Muislamu anapoingia Msikitini kabla hajakaa anatakiwa aswali rakaa mbili za maamkizi ya msikiti, Tahiyyatul-Masjid.
2.Swala za Qabliyyah na Ba’adiyah
Swala hizi za Sunnah huswaliwa kabla na baada ya swala za faradhi. Swala hizi zimegawanyika katika mafungu mawili, zile zilizokokotezwa sana, Mu’akkadah na zile ambazo hazikukokotezwa sana, Ghairu Mu’akkadah.
Sunnah ambazo ni Mu’akkadah ni zile ambazo Mtume (s.a.w)
hakuacha kuzitekeleza hata mara moja katika hali ya kawaida. Ghairu Mu’akkdah ni zile sunnah ambazo wakati mwingine Mtume (s.a.w) aliacha kuzitekeleza. Swala za Sunnah za Qabliyyah na Baadiyah zilikokotezwa (zilizo Mu’akkadah) na zisizo kokotezwa (zilizo Ghairu-Mu’akkadah) zimebainishwa katika jedwali ifuatayo ikiwa ni pamoja na idadi ya rakaa ya swala hizo:-