kupata maambukizi?
Kama upo hatarini kupata maambukizi, ni vyema ufike kituo cha afya na uonane na wataalamu wa ushauri nasaha. Hawa ni wataalamu ambao watakupatia maelekezo ya kufanya, na ushauri juu ya kujilinda na maambukizi kulingana na hali ya sehemu unayoishi.
Kama tatizo ni tabia ama namna ambavyo unavyoishi ndio hukutia katika hatari ya kupata maambukizi, jitahidi kubadili tabia na kuwa muaminifu. Kwa washiriki wa ngono kinyume na maumbie hii tabia ni hatari zaidi kupata maambukizi. Matumizi ya kondomu ni muhimu kama upo hatarini na unaishi na muathirika. Ni vyema kumuachisha ziwa mtoto mapema iwezekanavyo hata kabla ya kuota mengo yanayong’ata.
Mama mjamzito akiwa muathirika ahakikishe anafata masharti yote aliyopewa, ana awe anahudhuria kituo cha afya kama alivyopangiwa. Ameze dawa vyema na kwa utaratibu. Lishe bora kwa mama mnyonyeshaji na mwenye ujauzito ni muhimu sana. Wakifanya hivi wanaweza kupunguza hatari ya watoto wao kupata maambukizi.
Nini nifanye endapo ninahisi kuwa nimepata maambukizi ama nimeshiriki ngono na muathirika?
Hili ni katika maswali mengi yaliyopata kuulizwa na watu mitandaoni. Nini mtu afanye endapo atafanya ngono na muathirika ama nini mtu afanye endapo atahisi kuwa amepata maambukizi. Jibu la maswahi haya linaweza kuwa fupi tu nalo ni kumwambia aende kituo cha afya kisha akutane na watoa ushauri nasaha. Majibu zaidi juu ya maswli yake yatakayotokana na swali hili atayapata huko.
Mtu huyu anatakiwa afike kituo cha afya kwa sababu si kila anayeshiriki ngono na muathirika naye atakuwa na maambukizi. Kuna sababu nyingi zinazofanya mtu ashiriki ngono zembe na muatirika na asipate maambukizi. Hivyo huwenda naye akaondolewa hofu kutokana na maelezo yake ikawa hakuna haja ya kuishi kwa hofu kuwa ni muathirika.
Pia kituo cha afya anaweza kupatiwa dawa za kutumia iwe kama kinga ya kuzuia maambukizi mapya endapo atakuwa amewahi ndani ya muda muafaka. Siku hizi wauguzi wanaweza kujiweka salama kwa ailimia zaidi ya 90 baada ya kuingia katika hatari ya kupata maambikizi kama kujichoma sindano iliyomchoma muathirika na namna nyinginezo. Watu wanaobakwa hupatiwa dawa hizi iwe kama kinga endapo kutatokea maabukizi.
Ni matibabu gani hupatiwa mtu aliye hisi kupata maambukizi?
Endapo itahitajika na mtu akiwa amewahi kufika kituo cha afya kuna dawa anaweza kupewa ili kumlinda na maambukizi. Kuna matibabu aina 2 ambao ni PrEP na PEP. Dawa hizi hutumika kulingana na mazingira hatarishi yaliyompata mtu, na ni kwa kiasi gani huwenda atakuwa amepata maambukizi. Sasa hebu tuone nana ambavyo dawa hizi hutumika na je ni kwa kiasi gani mtu atakuwa salama.
PrEP ni ufupisho wa maneno pre-exposure prophylaxis. Daw hii hupatiwa mtu ambaye anahisi huwenda atakuwa amepata maambukizi. Kwa mfano mtu aliyeshiriki ngono akiwa na kondomu na mwenye maambukizi ama awe anamuhisi lakini hana uhakika kuwa ana maambukizi. Kwa hiyo kabla ya kupewa dawa hizi mtu huyo kwanza atafanyiwa vipimo kujuwa kama hana virusi kisha ndipo apatiwe dawa.
PEP kifupisho cha maneno post-exposure prophylaxis. Dawa hizi hupatiwa mtu ambaye amepata maambukizi mapya. Kwa mfano amejishoma na sindano ambayo amechomwa muathirika. Ama ameshiriki ngono zembe na mtu muathirika ama mtu aliyebakwa naye atapewa dawa hii.
Kuna dawa nyingi ambazo zipo kwenye matibabu haya mawili. Lakini pia zipo dawa mabazo zinafanya kazi zote mbili kama PrEP na kama PEP. Kwa mfano dawa iitwayo Truvada hii inafanya kazi zote mbili. Baada ya kumeza dawa hizi unaweza kuona mabadiliko kama:-
Tukitane makala inayofata tutakapoona mambo kadhaa kuhusu vidonda vya tumbo.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukuletea baadhi ya watu walio hatarini kupata fangasi
Soma Zaidi...Posti hii inahusu namna ya kumsaidia mgonjwa aliyepungukiwa na damu kwa sababu ya minyoo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu huduma kwa wanawake wenye mahitaji maalum, ni wanawake ambao wana shida ya akili, walionyanyaswa kijinsia, wakimbizi na wote wenye matatizo mbalimbali.
Soma Zaidi...Zipo aina nyingi za fantasy ambazo ni rahisi kuathiri binadamu. Wipe ambao haiathiri mdomo, nyayo, shemu za siri na kwenye ngozi.
Soma Zaidi...Hepatitis B Ni maambukizi ya ini ambayo yamekuwa sugu kuanzia mwezi na kuendelea.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi watu walio katika hatari ya kupata Maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi,ni kutokana na kazi zao pamoja na mazingira yao kwa hiyo wako kwenye hatari ya kupata Ugonjwa wa ukimwi.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunz akuhusu ugonjwa wa Bawasiri na dalili zake. Pia utajifunza njia za kujilinda nao.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za presha ya kushuka
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dalili za mtu aliyegongwa na nyoka, nyoka ni kiumbe ambacho Kina sumu kali na sumu ikiingia mwilini mtu huwa na dalili mbalimbali
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Magonjwa vya kurithi ambayo mara nyingi utokea kwenye jamii ni magonjwa ambayo yanaweza kutokea kwenye familia na wanafamilia walio wengi wakaweza kupata ugonjwa huo Magonjwa yenyewe ni kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...