swala ya witri na namna ya kuiswali

3.

swala ya witri na namna ya kuiswali

3. Swala ya Witri
Witri maana yake ni namba isiyogawanyika kwa mbili kama vile 1, 3, 5, 7, 9, 11 n.k. Sunnah ya witri huswaliwa katika kipindi cha usiku baada ya swala ya Al-Isha na kabla ya kuingia swala ya Al-Fajiri. Lakini ni bora kuichelewesha Witri na kuiswali katika theluthi ya mwisho ya usiku, baada ya swala ya kisimamo (tahajjud).



Mtume (s.a.w) alikuwa akiswali Witri pamoja na swala ya Tahajjud (Swala ya Usiku) na wakati mwingine alikuwa akiswali Witri mara tu baada ya Al-Ishaai. Ni vema kuswali witri baada ya al-Isha kama hakuna uhakika wa kuamka Usiku. Mtume (s.a.w) ameikokoteza sana swala ya Witri kama tunavyojifunza katika hadithi ifuatayo:



Buraydah (r.a) amesimulia, Nimemsikia Mtume (s.a.w) akisema; Witri ni haq (wajibu). Asiyeswali si miongoni mwetu. Witri ni wajibuโ€. (Abu Da udi)



Witri ina swaliwa kwa rakaa tatu. Huswaliwa kwa rakaa mbili na kutoa Salaam, kisha hukamilishwa na rakaa moja.



Namna ya Kuswali Swala ya Witri
1. Katika rakaa ya kwanza utasoma Sura ya Al-Aโ€™alaa (Sabbihisma) baada ya Suratul-Faatiha.


Katika rakaa ya pill utasoma Suratul-Kaafiruuna baada ya suratul-faatiha..



Katika rakaa moja ya mwisho. baada ya kusoma Suratul-Faatiha, utasoma Suratul- lkhlas, AI-Falaq na An-naas. Kuleta Qunut (dua) katika rakaa ya mwisho katika ltidali.


Dua tunayoileta katika Qunut ni hii ifuatayo:


Allahumma ihdidaa fii man hadaita "Ewe Mola n[ongoze kama wale uliouxiongoza"



Wa `aafinaa fiiman `aafaita "Na unininusuru kama hao uliowarursuru"



Watawallanii fiiman tawaffaita "Na unitawalishe pamoja na wale ulio watawalisha



wabaarik lii fii maa a'atwaitanii "Na unitilie pataka katika vile ulivyonipa



Waqinii sharra maa gadhwaita "Unikinge na shari ulizonikadiria"


Tabaarakta rabbanaa wataโ€™aalaita "Ni nyingi kabisa juu yetu baraka zako na umetukuka kweli kweli"


Ni muafaka kuleta dua nyinginezo vile vile kulingana na haja ya mwenye kuswali.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Main: Dini File: Download PDF Views 5065

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 kitabu cha Simulizi    ๐Ÿ‘‰2 Kitabu cha Afya    ๐Ÿ‘‰3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    ๐Ÿ‘‰4 Kitau cha Fiqh    ๐Ÿ‘‰5 Simulizi za Hadithi Audio    ๐Ÿ‘‰6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana: