image

Usiku wa lailat al qadir maana yake na fadhila zake. Nini ufanye katika usiku wa lailat al-qadir

Usiku wa lailat al qadir maana yake na fadhila zake. Nini ufanye katika usiku wa lailat al-qadir

Umuhimu wa usiku wa Lailatul Qadr



Umuhimu wa Usiku wa Lailatul Qadr umebainishwa wazi katika Qur-an kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:


Katika (usiku) huu hubainishwa kila jambo la hikima. Ndiyo hukumu itokayo kwetu; kwa hakika sisi ni w aletao (Mitume ili w awaongoe watu). (44:4-5).
Katika Suratul-Qadr tunasoma


“Hakika tumeiteremsha (Qur-an) katika Lailatul-Qadr (Usiku wenye heshima kubwa). Na ni jambo gani litakalo kujulisha ni nini huo usiku wa Lailatul-Qadr? Huo usiku (wa Lailatul-Qadr) ni bora kuliko miezi elfu. Huteremka Malaika na Roho (Jibril) katika usiku huo kwa idhini ya Mola w ao kw a kila jambo. Ni amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajir. ” (9 7:1 -5).



Tunajifunza katika aya hizi kuwa Allah (s.w) ameutukuza Usiku mmoja katika mwezi wa Ramadhani ili iwe kumbukumbu kwa Waumini wa umati huu wa Mtume Muhammad (s.a.w), ya kuletewa mwongozo pekee wa maisha yao kutoka kwa Mola wao. Mwongozo ambao huwa ni ponyo na rehma kwa Waumini na ambao hauwazidishii makafiri ila khasara:



Na tumeteremsha katika Qur-an (hayo mafundisho yake) ambayo ni ponyo (poza la nyoyo) na rehema kwa wanaoamini. Wala hayawazidishii (mafundisho haya) madhalimu ila khasara ” (1 7:82).



Tunafahamishwa katika aya zilizomo katika Surat Qadr kuwa Allah (s.w) ameutukuza usiku huu zaidi ya miezi elfu moja au miaka 83 na miezi 4. Ina maana kuwa muumini akifanya amali njema katika usiku huu, thamani yake katika malipo na katika uwezo wa kumfikisha mja kwenye lengo la maisha yake itakuwa ni kubwa zaidi ya thamani ya amali hiyo iliyofanywa kwa miezi elfu moja. Umuhimu wa lailatul-Qadr pia unabainika katika Hadith ifuatayo:



Ames imulia Abu Hurairah (r.a) kuwa Mtume (s.a.w) amesema: “Mwenye kufunga mwezi wa Ramadhani akiwa na Imani na akiwa na tegemeo la kupata malipo kutoka kwa Allah (s.w), basi dhambi zake zote zilizopita zitasamehewa. Na mwenye kusimama kwa swala katika usiku wa Qadr akiwa na imani na mategemeo ya kupata malipo kutoka kwa Allah, basi dhambi zake zote zilizotangulia zitasamehewa.” (Bukhari).



Ili kupata malipo na baraka ya usiku huu wa Lailatul-Qadr, Mtume (s.a.w) ametuhimiza sana kuupania huo usiku kwa kuzidisha ibada za usiku kwa kuswali, kusoma Qur-an, kumkumbuka Allah (s.w) kwa wingi na kuomba maghfira.



Aysha (r.a) ameeleza: Niliuliza: “Ewe Mtume wa Allah! Nifahamishe niseme nini nitakapoudiriki usiku uliobarikiwa ?” Akasema (Mtume s.a.w) sema; “Ee, Allah! Wewe ni Msamehevu Unayependa kusamehe, Basi (Nakuomba) Unisamehe”. (Ahmad, Ibn Majah, Tirmidh).



Usiku wa Lailatul-Qadr ni usiku uliofichwa na Allah (s.w). Yaani haijulikani siku maalum ya mwezi wa Ramadhani ambamo usiku huu hutokea. Kwa jitihada zetu tunaona hekima ya kufichwa usiku huu ni ili Waislamu wasiwe wavivu wa kufanya ibada katika mausiku yote ya mwezi wa Ramadhani na badala yake wakautegea usiku huo mmoja tu. Hata hivyo, kutokana na Hadith sahihi tunajifunza kuwa usiku huu hutegemewa zaidi kutokea katika kumi la mwisho la mwezi wa Ramadhani. Mtume (s.a.w) aliutafuta usiku huo katika kumi la mwisho kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:


Abu Sayed al-Khudr(r.a) am eeleza kuw a Mtum e (s.a.w) alikaa itiqaf katika siku kumi za kwanza za Ramadhani. Kisha akakaa tena itiqaf katika kumi la katikati la Ramadhani. Kisha aliinua kichwa chake akasema: “Hakika nilikaa Itiqaf katika siku kumi za mwanzo, niliutafuta usiku huu (wa Qadr). Kisha nilijiwa na kufahamishwa kuwa usiku huu hupatikana katika siku kumi za mw isho. Yule atakayekaa Itiqaf na mimi, basi na akae katika kumi la mwisho, kwa sababu nilionyeshwa kutokea kwake katika siku hizo lakini nilifanywa kusahau (siku gani hasa), japo niliuona mimi mwenyewe nikiwa (kwenye ndoto) nikiwa ninasujudu kwenye maji na matope. Basi utafuteni usiku huu katika siku kumi za mwisho na hasa mausiku ya witr ...” (Bukhari na Muslim).



Hadith hii inatufahamisha kuwa mtume (s.a.w) alibainishiwa u siku huo kuwa katika kumi la mwisho la Ramadhani na akakokoteza watu wakae Itiqaf katika kumi hilo.Pia kutokana na Hadith hii mausiku yenye mategemeo zaidi katika hili kumi la mwisho ni zile za witr - usiku wa 21, 23, 25, 27, na 29. Katika Hadith iliyosimuliwa na Zirri bin Hubaish (r.a) na kupokelewa na Muslim, usiku wa 27 umetiliwa mkazo zaidi. Lakini hasa alichosisitiza Mtume (s.a.w) sio kutegemea usiku mmoja tu kama vile usiku wa 27, bali kujizatiti kwa kuzidisha ibada za usiku kwa kuswali, kusoma Qur-an, kumkumbuka Allah kwa wingi, kuomba maghfira na dua mbali mbali kwa mausiku yote ya kumi la mwisho la Ramadhani.Hivi ndivyo alivyofanya Mtume (s.a.w) kama tunavyojifunza katika Hadith zifuatazo:



Aysha (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah alikuwa akijizatiti sana kufanya ibada katika mausiku ya kumi ya mwisho, kuliko ilivyokuwa kawaida yake katika wakati mwingine. (Muslim).



Aysha (r.a) ameeleza kuwa wakati usiku wa kumi la mwisho ulipoingia, Mtume (s.a.w) alikuwa akijifunga kibwebwe akikesha katika Ibada na akiamsha familia yake kwa swala. (Bukhari na Muslim).




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1235


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

DUA 113 - 126
DUA ZA WAKATI WA SHIDA Dua ya wakati wa taabu “LAA ILAAHA ILLA-LLAHUL-’ADHIMUL-HALIIMU. Soma Zaidi...

NAFASI YA SUNNAH KATIKA UISLAMU
Nafasi ya Sunnah katika UislamuMtume Muhammad (s. Soma Zaidi...

Je! inajuzu wanawake kuzuru makaburi?
As salaam alaykum warahmatullah wabarakatuh, nauliza inajuzu wanawake kuzuru makaburi? Soma Zaidi...

Maana ya dua na fadhila zake
Dua ni moja ya Ibada ambazo tunatakiwa kuziganya kila siku. Kuna fadhila nyingi sana za kuomba dua. Post hiibitakwenda kukujuza fadhila za kuomba dua. Soma Zaidi...

Maana ya sunnah (suna) na maana ya hadithi
Post hii itakufundisha maana ya neno sunnah katika Uislamu. Pia utajifunza maana ya neno hadithi katika uislamu Soma Zaidi...

kuwa mwenye hikma au hekima na faida zake
Elimu, pamoja na ubora wake, hainufaishi bila ya kutumiwa kwa hekima. Soma Zaidi...

Adabu ya kukaa na kula katika nyumba za watu
"Si vibaya kwa kipofu, wala si vibaya kwa kiguru, wala si vibaya kwa mgonjwa, wala kwenu, kama mkila katika nyumba zenu, au nyumba za baba zenu, au nyumba za mama zenu, au nyumba za ndugu zenu, au nyumba za dada zenu, au nyumba za ami zenu, au nyumba za s Soma Zaidi...

HADITHI NA SUNNAH
1. Soma Zaidi...

Hadithi Ya 32: Kusiwe Na Kudhuriana Wala Kulipiza Dhara
الحديث الثاني والثلاثون "لا ضرر ولا ضرار" عَنْ أَبىِ سَعيدٍ سَعْدِ بْن مَالكِ بْن سِنَانٍ الْخُدريِّ رضي الله عنه  أَنَّ رَسُولَ اللّ?... Soma Zaidi...

DUA ZENYE MANENO HAYA HUJIBIWA
SIFA ZA (MANENO NA MATAMSHI YA) DUA YENYE KUJIBIWA. Soma Zaidi...

DUA 41 - 50
41. Soma Zaidi...

Dua za kuomba wakati unapokuwa na maumivu kwenye mwili
Posti hii inakwenda kukufundisha dua za kuomba wakati wa kuwa na maumivu kwenye mwili wako. Soma Zaidi...