Kukaa itiqaf na sheria zake hasa katika mwezi wa ramadhani

Kukaa itiqaf na sheria zake hasa katika mwezi wa ramadhani

Kukaa itiqaf na sheria zake hasa katika mwezi wa ramadhani

Kukaa Itiqaf



Kukaa Itiqaf katika kumi la mwisho la Ramadhani ni sunna iliyokokotezwa. Ki-lugha “Itqaf” ina maana ya kukaa mahali. katika sheria ya Kiislamu “Itiqaf” ni kukaa msikitini kwa ajili tu ya kumkumbuka na kumtukuza Allah (s.w) na kufanya ibada maalum kama vile kuswali, kusoma Qur-an na kufanya amali yoyote njema ambayo inaruhusiwa kufanyika msikitini nje ya shughuli za kawaida za kutafuta rizki. Kwa hiyo mahali pa kukalia “Itiqaf” ni msikitini kama ilivyotajwa katika Qur-an:



“... Wala msichanganyike nao, na hali mmekaa Itiqaf misikitini .... ” (2:187).



Misikiti inayokaliwa Itiqaf iwe ni ile inayoswaliwa jamaa na Ijumaa ili pasiwe na haja ya kutoka kwa swala za jamaa au kwa swala ya Ijumaa. Wanawake wanaruhusiwa kufanyia Itiqaf zao majumbani mwao katika sehemu zao za kusalia lakini baada ya kupata ruhusa kutoka kwa waume zao. Kwa muda wote mtu atapokuwa katika Itiqaf haruhusiwi kutokatoka msikitini ila kwa dharura kubwa sana kama vile kwenda haja au kwenda kula. Mtu akiwa katika Itiqaf hulazimika kujitenga na shughuli zote za kutafuta maslahi ya maisha na shughuli zote za kijamii kama vile kutembelea wagonjwa, kuhudhuria mazishi, na kadhalika. Mtu anapokuwa katika Itiqaf haruhusiwi kuchanganyika na mkewe.


“ ... Na w ala msichanganyike nao na hali mnakaa Itiqaf msikitini. (2:187).
Kwa ujumla katika muda huu wa kukaa Itiqaf, Mu’takif (Mwenye kukaa Itiqaf) anatakiwa ajihusishe tu na ibada maalum kama vile kuswali, kusoma Qur-an, kuleta tasbihi, tahmid, tahalili, takbir, istighfar na maombi mbali mbali.



Mu’takif anaruhusiwa kuja na matandiko yake msikitini na kuyaweka mahali pa uficho ambapo hayatawakarahisha watu wakati wa swala ya jamaa. Katika miezi mingine isiyokuwa Ramadhani mtu anaweza kukaa itiqaf kwa muda wowote ule, siku moja au masaa machache. Ni vyema mtu anapokuwa hana shughuli muhimu, anuie kukaa Itiqaf msikitini badala ya kujiingiza kwenye shughuli zisizo muhimu au shughuli za upuuzi zenye kumuingiza katika dhambi na kumpotezea muda ambao ni rasilimali pekee ya maisha yake. Katika mwezi wa Ramadhani Itiqaf imekokotezwa sana katika kumi la mwisho ili kumuwezesha Muumini kuudiriki usiku wa Lailatul-Qadr - akiwa katika hali ya kumkumbuka Allah (s.w). Mtume (s.a.w) alikuwa akikaa Itiqaf katika kumi hili la mwisho kama tunavyojifunza katika hadith zifu atazo:



Ames imulia Abdullah bin Umar (r.a) kuwa Mtume (s.a.w) alikuwa akikaa Itiqaf katika siku kumi za mwisho za mw ezi wa Ram adhani. (Bukhari na Muslim).



Aysha (r.a.) amesimulia kuwa Mtume wa Allah alikuwa akikaa Itiqaf katika siku kumi za mwisho za Ramadhani mpaka alipotawafu (Allah alipo mchukua).Kisha wakeze waliendelea kukaa Itiqaf baada yake. (Bukhari na Muslim).




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views: 3007

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Dua za Mitume na Manabii    

Post zinazofanana:

Jinsi ya kutawadha hatuwa kwa hatuwa

Kutawadha ni katika ibada muhimu za mwanzo kutakiwa kuzijuwa na ni lazima. Swala yako haitaweza kutimia bila ya kujuwa udhu. Inakupasa kujuwa nguzo za udhu, yanayoharibu udhu na namna ya kutawadha kifasaha. Hapa utajifunza hatuwa za kutawadha

Soma Zaidi...
Kusimamisha swala.

Kwenye kipengele hiki tutajifunza maana ya swala ni nin?. Na masharti ya swala.

Soma Zaidi...
Utaratibu wa kuzika maiti ya kiislamu, hatua kwa hatua

Kuzika Kuzika ni kitendo cha nne cha faradh tunacho lazimika kumfanyia ndugu yetu aliyetutangulia kufa.

Soma Zaidi...
Ni kwa nini lengo la Funga na swaumu halifikiwi na wafungaji?

Kwa nini Lengo la Funga halifikiwi na Wafungaji Wengi?

Soma Zaidi...