6. Swala ya Idil-Fitri na Idil-HajjIddil-Fitri na Iddil-Hajj ni swala za Sunnah zilizokokotezwa. Iddi hizi mbili zinazofahamika vyema kwa Waislamu kuwa ni vilele vya siku mbili baada ya kukamilisha nguzo ya Funga na Hajj. Kielelezo cha kilele cha sherehe katika Uislamu si ngoma wala tarumbeta, wala si kula na kunywa sana, bali ni kumkumbuka Allah (s.w) na kumtaja kwa wingi.Swala ya Idd inaswaliwa baada ya jua kuchomoza na kabla ya jua kufika katikati. Ina rakaa mbili na khutuba kama swala ya Ijumaa lakini tofauti na Ijumaa, khutuba hufuatia baada ya swala. Kama ilivyo swala ya Ijumaa, swala za Idd mbili ni swala za jamaa. Ni sunnah ku swalia Idd uwanjani ili kukusanya jamaa kubwa zaidi.Swala ya Idd ikiangukia IjumaaMtume (s.a.w) ametoa ruhusa ya kutoswali swala ya Ijumaa iwapo itakuwa imeswaliwa swala ya Idd iliyoangukia siku ya Ijumaa kwa mujibu wa Hadithi zifuatazo:-
Zaid bin Arqam (r.a) ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) alisw alisha Idd kisha akatoa ruhusa kwa swala ya Ijumaa, akasema: “Anayetaka kuswali na aswali”. (Vitabu Vitano vya Hadith).Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Katika siku yenu hii ya leo zimekutana Idd mbili (yaani Idd na Ijumaa)basi anayetaka asiswali Ijumaa (swala ya Idd inatosheleza) lakini sisi tutaswali Ijumaa”. (Abu Daud).Kutokana na Hadithi hii ya mwisho, hii ni ruhusa tu na ni bora kuswali Iddi na Ijumaa kwani Mtume mwenyewe alifanya hivyo.