Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo zinaweza kutokea iwapo Kuna upungufu wa homoni ya progesterone.
1. Pre menstrual syndrome ( ni hali ambayo uwakumba wanawake) kwa kawaida uanza wiki Moja Hadi mbili kabla ya kuona siku zake za mwezi , mwanamke anaweza kuona uchovu miwasho ya ukeni uwepo wa vipele vyekundu na vyeusi na pengine vipele hivyo vinaweza kutokea kwenye sehemu zake za Siri pamoja na usoni na pia mwanamke anaweza kuwa na mabadiliko ya mood kama ifuatavyo.
2. Kutokwa na mimba .
Kama Mama ana mimba inaweza kutoka kwa sababu ya kutokuwepo kwa homoni ya projestron kwa sababu usaidia katika makuzi makubwa ya mtoto.
3. Kuongezeka uzito kwa ghafla.
Kuna wakati mwingine unaweza kuona mwanamke anaongezeka Uzito ghafla ukadhani labda maisha yamemkubali kumbe ni upungufu wa homoni aina ya progesterone.
4 . Kuwepo kwa wasi wasi ambao haukuwepo hapo mwanzoni hali hii utokea ghafla kwa wanawake kila kitu anachokifanya anakifanya kwa wasi wasi mkubwa sana.
5. Kukosa usingizi.
Hali hii utokea sana kwa wamama ambao Wana upungufu wa homoni hii hasa wale akina Mama walioingia kwenye menopause wanaopatwa na hali ya kukoka usingizi.
6. Maumivu au uvimbe kwenye maziwa
Kwa kawaida maumivu kwenye maziwa utokea na kwa mara nyingine uvimbe, kwa upande wa uvimbe matibabu yanaoaswa kutolewa Ili kuepuka matatizo mengine yaliyo makubwa zaidi.
7. Kuwepo kwa kizungu zungu mara kwa mara.
Kama homoni hii ya progesterone imepungua utasikia akina Mama walio wengi Wanalalamika kuhusu kizungu zungu.
8. Kuwepo kwa ugumba.
Kwa kawaida homoni ya progesterone inasaidia sana kwenye makuzi ya mtoto kwa hiyo ikikosa usababisha Mama kukosa mtoto inawezekana mimba ikawa imeshatungwa ikatoka au mimba haitungwi kabisa.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
SIKU YA KUPATA UJAUZITO Mimba hutokea pindi mbegu ya kiume (sperm) inapokutana na yai la mwanamke (ova) na kuungana kwa pamoja kutengeneza selli moja iitwayo zygote.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuongea na Mama mjamzito ili kuweza kugundua tatizo lake na kutoa msaada pale penye uhitaji.
Soma Zaidi...Utajifunza sababu za maumivu ya uume na uke wakati wa tendo la ndoa na baada ya tendo la ndoa na matibabu yake.
Soma Zaidi...Mama mjamzito anaruhusiwa kushiriki tendo la ndoa mpaka siku ya kujifungua Kama mume wake pamoja na yeye akiwa Hana maambukizi ya zinaa na Kama akiona dalili zozote zile za hatari ndio hataruhusiwa kushiriki tendo la ndoa.
Soma Zaidi...Nitajuwaje kama mjamzito amekaribia kujifunguwa, ni dalili gani anaonyesha, dalili za uchungu wa kujifunguwa
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ya kutumia madawa ya kupunguza maumivu,ni madhara ambayo utokea kwa mtu anayetumia madawa ya kupunguza maumivu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mambo ambayo Mama mjamzito anaweza kuulizwa pindi anapokuja kwenye kliniki ya uzazi ,ni mambo muhimu na ya lazima yanayopaswa kuongea na Mama mjamzito ili kuweza kuona maendeleo yake kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kazi ya homoni ya HCG katika kupima mimba, HCG maana yake ni human chorionic gonadotropin ni homoni ambayo uonekanekana kwenye mkojo na damu kama mtu ana mimba.
Soma Zaidi...