Menu



Lengo la swala

Lengo la Kusimamisha SwalaBila shaka swala imepewa umuhimu mkubwa kiasi cha kufanywa nguzo kubwa ya Uislamu kutokana na lengo lake.

Lengo la swala

Lengo la Kusimamisha Swala
Bila shaka swala imepewa umuhimu mkubwa kiasi cha kufanywa nguzo kubwa ya Uislamu kutokana na lengo lake. Lengo la swala limebainishwa katika Qur-an kama ifuatavyo ”Soma uliyoletewa wahyi katika kitabu (Qur-an) na usimamishe swala. Bila shaka swala (ikiswaliwa vilivyo) humzuilia (mwenye kuswali na) mambo machafu na maovu, na kwa yakini kumbuko la Mwenyezi Mungu (lililomo ndani ya swala ni jambo) kubwa kabisa (la kumzuilia mtu na mabaya). Na Mwenyezi Mungu anayajua mnayoyatenda.” (29:45).

Kutokana na aya hii tunajifunza kuwa lengo la kusimamisha swala ni kumtakasa mja na mambo machafu na maovu. Kwa maana nyingine, tunajifunza kuwa swala ikisimamishwa vilivyo, humfanya msimamishaji awe mtu mwema mwenye kutakasika na mambo machafu na maovu na mwenye kuendea kila kipengele chake cha maisha kwa kumtii Allah (s.w).

Labda tujiulize swali: Ni nguvu gani au ni msukumo gani uliomo katika swala unaomfanya mwenye kuswali atakasike na maovu na awe na tabia njema anayoridhia Allah (s.w) Linaloleta mabadiliko haya makubwa katika tabia na utendaji wa Muumini, ni lile kumbuko la Allah (s.w) lililomo ndani ya swala. Kwa hiyo lengo hili la swala litapatikana tu pale mwenye kuswali atakapokuwa na mazingatio na kumkumbuka Allah (s.w) katika kila hatua ya swala.


                   

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea

Ndio     Hapana     Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Main: Post File: Download PDF Views 754

Share On:

Facebook WhatsApp

Post zinazofanana:

mgawanyiko katika quran

MGAWANYIKO KATIKA QURAN Juzuu, Sura, Aya, Manzil, Qara Wataalamu wa elimu za Qurani katika fani za uandishi na usomaji wameigawanya Qurani katika mafungu ili kuwezesha urahisi kwa wasomaji wa qurani.

Soma Zaidi...
Umuhimu wa ndoa na kuoa ama kuolwa katika jamii

Matamanio ya jimai ni katika maumbile na hayaepukiki.

Soma Zaidi...