picha

Kafara ya mwenye kuvunja masharti ya ihram

Kafara ya mwenye kuvunja masharti ya ihram

Kafara kwa mwenye kuvunja masharti ya Ihram



Allah (s.w) kwa Urehemevu wake, ametoa nafuu kwa wale watakaovunja masharti ya Ihram kwa kutoa fidia isipokuwa kwa kosa la jimai.Tunafahamishwa katika Qur-an:


“... Na atakayekuwa mgonjwa katika nyinyi au ana vya kumuudhi kichw ani mw ake (akafanya yaliyokatazw a, kama vile kunyoa), basi atoe fidia kwa kufunga au (kwa kutoa) sadaqat au kuchinja mnyama ...” (2:196)


Katika Hadith tunafahamishwa:
Ka’ab bin Ajra (r.a) ameeleza: “Nilipokuwa katika (hali ya) Ihram kwa ajili ya ‘Umra nilisumbuliwa sana na chawa kichwani mwangu. Mtume wa Allah (s.a.w) akaniambia ninyoe kisha nifunge siku tatu au nichinje mbuzi wa sadaqat au niwalishe maskini sita. (Bukhari, Muslim, Abu Da ud).
Kwa hiyo kwa Muharim atakayevunja sharti lolote la Ihram atalazimika kutoa kafara kwa ama


(i) kufunga siku 3 au


(ii) kumchinja mbuzi na kuitoa nyama yake sadaqat au


(iii) kulisha maskini sita.



Kumwingilia mke ni kosa lisilosameheka kwa kutoa kafara bali hubatilisha Hija au ‘Umra moja kwa moja. Ama kwa mume aliyefanya mapenzi na mkewe kwa kubusiana na kumkumbatia bila ya kufanya kitendo cha ndoa, atatoa kafara ya ngamia (au thamani yake) kama atatokwa na manii na kama hatatokwa na manii, atatoa kafara ya mbuzi.
Kafara kwa mwenye kuwinda au kuonyesha windo akiwa katika Ihram ni mbuzi iwapo mnyama huyo ana ukubwa wa mbuzi, au mdogo zaidi kuliko hivyo; vinginevyo atatoa kafara ya mnyama aliye sawa na huyo aliyemuwinda au atatoa thamani yake anunue vibaba vya chakula kinacholiwa sana katika sehemu hiyo, na kumlisha kila maskini kwa vibaba vitakavyopatikana. Hivi ndivyo tunavyoagizwa katika Qur-an:


Enyi mlioamini! Msiue mawindo na hali ya kuwa mmo katika Hija au ‘Umra. Na miongoni mwenu atakayemuua makusudi basi malipo yake yatakuwa kwa (kuchinja) kilicho sawa na alichokiua katika wanyama wanaofugwa kama watavyohukumu waadilifu wawili miongoni mwenu.Mnyama huyo apelekwe ilipo Ka ’aba (akachinjwe na kutolewa sadaqat huko) au badala ya hayo ni kufunga, ili aonje ubaya wa jambo lake (hili). Mw enyezi Mungu ameyafuta yaliyopita; lakini atakayefanya tena Mw enyezi Mungu atam uadhibu. Na Mw enyezi Mungu ndiye Mw enye Nguvu na Mwenye kuadhibu. (5:95).




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: General Main: Dini File: Download PDF Views 1213

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi    👉2 ai web app    👉3 Bongolite - Game zone - Play free game    👉4 Dua za Mitume na Manabii    👉5 Simulizi za Hadithi Audio    👉6 web hosting   

Post zinazofanana:

KUAMINI MALAIKA

Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala

Soma Zaidi...
fadhila za kusoma quran

Fadhila na umuhimu wa kusoma quran 1.

Soma Zaidi...
mgawanyiko katika quran

MGAWANYIKO KATIKA QURAN Juzuu, Sura, Aya, Manzil, Qara Wataalamu wa elimu za Qurani katika fani za uandishi na usomaji wameigawanya Qurani katika mafungu ili kuwezesha urahisi kwa wasomaji wa qurani.

Soma Zaidi...
DARSA ZA TAWHID

Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala

Soma Zaidi...
HISTORIA YA UANDISHI WA HADITHI

Historia fupi ya uandishi wa Hadith za Mtume (s.

Soma Zaidi...
swala za tahiyatu al masjid, qabliya na baadiya

Muislamu anapoingia Msikitini kabla hajakaa anatakiwa aswali rakaa mbili za maamkizi ya msikiti, Tahiyyatul-Masjid.

Soma Zaidi...