1.
1. Twahara
Maana ya Twahara:
βTwaharaβ ni neno la Kiarabu lenye maana ya usafi wa nje ulioambatana na usafi wa ndani ya mtu. Usafi wa nje unahusiana na usafi wa mwili na nguo na usafi wa ndani unahusiana na utakaso wa nafsi. Mwili na nguo hutwaharika kwa kusafisha kwa kufuata maelekezo
ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Ama nafsi hutwaharika kwa kumtii Allah na Mtume wake kwa kufuata maamrisho yao na kuacha maovu na machafu waliyotukataza. Watu waliotwaharika kwa mtazamo huu hupendeza mbele ya Allah (s.w) kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:
β...Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanaotubu na huwapenda wanaojitakasa (wanaojitwaharisha)β (2:222)
β...Humo wamo watu wanaopenda kujitakasa. Na Mwenyezi Mungu anawapenda wajitakasaoβ. (9:108)
Kwa ujumla tunaweza kusema twahara kwa mtazamo wa Qur-an ni usafi wa nguo zetu, miili yetu, hisia zetu, mawazo yetu na mwenendo na tabia zetu kwa mujibu wa maelekezo ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
Pamoja na maana hii ya ujumla, Muislamu aliyetwaharika na kuwa tayari kusimama kwenye swala ni yule aliyeepukana na Najisi na Hadathi. Hivyo tunapojitwaharisha kwa ajili ya swala tunajishughulisha na kuondoa Najisi na Hadath.
Umeionaje Makala hii.. ?
Je inapoonekana sehemu moja tufunge duania nzima ama tufunge kwa kuangalia mwandamo katika maenro tunayoishi.
Soma Zaidi...Haya ni mamno muhimu yanayozingatiwa kabla ya kuanza zoezi la kugawa mirathi ya marehemu.
Soma Zaidi...Lengo la Kusimamisha SwalaBila shaka swala imepewa umuhimu mkubwa kiasi cha kufanywa nguzo kubwa ya Uislamu kutokana na lengo lake.
Soma Zaidi...- Watumwa walikuwa wakikamatwa na kutezwa nguvu bila kujali utu na ubinaadamu wao.
Soma Zaidi...