Swala za sunnah na faida zake

Swala za sunnah na faida zake

Swala za sunnah na faida zake

Kusimamisha Swala za Sunnah



Baada ya Swala tano za faradhi, kuna swala nyingine za nyongeza alizozisimamisha Mtume (s.a.w) na akatuagiza nasi tumuigize. Swala hizi za ziada tunaziita Swala za Sunnah (Nawafil).



Lengo la Swala za sunnah ni lile lile la swala za faradhi la kututakasa na mambo maovu na machafu. Ni muhimu kwa kila Muislamu kudumisha hizi swala za Sunnah kwa sababu zifuatazo:



1.Kusimamisha Swala za Sunnah ni katika kumtii na kumuigiza Mtume (s.a.w), jambo ambalo ametuamrisha Allah (s.w) katika Qur-an:
2.Kusimamisha swala za sunnah kutatupelekea kufikia ucha Mungu kwa wepesi.


3.Swala za Sunnah pia zina kazi ya kujaziliza swala za faradhi ambazo kwa sababu ya udhaifu wa kibinaadamu hazikuswaliwa kwa ukamilifu unaostahiki.Kama tunavyojifunza katika Hadithi zifu atazo.



Imesimuliwa na Abu Hurairah (r.a) kuwa Mtume wa Allah amesema: Amali ya kwanza atakayoulizwa mtu siku ya Kiyama (siku ya Hukumu) ni Swala. Swala zake zikiwa zimekamilika atafuzu. Swala zake zikiwa pungufu atafeli na kuhasirika. Kama swala zake za faradhi zitakuwa zimepungua, Allah (s.w) atasema angalia kwa mja wangu kama anaswala za ziada (Sw ala za Sunnah) ili zichukuliwe kujazia sehemu iliyopungua katika sw ala za faradhi. Kisha ndio vitendo vyake vingine vitaangaliw a kwa namna hiyo hiyoโ€. (Tirmidh, Abu Daud, An-Nasai, Ibn Majah na Ahm ad).



Swala za Sunnah ni nyingi. Muislamu anatakiwa, kila atakapohisi kuhitajia msaada wa Allah (s.w) atatawadha na kuswali kwani Allah (s.w) anatuagiza:


โ€œJisaidieni (katika mambo yenu) kwa kusubiri na kuswali, na kwa hakika jambo hilo ni gumu isipokuwa kwa wanyenyekevu. Ambao wana yakini ya kwamba watakutana na Mola wao na watarejea kwakeโ€. (2:45-46)



Hata hivyo katika kitabu hiki tutajihusisha na Swala maalum za Sunnah zifuatazo:




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views: 3569

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 kitabu cha Simulizi     ๐Ÿ‘‰2 Simulizi za Hadithi Audio     ๐Ÿ‘‰3 Madrasa kiganjani     ๐Ÿ‘‰4 Dua za Mitume na Manabii     ๐Ÿ‘‰5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     ๐Ÿ‘‰6 Kitabu cha Afya    

Post zinazofanana:

Sifa za imamu wa swala ya jamaa

Post hii inakwenda kukupa sifa za imamu wa msikitini anayepasa kuswalisha swala ya jamii.

Soma Zaidi...
Hii ndio hutuba ya ndoa ya kiislamu

Hapa utajifunza utaratibu wa hutuba ya ndoa ya kiislamu. Sharti za jutuba ya ndoa na jinsibya kuozesha

Soma Zaidi...
Swala ya tarawehe jinsi ya kuiswali

Post hii itakwenda kukufundisha kuhusi swala ya tarawehe, faida zake na jinsi ya kuiswali.

Soma Zaidi...
Watu wanaolazimika kufunga mwezi wa Ramadhani

Hapa utajifunza watu ambao wanalazimika kufunga mwezi wa Ramadhani.

Soma Zaidi...
Kwanini lengo la funga halifikiwi na wafungaji wengi

Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...